www.bible-teaching.dk

  Index


  

                                                                                                                          aug. 2006

  Water Baptism

                                                                                                            

 

Ubatizo kwa maji

Vagn Rasmussen

 

 

 

 

 

Ubatizo kwa maji.

 

Yesu akasema: Yohana 3:5. Yesu akamwambia, "Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuona ufalme wa Mungu."

Ubatizo wa bwana wetu Yesu Kristo:

Mariko Mtakatifu 1:9 Siku hizo, Yesu alifika kutoka Nazareti, mji wa Galilaya, akabatizwa na Yohane katika mto Yordani.

Kila aminiye ameitwa kufuata Yesu. Yesu ndiye mfano wetu mkuu. Kama wafuasi wa Yesu Kristo, tunapaswa kumfuata Yesu hata katika ubatizo na kwa jinsi hiyo, ya kubatizwa kwenye maji mengi. Yesu alibatizwa katika mto yordani kwenye “maji mengi”

 

Yesu aliamuru wafuasi wake ( na wote waliamini baada yao) kufanya vivyo hivyo:

Mariko Mtakatifu 16:15-16 Basi, akawaambia, "Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu v16, Anayeamini na kubatizwa ataokolewa; asiyeamini atahukumiwa, v17, Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya......

 

Ubatizo kwa siku ya Pentecost:

Matendo ya Mitume 2:38, Petro akajibu, "Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile zawadi ya Roho Mtakatifu.

 

Kutubu dhambi huja kabla ya ubatizo kwa maji. Anayebatizwa lazima atubu dhambi na kusamehewa kwanza kabla ya kubatizwa.

Ubatizo si shauri la kuondoa uchafu mwilini, bali ni ahadi kwa Mungu inayofanyika katika dhamiri njema. 1 Peter 3: 21. Kuzaliwa mara ya pili hutokana na toba sio ubatizo. „Kuzaliwa mara ya pili“ ni tendo la kiungu wala si la binadamu.

 

Mifano ya ubatizo wa maji katika bibilia:

Ubatizo wa Mwedhiopia. Acts 8:38-39. Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo ofisa wakashuka majini, naye Filipo akambatiza.      V39, Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake akiwa amejaa furaha.

Nyumba ya Lydia.Acts 16:14-15.

Askari wa gereza. Acts 16:25-33 hasa msitari wa 33.

Kwa Cornelio. Acts 10:47

 Mawaidha na mafundisho juu ya ubatizo.

Katika ubatizo, utu wa kale huzikwa. Kubatizwa kwa maji ni dhihirisho wa kufa na kufufuka.

Col.2:12, Maana, mlipobatizwa mlizikwa pamoja na Kristo, na katika ubatizo, mlifufuliwa pia pamoja naye kwa imani yenu katika nguvu ya Mungu ambaye alimfufua Kristo kutoka wafu.

Romans 6:4, Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya.

Ubatizo sio kuondolewa kwa uchafu wa mwili, bali ni kufanya agano na Mungu kwa dhamiri safi. 1 Peter 3:21….ambayo yalikuwa mfano wa ubatizo unaowaokoa ninyi sasa. Ubatizo si shauri la kuondoa uchafu mwilini, (bali ni ahadi kwa Mungu inayofanyika katika dhamiri njema) Huwaokoeni kwa njia ya ufufuo wa Yesu Kristo.

 

Mtu hubatizwa mara moja tu.

Ephesians 4:5, Kuna Bwana mmoja, imani moja na UBATIZO MMOJA;

Ubatizo haitaji kudhihirishwa, kwa mfano na karamu speshieli ama karamu ya kuhidhinishwa. Kunyanyushiwa maji kwa uso kwa watoto wadogo haikubaliki kama ubatizo wa kibibilia.

 

Kwa nini ubatizo?

Yesu kwa hakika alituamuru tubatize wanaokoka.

Mathew 28:19-20, Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu, v20, Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni……

Lini waweza kubatizwa?

Mradi mtu hakika ameokoka na anakiri Yesu Kristo ni bwana, anaweza kubatizwa. Katika kitabu cha matendo ya mitume, tunapata kwamba watu waliweza kubatizwa mara tu walipo okoka.

 

Soma pia:

Acts 8:36-37…Kuhusu mhasi wa Edhiopia

Acts 10:47-48…Cornelio

Acts 16:33..Askari wa gereza macedonia.

Mtu anyetaka kubatizwa lazima mwenyewe  amini yesu Kristo ni mwana wa mungu na ni mwokozi na bwana wake. Huu tu, ndio ubatizo wa waumini. Hivyo basi, watoto wachanga na wadogo hawastahili kubatizwa, kwa maana hawaitaji wala hanana uwezo wa kuamini. Bibilia haidai ukomavu wa aina fulani ama kwa muda fulani kama kanuni.

 

Jinsi ya kubatizwa 

Baada ya kupata mafundisho sahihi ya kibibilia, yule wa kubatizwa aweza kubatizwa kwa maji mengi. Ubatiso waweza kufanyika nje, mahali ambapo pana maji ya kutosha. Makanisa mengine wana beseni maalum ya kuweza kuweka maji mengi ya ubatizo.

Dhehebu zingine hupeana kasiki maalum ya kuvaliwa na walio batizwa kwenye sherehe za ubatizo.kasiki sio lazima. Kaniza nzima ina shiriki na uadhimishaji ni siku ya kusherekea.

Walio batizwa wakaribishwa kanisani kama washirika wapya ambao wameongezeka kanisani. Kwa kawaida ni mchungaji ama mmoja wa wazee kanisani waweza kubatiza.

Ni mchungaji ama viongozi ndio wanaostahili kufundisha somo la ubatizo kwa  wanao batizwa kabla ya kuadhimisha ubatizo.

 

Jinsi ya kubatiza 

Baada ya yule anayebatizwa kukiri imani yake katika Yesu Kristo, Anaweza kuingia majini pamoja na yule anaye batiza. Baada ya maombi fupi kwa anayebatizwa, mbatizaji atasema: “ Ninakubatiza wewe…………..(jina la anaye batizwa) kulingana na imani yako na kukiri kwako, nakubatiza kwa Yesu Kristo, katika jina la baba, la mwana, na la Roho mtakatifu.

 

Ilani,wanaobatizwa hawabatizwi kwa chama fulani, wala KATIKA jina la yesu, bali ni kubatiza kwa Yesu Kristo, katika jina la baba, la mwana na la Roho mtakatifu.

Baadaye, waliobatizwa wanaombewa na kukaribishwa kwenye umati kama washirika.

 

Kanisa ina paswa kutoa cheti, andiko la kudhibitisha, kwamba aliyebatizwa amepokea ubatizo wa kibililia.

 

Katika kanisa ya kale, watoto hawakuwa wanabatizwa. Katika karne ya pili- tatu baada ya Kristo, makanisa mengine waanza kubatiza watoto kwa kuchovya kwa maji baridi. Punde makanisa mengine wakaanza kunyunyiza maji. Mwishowe, kanisa la kiroma wakabatiza watoto. Makanisa la Lutheran pia na makanisa ya injili wakafuata ubatizo huo. Ushirika na wokovu ikawa katika ubatizo. Toba haikutiliwa mkaso kwa mtu kuwa mshirika wa kanisa.