Index                                                         update 26. feb. 2008

 

 

WAFUNAJI WA NAFSI ABC

    By Vagn Rasmussen     Translation by Lydia Madsen

 

 

 

                                                                                                                                                                                                                     

 

Wafunaji wa nafsi ABC

 

Mark 16:15-20  

                             Huduma/uiinjilisti

Wakristo wachache sana wameitikia mwito wa Bwana

Wakristo wengi sana hawajawahi kuelewa mipango ya Mungu maishani mwao.

Wao ni watoto wa kiroho maishani yao yote.

Sababu hii inamhusunisha Roho Mtakatifu mbali na maisha ya wakristo wengi-kukosa kuingia katika mpango wa Mungu, kuitikia mwito wa Mungu na kupokea maono.

Wahuduma wa kweli wana mwito wa kiungu na maono ya kiungu kusimamisha huduma zao.

Ni wangapi wenu wamewahi muongoza mwenye dhambi mmoja katika toba?

Ni wangapi wenu wataingia mbinguni mikono mitupu?

Ni wangapi wamemshuhudia Bwana kwa mwenye dhambi?

Ni wakristo wangapi wanaionea aibu injiri ya Yesu Kristo? Na hawadhubutu kumukiri Kristo kwa wenye dhambi?

Unamsikia mtu akiomba kwa machozi na ushungu mwingi akiwa hospitalini, madaktari wamenyosha mikono na akapewa muda mfupi kama siku kumi na nne za kuishi, akaomba maombi haya ya uchungu: “Bwana, kama utanipona, BASI nitaenda na kuhubiri neon lako mahali popote utanituma.”  Alifariki kabla ya siku kumi na nne.  Kwa nini?  Roho Mtakatifu ameshahusunishwa muda mrefu uliopita.  Imani imeondoka kitabo sana.

 

 

 

 

 

 

 

 

William Booth mwanzilishashi wa Njeshi la Wokovu, alitabiri katika miaka yake ya mwisho:

Katika siku za mwisho kutakuwa:          Ukristo bila Roho Mtakatifu,

                                                                 Wokovu bila toba,

                                                                 Wokovu bila kugeuka,

                                                                 Mbinguni bila kusimu,

                                                                 Ukristo bila Yesu

                                                                

 

 

Kuwa mtu wa kufuna mioyo/nafsi......

Ukitaka kufanikiwe kwa kuleta watu kwa Yesu lazima uwe na huruma kwa waliopotea na wenye dhambi.

Yesu anataka kuokoa kila nafsi aliyeiumba!

 

Twaweza kuwa wafunaji wa nafsi kwa njia nyingi.

1.  Unaweza kuwaombea wenye dhambi ili waokoke.

2.  Hali ya kuwasiliana kibinafsi(ana kwa ana)

3.  Unaweza kuwakarimbisha watu kwa mkutano wenye nguvu za roho mtakatifu.

4.  Unaweza kumtuma muhubiri katika kuhudumu kwa pesa zako.

5.  Unaweza kueneza injili kwa nyimbo na musiki.

6.  Unaweza kupeana vitabu, vijitabu, masomo ya kikristo ama kuwakaribisha watu kwa ibada.

7.  Unaweza kuelezea watoto njia ya wokovu na kuomba nao maombi ya toba.

8.  Unaweza kufanya mikutano ya nje ya injili na kupitisha habari za wokovu.

9.  Unaweza kuitikia Matayo 28. na Mariko 16:

Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

huburi injiri kwa mataifa yote, hata majirani wako, mnaofanya kazi pamoja, wandugu na wageni wote walio katikati yenu.

 

Kuna Uwezekano na hali nyingi mno.

Jivishe silaha zote za Mungu.

Silaha za Mungu ni  Waefeso 6:13-18  Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti. Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.  Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu. Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.

 

 

 

 

 

 

 

 

Kuna mambo matatu ya kumwambia mwenya dhambi:

a)  Yesu anawapenda watu wote.

b)  Yesu anaweza kusamehe dhambi zote – kama mtu akitubu na kukiri.

c)  Yesu yu karibu kurudi

 

Ongea neno la Mungu, hasa AGANO KUMI.

Muelezee kuhusu upendo wa Mungu na pia haki yake.

Mwamini Roro Mtakatifu kudhimbitisha yale unayoyasema.

Shuhundia kwa jinzi ile mwenye dhambi ataguzwa na kutabua dhambi zake.

 

Jifunze jinzi ya kuongoza mwenye dhambia kwa maombi ya toba, akirudia baada yako.

Wacha arudie mombi yako mustari baada ya mwingine.

 

Hapa kuna dokezo:

Bwana Yesu – Naja kwako vile nilivyo – natubu dhambi zangu – Nakiri ya kuwa mimi ni mwenye dhambi – Yesu naomba unisamehe dhambi zangu zote – Naomba uiokoe nafsi yangu – nipe Roho wako Mtakatifu aishi ndani yangu.  Nayatoa maisha yangu kwako – Nakushukuru kwa uzima wa milele. Amen.

 

Maneno ya muhimu, vunguo katika maombi ya toba:

Kutubu dhambi – kukiri dhambi.

Kumuomba Yesu msamaha kwa dhambi zote za kale.

Kumuomba Yesu aokoe nafsi yake.

Kusalimisha maisha kwa Yesu Christo kama Bwana.

Kumshukuru Yesu kwa ajili ya wokofu na uzima wa milele.

Pokea kwa imani.

 

 

HARAKATI ZA WOKOVU

1) Utambuzi wa dhambi

2)  Kutubu dhambi

3)  Kuasha dahmbi – wengi watatambua dhambi zao, lakini hawataACHA na kuzikana kabisa 100%

4)  Uazimaji

  Hatua zote nizamuhimu ama muumini mpya atarudi myuma haraka sana.

 

 

 

 

 

Himiza muumini mpya:

1)  Kutoa ushuhuda wa wokovu kwa watu, ama mtu nakumwambia ati amefanyika muumini/mkristo.

2)  Muhimize asome biblia kila siku.  Hakikisha ati wana bibilia. Neno la Mungu ni mkate wa kila siku wa nafsi zetu.

3)  Elezea umuhimu wa kumwomba Yesu kila siku.  Maombi ni kwa ajili ya nafsi kama vile kuvuta hewa safi ni kwa ajili ya mwili.

4)  Kuwa na ushirika na wakristo wengine angalao mara moja kwa wiki, kuhudhuria ibada za kaniza.  Kuwa mshiriki wa kanisa.

5)  Uungana wa kikundi cha waombezi/mikutano ya nyumba katika ya wiki.  Siku saba katoka ibada ya juma pili ni muda mrefu sana kwa muamini mpya.

6) Muhimize asome fasihi zuri za kikristo, ikiwezeka mpatie vitabu vizuri ama casseti za nyimbo zenye zimenjaa Roho Mtakatifu.

 

 

Wakati mwingi habari za wokovu huhubiriwa bila kutaja ubatizo wa Maji, na mara moja moja hutaja kuhuzu ujazo wa Roho Mtakatifu.

Vijitabu vingi, kama vipo, HAVITAJI kuhusu ubatizo wa maji na ubatizo wa Roho Mtakatifu.  Mtume Peter katika kuwahubiria wenye dhambi katika siku ya Pentekosti alisema:

 

 (Matendo ya mitume 2:38) Petro akajibu, "Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile zawadi ya Roho Mtakatifu.

 

Maandiko ambayo ni fungua kuhusu wokovu:

Matendo ya mitume 2:21 Hapo, yeyote atakayeomba kwa jina la Bwana, ataokolewa.`

 

Matendo ya mitume 4:24 Waliposikia habari hiyo waliungana pamoja katika kumwomba Mungu wakisema, "Bwana, wewe ni Muumba wa mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo!

(Jina Yesu kwa kihibrania ni Yeshua, kumaanisha wokovu.)

 

Matendo ya mitume 16:31 Wao wakamjibu, "Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa pamoja na jamaa yako yote."

 

Warumi 10:9 Kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka wafu, utaokoka.

 

Warumi 10:10 Maana tunaamini kwa moyo na kukubaliwa kuwa waadilifu; na tunakiri kwa midomo yetu na kuokolewa

 

Yohana 6:37 Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,

 

Warumi 3:23 Watu wote wametenda dhambi na wametindikiwa utukufu wa Mungu.

 

Yohana 3:16 Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

 

 

Umuhimu wa kunena neon la Mungu, Amri Kumi:

Uinjilisti

1) Injili ya upendo, furaha na amani? Ama – kuhubiri sheria, amri kumi, njia mzuri ya kushawishi kuhusu dhambi, haki na hukumu!

2)  Peana mwaliko wa wokovu wakati wenye dhambi wameshawishika na usiWASUKUME, ama utawafuna wenye kurudi nyumba wakati kanuni lako ni kuwafuna wanafunzi.

80% ya wale waliofanya uamuzi kwa Yesu wanarudi nyuma kwa sababu ya injiri mbaya ya siku mbili. 

Kanisa limenjaa waliorudi nyuma, kwa sababu wengu waliorudi nyuma walitoka kanisa baada ya muda mfupi lakini bado wengi waliendelea kukaa kanisani wakiwa wamerudi nyuma kisiri.

3)  Mahubiri ya kubeba-msalaba, kujikana-mwenyewe na utakatifu lazima iambatane na injili ya Sheria ya Mungu – ama wasikirisaji wako wataendelea kukosa MAANA ya dhambi!

Kusudi la sheria ya Mungu (TORA) ni hatua nne:

                            

 

1)  Kuonyesha ulimwengu HATIA yao mbele za Mungu.

2)  Kupeana ELIMU kuhushu dhambi

3)  Kuonyesha  KILINDI cha dhambi zetu.

 

4)  Kuwa MKUU WA SHULE kutuongoza wa Kristo.

5)  Kusukuma watu wajitoe? – Usifanye! 

Bila kushawishika kwa ajiri ya dhambi 80 -90 % watarudi nyuma baada ya muda mfupi!

 

6)  Ni muhimu sana:  Sheria ya Mungu lazima ihubiriwe kabla ya uamuzi wowote.

Hiyo ndiyo sababu ni mafuno kidogo tu inatokana na uinjilisti wa siku hizi na mahubiri na kushuhudia kuhusu Yesu.

 

7)  Mithali 11:30  Mwenye hekima huvuna nafsi: “inachukua hekima kuvuna nafsi”!

Mwaliko usiofaa, unaowaahidi maisha ya ukristo yenye raha, wakati watu wanafanya uamuzi kutokana na HIZIA: uamuzi wa namna hii haudumu kwa muda mrefu.  Watu wengine hufanya uamuzi na kutafuta wokovu kwa anjili ya HOFU ya kwenda jehanamu. Hii pia ni uamuzi kwa jinzia mbaya.  Uamuzi wa kweli na wakudumu ni ule unaeletwa kwa kushawishika kindani kuhuzu dhambi

Kupitia udhimbitisho mkuu wa Roho Mtakatifu.

 

8) Mwaliko wa wokovu mbaya utawafanya watu kugeuka bali na Ukristo!  Waliorudi nyuma watageuka kinyume na habari za wokovu hata zaidi.

9 kati ya 10 ya uamuzi wa siku hizi unatokana na HIZIA ama HOFU na SIYO kwa anjili ya kushawishika kwa undani kwa anjili ya dhambi!

 

9)  Mwenya dahambi lazima AELEWE  dhambi zake, kinyonge, na hudumu yake.  Nikupitia tu mahubiri kuhusu sheria ya Mungu yaweza kuonyesha haya.  Roho Mtakatifu atadhihirisha sheria ya Mungu inayohubiriwa.  Roho Mtakatifu hawezi dhimbihirisha kanuni tu za kibinadamu zikihubiriwa.  Ni sheria Ya Mungu tu ambayo ina kipimo dhambiti kuhuzu nini dhambi!

 

10)  Finney alisema: “Natia nguvu eti sheria (ya Mungu) ndiyo amri na amri pekee ambayo inaweza pima hatia ya dhambi.

 

11)  Finney alikuwa na 20% waliorudi nyuma.  Mahubiri yake yalileta uamuzi uliyofanya waaumini kuweka mizizi yao ndani kwenya neneo la Mungu na hivyo hawakurudi nyuma.  Majaribu na matezo yaliwafanya waumini wapya KUKUA tu.

Ndini ya mafanikio na “ndini ya raha” wongofu unaotokana na ahadi za uongo na nia mbaya inawafanya hao waliorudi nyuma kuwa na hasira na uchungu kwa Mungu na wanadamu.

 

12)  Angalia kama waumini wana matunda.

Wale walio na uongofu usiyo wa kweli hawatakuwa na matunda.  Hawajapitia mlango, ambao ni Yesu Kristo.

 

13) Sheria ya Mungu ni kali zaidi ya sheria na kiwango cha mwandamu.

Sheria za Mungu zimeandikwa kwa mioyo yetu, Wayahudi na watu wa Mataifa wanajua yaliyo mema na mabaya.  Hata kabila zenye hazinjasoma za kiafrika wanayo sheria ya Mungu mioyoni mwao, “Usiue”  “Usiibe”

 

14)  Kama tunamaanisha kuufikia ulimwengu kwa Mungu, LAZIMA turundie kanuni za uinjilisti na mahubiri ya kibiblia na kuleta wazi sheria ya MUNGU.  Yesu hakuja kuondoa sheria katika kanisa la agano njipya, alikuja KUTIMIZA sheria.  Amri kimi zimeandikwa na barua ya upendo katika mwiyo yetu iliyozaliwa mara ya pili.  Yesu alitupatia hali ya uungu wake kuishi katika roho zetu.  Mtu asiye na Roho wa Kristo hana uhusiano NAYE. Yesu Kristo alituachia sheria kupitia kwetu na ndani yetu.

 

15)  Sheria inahimiza kuhuzu dhambi.

Roho mtakatifu anadhimbitisha tu kuhubiriwa kwa Amri kumi, sheria ya Mungu na neno la Mungu.

Kuhubiri tu

 

16)  Sheria inazaa kuelewana.

The unawake sinner will not seek God until he understands his true condition before his Creator.

Mkristo ambaye amelala hatamtafuta Mungu mpaka aelewe hali yake ya kweli mbele za Muumba wake.

Warumi 3:11

Mungu anataka wenye dhambi wafundishwe ili waweze kuelewewa.  Matayo 28:19-20...Kwa hivyo YAFUNDISHE mataifa yoe.....

Hosea 4:6  Watu wangu wanapotea kwa kukoza MAARIFA...

 

17)  Sheria inaweka wazi dhambi

Mt. 5:27-28 whoever looks at a woman to lust for her has committed adultery.

Matayo 5:27-28 "Mmesikia ya kuwa watu waliambiwa: `Usizini!`
Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.

Yesu anatia nguvu sheria,  Matayo 5:18  Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya Sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia.

 

18)  Sheria humtayarisha mwenye dhambi, humtayarisha kwa neema ya Mungu.

Luka 19:2  Zachayus alirurindisha mara nne – Alikuwa amesoma Kutoka 22:1 ....Kombee aliyeibiwa hurenjeshwa na kondoo wane.

 

 

19)  Sheria ni MKUU WA SHULE.

Sheria itawanyamazisha.  Baada ya kusikia sheria, hakuna mtu atakuwa na sababu zozote.

 

20)  Wesley alihubiri 90% sheria na 10% neema.

 

21)  Tukuhubiri jehanamu bila kuhubiri sheria,  watu watatubu na kujitoa kwa ajili ya HOFU na sio kwa sababu wamehizwa kuhusu dahmbi kwa kuhubiriwa sheria.  Gafla, waliyotubu kwa ajili ya hofu watarudi nyuma.

 

22)  Kuna upinzani mwingi sana katika mahubiri ya namna hii, yaani kuhubiri sheria na mashauri kamili ya Mungu.

Watu wanaopinga watakwambia usome barua za Paulo kwa Wagalatia ambao wanasheria.  Lakini ukweli wa mabo ni kuwa, Wagalatia wangejaribu kuokoa kwa matendo yao, kwa kuweka sheria na SIYO kwa kuhimizwa kuhusu dahmbi, toba, msamaha wa dhambi, na kwa damu Yesu inayosafisha.

 

23)  Melanchton alisema: “Lakini kuna wengi wanaoongea kuhusu msamaha wa dahambi, lakini hawazungumzi chochote ama kidogo tu kuhuzu toba.  Kama hakuna msamaha wa dhambi bila toba, basi toba haieleweki bila toba.  Kwa hivyo, kama kuna hubiriwa kuhuzu msamaha wa dhambi bila toba, inafuata mfano wa watu hao wamechapokea msamaha wa dhambi, na hivyo wahakuwa na ujasiri na bila hofu, ambayo ni dhambi na makoza makubwa sana kuliko yale yalitokea kabla yetu.

Wapendwa, twahitajika kubandiri msogeleo wetu kwa wenye dhambi na kuwaletea uhimizo unaota ndani ya moyo kwa kutumia sheria.

 Athiri ya kuhubiri sheria kwa wenye dhambi inatiwa nguvu sana na maombi ya uombezi kupitia athari ya Rohowa maombi.  Warumi 8:26  Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka

Zechariah 2:10  na nitamwaga katika nyumba ya Daudi.... Roho wa neema na MAOMBI na watanitazama, yule waliye chomeka na wataomboleza kwa ajili yake.......

 

Jinzi ya pokea Kwa wingi ROHO WA MAOMBI?  Jawabu ni lahizi sana, lakini yenye kumaanisha:  “Kujitoa kamili, kuchukua msaraba wako, kujikana mwenyewe, maisha safi na matakatifu, huruma kwa mioyo iliyopotea, kubandirisha  mtindo katika kufunga na kuomba.  Yesu alifunga na kuomba siku arobaiini kabla ya kusema:  Luke 4:18"Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,

Yesu Kristo alitayarisha huduma yake kupitia siku 40 za kufunga na kuomba.  Je twaweza kwa njia nyingine rahizi?

Bila ROHO WA MAOMBI hauwezi kumtumikia  Bwana kamiri.  Roho wa maombi akiwa ndani yake waweza kuwa chombo muhimu mikononi mwa Bwana kwa anjili ya wokovu wa maelfu na maelfu ya mioyo iliyopotea.  Ni haba sana kupata ROHO WA MAOMBI mwingoni mwa wakristo.

 

24)  Bila upako – hakuna matokeo.

Kama hautaomboleza katika maombi, utaomboleza katika kuhubiri (Ni vigumu kuhubiri bila upako, kama hautaomba ndani ya Roho akiomboleza kwa anjiri ya mioyo iliyopotea.

Bila roho wa maombi huwezi kufika mbali.  Kutumika katika Roho wa maombi utatimizi hata yale yasiyo wezekana.

 

25)  Mwaliko wa wokovu  kiurahisi – Usifanye!

Ripoti kutoka India yaonyesha mwitikio kwa wingi, lakini bila kudumu.  Utafitaji waonyesha kwamba karibi 100% wanarundi nyuma.  Hakukuwa na uhimizaji wa kweli wala ufuatiliaji wowote.

 

26)  Siyo uwamuzi mwema tu, lakini kuongolewa kwema.

Uamuzi mzuri hautoshi na hufanyika uongofu usiyo wa kweli, mwishowe huzaa wenye kurudi nyuma na machungu.

Kubandirishwa kuzuri kutokana na kuhimizwa kwa kindani kuhusu dahambi huzaa maisha mazuri ya Kristo yenye matunda.

 

27)  Hubiri injili bila uoga.

Wesley alikuwa ni muhubiri wa haki.  Aliinua utakatifu wa Mungu, sheria ya Mungu, haki ya Mungu, hekima ya mahitanji yake na haki ya gadhabu yake!

Halafu angewageukia wenye dhambi na kuwambia ukubwa na makoza yao, uwazi wao uliyo wazi, matokeo yake na dhawabu lake.

Nguvu za Mungu zingeshuka  kwa njia kuu saa, kwamba habari za kweli zasema kuwa, katika fursa moja, baada ya watu kuondoka, kulikuwa na watu 1800 waliyo lala chini kwa nguvu za Roho Mtakatifu wenye kuzimia kabisa kwa sababu walikuwa na ufunuo wa utakatifu wa Mungu, na hivyo walikuwa wameona ukuu wa dhambi zao!

Wesley alihubiri kanuni lote la Mungu na Mungu akabarika neon lililohubiri na ishara zikafuata.

 

28) Kubatizwa kwa moto.

Mhali popote niendapo huwapata wakristo waliobatizwa kwa Roho Mtakatifu lakini SIYO KWA MOTO!  Luke 3:16 Hapo Yohane akawaambia wote, "Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo zaidi kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

 

Hatua kumi za kushawishi wenye dhambi.

1.              Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

2.              Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.

3.              Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

4.              Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

5.              Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi.

6.              Usiue

7.              Usizini

8.              Usiibe

9.              Usimshuhudie jirani yako uongo.

10.          Usiitamani nyumba ya jirani yako.

 

Weka wazi sheria, amri kumi kwa mwenye dhambi – na walio rudi nyumba ambao wanajifisha nyuma ya ndini, na pia waliorudi nyuma nje ya kanisa.  Kuna wengi ambao siyo moto wala baridi na waliorudi nyuma ndani na nje ya madhehebu yote pamoja na wakristo, ambao ni wakristo tu kwa jina, na kwa hivyo siyo wakristo waliotubu!

Ni wale wahubiri, wainjilisti ambao wanaupako wa Roho Mtakatifu, wanaweza kuhubiri injili ya namna hii bila kusita.

Ili kufanikiwa na kutumika katika huduma ya namna hii, lazima iwe imeambatana na maombi mengi, utakazo, kujitoa na kujipeana kamili na unyenyekefu mbele za Bwana Yesu Kristo.

 

Mwelekeo wa wenye kufuna mioyo wanapowashuhudia wenye dhambi:

Mwinue Mungu na utakatifu wake

Hubiri sheria ya Mungu, kuweka wazi amri kumi.

Haki ya Mungu

Hekima ya mataranjio ya Mungu

Haki ya gadhabu yake.

 

Wageukie wenye dhambi:

Waambie ubaya wa hatia yao.

Uaazi wao

Adhabu yake

 

Onyesha upendo wa Yesu na uelekeze katika upendo wa Yesu Kristo na nguvu zake wakusamehe dhambi.

Ongeza picha ya Baba Mungu Baba, Mungu ni upendo.

 

Ona kama watu wemeshawishika kabla ya kuwalika mbele.

Ni dhambi zile tu ambazo zimekiliwa, kutubu na kuwachwa, ambazo zimesamehewa!

Mwenye dhambi ambaye hataacha dhambi zake, humhuzunisha Roho Mtakatifu na yuko katika hatari kubwa.

 

Mungu mkuu na ambariki kila mfunaji wa mioyo huko nje.  Kwa kweli zipo zawadi kuu ambazo zinakusubiri, ila, tuzifanye kazi kwa ajili ya zawadi, lakini wacha tufune mioyo ili tumpendeze Bwana wentu mpedwa Yesu Kristo na tuitikie mwito wake wa kuwa wafunaji wenye hekima.

Matayo 28:18-20 Yesu akaja karibu, akawaambia, "Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu; mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.Wafundisheni kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote; naam, mpaka mwisho wa nyakati."