Prayer of the Believer.

 


 Index

 

 

 

Utangulizi 

                                                                                                                    Shasisho la mwisho nov. 2005

 

     Maombi ya muumini

 

    Vagn Rasmussen

 

 

YALIYOMO:

 

MAOMBI YA MUUMINI:

 

1.              Maelezo

 

2.              Maombi na jina la Yesu

 

3.              Maombi na imani. Vizingiti mpya wa imani.

 

4.              Maombi na neno la Mungu.

 

5.              Maombi na Roho Mtakatifu.

 

6.              Maombi na kuabubu katika hekalu la kale.

 

7.              Maombi na ufufuo.

 

8.              Shule ya maombi.

 

9.              Bidii ya maombi.

 

10.          Maombi na kufunga.

 

11.          Maombi na kufukuza mapepo.

 

12.          Maombi na kufunga kwa Danieli (Afya)

 

13.          Maombi na Kuongozwa na roho. ( Njia 7 )

 

14.          Maomba katika chumba cha maombi.

 

15.          Maombi ya pamoja.

 

16.          Maombi katika umati.

 

17.          Maombi katika familia.

 

18.          Maombi na Nyimbo katika Roho

 

19.          Maombi na vibawa vya Roho Mtakatifu.

 

20.          Maombi na vita vya kiroho.

 

21.          Upingamizi katika maombi

 

22.          Uvumilivu katika maombi

 

23.          Maombi na upendo wa Mungu

 

24.          Maombi na uponyaji wa roho. Uponyaji wa hisia

 

25.          Maombi na uombezi. ( maombi ya uombezi )

 

26.          Maombi na utakatifu. Maombi na upako

 

27.          Maombi na kuugua kwa nafsi

 

28.          Maombi ya kufungua na kufunga

 

29.          Maombi na kuabudu miungu( Occultsm)

 

30.          Maombi ya kinabii

 

31.          Mikutano ya maombi na jinsi ya kuongoza

 

32.          Maombi na mapenzi ya Mungu. ( Jinsi ya kujua mapenzi ya Mungu )

 

33.          Maombi na huduma-Afisi maalum ya mitume, Maombi na neno.

 

34.          Maombi katika bibilia. Yesu, Danieli, Hannah, Daudi, Ayubu, Abrahamu, Musa, Jabez, Mfalme Hezekiah, Sulemani na umati wa Yerusalemu.

 

35.          Maombi kama huduma maalum. Anna Mnabii.

 

36.          Maombi na fungu la kumi. Malaki 3:10

 

37.          Maombi na kupakwa mafuta

 

38.          Kujazwa na Roho wa Mungu. Usafi wa kiroho

 

39.          Maombi na kutoa msaada. Matendo ya mitume 10

 

40.          Baraka na maombi katika bibilia. ( Baraka za Haruni, baraka za kitume

 

41.          Maombi na mahubiri

 

42.          Maombi, Ahadi za Mungu Katika bibilia na masharti ya majibu ya maombi

 

43.          Maombi na shukrani kwa Mungu siku zote

 

44.          Roho ya neema na mahitaji

 

45.          Maombi na kuabudu katika wimbo

 

46.          Maombi ya Kujenga

 

47.          Maombi na ubatizo katika moto

 

48.          Maombi na majaribu

 

49.          Maombi na utukufu wa Mungu

 

50.          Mbinu za maombi, maombi na kufanya maombi

 

51.          Kupuuza maombi.

 

 

 

 

 

1. MAELEZO

Maombi ni mawasiliano na Mungu.

Maombi hubadilisha tabia yetu na utu wetu kwa uwema.

Inavunja ubinafsi wetu.

Maombi huzaa nguvu.

Maombi hufungua mlango kwa ghala la Mungu.

Maombi itakupa utawala juu ya Shetani.

Maombi ni kuwa na Mungu, kuwa na ushirika naye.

Maombi ni kufanya kazi na Mungu.

Mungu anategemea maombi yako. Dhibitisho: Ez.28:30-Mungu Yahweh anatafuta mtu anayeweza KUSIMAMA KWENYE PENGO. Lakini hajapata mtu.

 

                             2. MAOMBI NA JINA LA YESU.

Yohana Mtakatifu 14:13, “Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.”

Yohana Mtakatifu 15:16, “Ninyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapa ninyi chochote mumwombacho kwa jina langu.”

Yohana Mtakatifu 16:23-24, “Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni. Ms 24, Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.”

 

Tazama hamjauliza lolote kwa jina langu, Ulizeni nanyi mtapokea, ili furaha yenu iweze kukamilika.

 

Yohana Mtakatifu 16:26, “Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu;

 

Hamtaweza kuja kwa baba kwa jina lenu, ametupa jina lake Yeshua, Yesu ametupa jina lake, ili tuwaponye wagonjwa, tutoe mapepo na kwa hakika pia kwa KUOMBA kwa jina la Yesu kristu lenye baraka.

 

Baba na jamii yake:

Baba anapendezwa kuwapa watoto wake chochote na kila kitu ambalo kwa hakika tuna imani kwalo na pia kuliulizia.

 

Kila muumini aliyezaliwa mara ya pili ni mmoja wa jamii ya Mungu.

 

 

 

                             3. MAOMBI NA IMANI. ( uchambuzi mpya wa imani. )

Mambo mawili muhimu katika maombi ni, 1) Roho Mtakatifu

                                                                      2) Imani.

 

Kama vile moto itahitajika kuteketesa, Roho Mtakatifu anahitajika kwa maombi.

 

a)      Tunapataje imani?

b)       Imani ni nini?

c)      Imani na tumaini

d)      Imani na hisia

e)      Inamaanisha nini kuamini kwa moyo?

f)       Kukiri – ni ufunguo wa imani.

g)      Kukiri hurejesha uhusiano uliovunjika.

-Kukiri raha ya muumini katika Kristu

-Kukiri ya hakika na sio ya hakika

-Imani ya ufanisi

-Adui wa imani

-Imani itokanayo na Mungu

 

a)    Tunapataje imani?

Warumi 10:17,“Hivyo basi, imani inatokana na kuusikiliza ujumbe, na huo ujumbe unatokana na neno la Kristo.

Imani huja kwa moyo wako kwa kusikia neno la Mungu ( kusoma neno la Mungu )

Soma bibilia kila siku, shika ahadi za mungu katika bibilia.

Imani pia huja kwa kuifanyia kazi kiwango cha imani uliyonayo tayari. ( kila mmoja ana kiwango cha imani kutoka kwa Roho mtakatifu.)

Warumi 12:3, ...Fikira zenu na ziwe na kiasi kufuatana na KIPIMO CHA IMANI Mungu aliyomgawia kila mmoja.

 

Imani ina SEHEMU KATIKA ROHO MTAKATIFU. Unapojazwa zaidi, ndivyo imani inaongezeka.

2 Wathesalonike 1:3, .............kwani imani yenu inakua sana......

 

Imani yetu waweza kukua. Tunatumia imani tulio nayo, kupitia majaribu katika hali zetu za kawaida. Kama vile mtoto anapotumia misuli anakuwa mwenye nguvu, pia nasi tunakuwa wenye nguvu katika imani tunapoifanyia kazi.

Kila mmoja ana kiwango cha imani. Warumi 12:3,..... kufuatana na kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja.

 

 

 

b)    Imani ni nini?

 

Hebrania 11:1, ”Kuwa na imani ni kuwa na hakika ya mambo tunayotumainia; kusadiki kabisa mambo tusiyoyaona.”

 

Imani ni bayana. Anga tunayoiona haikuumbwa bure, bali ni kutokana na BAYANA, iliumbwa kutokana na VITU VISIVYO ONEKANA.

Imani ni chanzo ambacho inaweza kubadilisha hali kutokana na visivyo onekana hadi vile vinavyo onekana.

 

 

c)     Imani na tumaini

 

Tumaini ni kwa usoni. Imani inajua kile tayari inalo. Ni uhakikisho, ni kwa muda tu, hadi litakapo onekana. Mariko Mtakatifu 11:24, “Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa.”

 

                      d) Imani na hisia

 

Dhihirisho ya imani uliyonayo kwa jambo ambalo umeiombea sio HISIA yoyote ya nguvu unayosikia, bali dhibitisho ya kwamba umepata jibu la maombi yako ni kuwa na amani. Ni kule kuwa na imani katika neno la Mungu na ahadi zake. Usitegemee hisia zako, inaweza kwa ghafla kugeuka kuwa mabaya. Liamini neno la mungu na amani moyoni itasimama kama mwamba wakati imani inajaribiwa.

 

 

e)     Inamaanisha nini kuamini kwa moyo?

Mariko mtakatifu 11:23, “Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: `Ng`oka ukajitose baharini` bila kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika, atafanyiwa jambo hilo.”

Kwa moyo unaamini, sio kwa mawaso. Unaweza kuwa na vita vya ajabu kwa mawaso yako na uwe na amani na imani moyoni mwako kwa muda huo huo! Hivyo basi inua imani yako cm 30 kutoka kwa akili yako hadi kwa moyo wako. Shetani anaweza tu kuvamia akili yako, mawaso yako lakini sio roho yako, ambayo iko ndani ya moyo wako.

 

 

f)      Kukiri – ni ufunguo wa imani

 

Mariko mtakatifu 11:23-24,…..Amini ya kwamba vitu ambavyo AMESEMA itatima, mtapata lolote ASEMAVYO.

Warumi 10:10, “Maana tunaamini kwa moyo na kukubaliwa kuwa waadilifu; na tunakiri kwa midomo yetu na kuokolewa.”

Kukiri neno la mungu huongeza imani! Kuubiri neno la Mungu, Maombi, Kufunga na zaidi kujazwa kwa roho mtakatifu huongeza imani pia.

 

 

                      g) Kukiri hurejesha uhusiano uliovunjika.

Mariko mtakatifu 11:25, “Mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu.*fg* hata Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu."

 

 

-         Kukiri raha ya muumini katika kristu.

 

 2 Wakorinto 5:17, “Mtu yeyote akiungana na Kristo huwa kiumbe kipya, mambo ya kale yamepita, hali mpya imefika”

 

Hiyo ndio kukiri iliyo bora. Ni mabadiliko kamili katika maisha ya mtu.

 

- Kukiri ya hakika na yenye sio ya hakika 

2 Timoteo 1:7, “Kwa maana Mungu hakutupa Roho wa kutufanya tuwe waoga, bali alitupa Roho wa kutujalia nguvu, upendo na nidhamu.”

Usi kiri hofu na kutoamini katika maombi yako, bali kiri kile neno la Mungu linasema.

 

- Imani na ufanisi

3 Yohana 1:2, “Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni.”

Kumbumbu la torati(Deut) 28:1-12,……utabarikiwa……

Hapa Mungu amenakili mambo mengi ambayo bwana atatubariki ikiwa tutamtii na kuweka imani yetu kwa matendo.

 

- Adui wa imani

Shetani ni adui wa kwanza. Ataweka imani yako kwenye majaribu tena anajaribu kutoa imani yako kwa kuleta majadiliano na hisia zetu za kawaida.

 

Miango za maarifa (senses) – miango zako maarifa 5 yaweza kudanganywa na imani yako ikapotea.

 

Akili zetu bila Roho mtakatifu ni adui wa imani(carnality)

 

Imani iko ndani ya roho yako kwa moyo wako. Hofu huamini kile shetani analeta na kuilazimisha ndani ya mawaso yako zaidi ya vile ambavyo unavyoamini NENO LA MUNGU.

 

Uko na kauli ya kukata, uamini katika hofu yako ama uamini katika ahadi za mungu kwa neno lake.

 

Uwezipokea lolote, iwe ndogo bila imani.

 

Unawezapokea kila kitu ukiwa na imani.

 

 

- Amani itokanayo na Mungu.

Mariko 11:22, Yesu akawaambia, "Mwaminini Mungu

Hapa Yesu anatoa somo la ajabu kuhusu imani. Kutokana na Yesu kuweka imani kwa matendo, Mti wa msabibu ulinyauka na kukauka usiku huo baada ya neno lake la imani. Alinenea mti lenye uhai na likakauka. Uzima na mauti huamuliwa kwa imani.

 

 

 

                      4. MAOMBI NA NENO LA MUNGU.

 

Maomba lazima iwe na msingi wa neno la Mungu – bibilia. Imani yetu lazima isimamie ahadi zilizoko kwenye bibilia. Mungu amempa mwanadamu maelfu ya ahadi kuhusu kila eneo la maisha katika neno lake. Maombi na mahitaji yetu yeweza kupatikana sehemu fulani kwa neno katika ahadi tulizopewa.

 

Imani ni:- katika maombi kurudisha ahadi za mungu kwenye bibilia enzini mwa mungu.

 

Imani ni mkono unaofuta ahadi za Mungu kutoka kwa ghala lake na ukapokea.

 

Lakini maombi ya IMANI itatenda.

 

 

 

                      5. MAOMBI NA ROHO MTAKATIFU:- ROHO YA MAOMBI

 

Warumi 8:26-27,“Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka.Vs 27,Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu.

 

Kuna sehemu spesheli ya roho ya maombi, Utatu wa Mungu, Mungu Roho mtakatifu anaomba ndani yako kwa baba wa mbinguni. Wakati huo huo, Yesu aliyefufuka ndiye anaye tuunganisha katika utatu akisimama katika hekalu la mbinguni, akituombea na kufanya maombezi kwa baba kwa ajili ya wateule wote. Wahebrania 7:24-25.

 

Kristu anateketesa maombezi tukufu katika madhabau kama kuhani wetu mkuu katika hakalu la mbinguni. Lakini kwanza alitonesha damu yake takatifu juu ya sanduku la agano na kisha kitambaa cha hekalu lilipasuka mara mbili( Kwa vipande viwili ) kwanzia juu hadi chini. Matayo mtakatifu 27:51

 

Daudi akasema katika Saburi 141:2, Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba….”

 

Uvumba ni ishara ya maombi. Moto wa kifukizo inasimamia Roho mtakatifu. Yesu akasema,”Ombeni Katika Roho na Kweli. Yohana Mtakatifu 4:23

 

Maombi ya uombezi ni ya nguvu tu, wakati inaathiriwa na ROHO YA MAOMBI.

 

 

 

                      6. MAOMBI NA KUABUDU KATIKA AGANO LA KALE.

 

Mpango wa Hekalu:

Hema ya kukutania: Madhabau ya ubani na beseni yenye maji.

 

Mahali Patakatifu: upande wa kulia, meza ya mkate. Kushoto, mti wa mishumaa( yenye vipande saba ) na kwenye kitambaa, ni madhabau ya dhahabu.

 

Mahali patakatifu pawatakatifu: Kuna sanduku la agano na maserafi wawili wakifunika ( kiti cha rehema ) na mabawa zao, na juu yao kuna ng,aa na wingu wa utukufu ama (shechinah glory), ambapo Mungu amekaa.

 

Viungo vya uvumba:

 

Kutoka 30:34……natafi, shekelethi, kelbena, viugo vya manukato vizuri na ubani safi. Vs 35.

 

Kuna viungo vitano vya uvumba, vyote vina uzito sawa.

 

Zimepondwa na kuchanganywa vyema, na kuchomwa na moto takatifu.

 

Kuna aina mingi ya maombi, kama viongo vitano katika uvumba, hivyo kuna aina tano za maombi:-

                      1). Maombi ya shukrani

                      2). Maombi ya sifa

                      3). Maombi ya kuabudu

                      4). Maombezi

                      5). Maombi ya mahitaji yako mwenyewe na kukiri dhambi. Maombi mengine; nyimbo katika roho,

                            kunena kwa lugha (ndimi),  na maombi mengine n.k.

 

Saburi 141:2, Sala yangu ipae mbele zako kama UVUMBA, kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.”

 

 

Daudi akasema, maombi yake ni kama manukato ikielekea kwenye kiti cha enzi cha Mungu Yahweh.

 

Ufunuo 5:8,…..Kila mmoja, alikuwa na kinubi na bakuli za dhahabu zilizojaa ubani, AMBAO NI SALA  ZA WATU WA MUNGU.”.

 

Maombi ya watakatifu imehifadhiwa mbinguni.

 

Ufunuo 8:3-5,….Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu, juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi.vs 4, Moshi wa ubani ukapanda juu, pamoja na sala za watu wa Mungu, kutoka mikononi mwake huyo malaika aliyekuwa mbele ya Mungu.

 

Mstari wa 5,Kisha malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.

 

 

 

                      7. MAOMBI NA UFUFUO.

 

David Brainard  aliomba kwa ajili ya ufufuo kati ya makabali ya kihindi huko Amerika kusini.

 

Watu watano waombezi kwa vyumba vya mbao katika New Hebrides walileta ufufuo kwenye masiwa.

 

Maombi ya Yonghi Cho na mama mkwe, wakifunga na kuomba ilileta ufufuo kule seoul, Korea.

 

Arthur Miller aliomba kwa ajili ya ufufuo kule Argentina. Upepo wa nguvu ulishuka wakati wa kuanzishwa kwa chuo cha bibilia ambapo ufufuo ulianzia.

 

Evans Roberts aliudhuria mikutano ya maombi kwa miaka 13 na ufufuo ukapenya kule Wales.

 

Mel Tari na umati wa watu pamoja naye waliomba na ufufuo ukaja kama moto kule Indonesia.

 

Na mifano mengi ya maombi ya hakika ulilteta ufufuo.

 

Neno la ombi la ufufuo;

 

2 Mambo ya Nyakati 7:14, Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”

 

Ni jukumu la wakristo kuwa na ufufuo, na kuomba kwa ajili ya ufufuo, kutubu njia zao za maovu ili mungu mwenyezi aweze kumwaga Roho wake wa ufufuo kwa taifa na kuiponya na kuisamehe dhambi zao kwa sababu hawakuwa nuru na chumvi kwa taifa.

 

 

 

                      8. SHULE YA MAOMBI.

 

Ikiwa unaamini maombi, tayari uko katika shule ya maombi ya Mungu. Unajifunza kila wakati unaomba. Unavyo omba zaidi, ndivyo unavyo itimu. Ikiwa umefanya maombi hali yako ya kawaida ama umefanya maombi kama uduma yako mbele ya mungu, basi unaweza fanyia Mungu kazi kubwa.

 

 

                      9. BIDII YA MAOMBI .

 

Kuomba wakati mwingine ni kazi ngumu. Ni kama una chimba mafuta. Inagharimu ufanye kazi saa baada ya saa, siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi. Hatimaye, siku moja mafuta itajipuka- na mwishowe umepenya. Kuomba ni kama kujenga nyumba kwenye mwamba. Inabidi uchimbe shimo mingi kwenye mwamba na baadaye ukiakishia moto, kazi nyingi inafanyika kwa muda mfupi. Hivyo ndivyo ilivyo na maisha ya maombi. Punde unapenya katika roho na Mungu anatenda makuu.

 

 

                      10. MAOMBI NA KUFUNGA.

 

Maombi ya kufunga ndiyo maombi yenye nguvu. Ikiwa unataka nguvu kwa Mungu, basi inabidi uingie maombi ya kufunga kwa siku nyingi, wiki kadhaa ama siku 40 kufunga. Kufunga na kuomba ni njia fupi kugusa MOYO WA MUNGU na kupata nguvu katika maombi.

 

( Tazama pia katika kitabu kuhusu jinsi ya kufunga kwa siku nyingi: Kijitabu juu ya kufunga na kuomba.)

 

 

                      11. KUOMBA NA KUFUKUZA MAPEPO.

 

Mathayo mtakatifu 17:21,….Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.”

 

Kijana huyo ambaye alikuwa na kifafa, hangeweza kuwekwa huru kutokana na kupagawa, ila tu kwa kuomba na kufunga.

 

Mathayo mtakatifu 12:29, "Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang`anya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu?

 

Kufunga mtu mwenye nguvu inagharimu maombi ya nguvu na pengine pamoja na kufunga.

 

 

                      12. MAOMBI NA KUFUNGA KWA DANIELI ( AFYA ).

 

Danieli alikuwa mtu spesheli wa maombi. Dan 6:11,…aliomba mara tatu kwa siku…..

 

Danieli pia alikuwa mtu wa hekima. Wakati mwingine alikula mboga tu na kunywa maji peke yake.

 

Alikula chakula sawa na kile kilicholiwa katika shamba la Edeni kabla ya mwanguko wa mwadamu.

Ni kana kwamba tukila chakula hicho, ni rahisi kuota ndoto na kuona maono; ni rahisi pia kujazwa na Roho mtakatifu na kuwa na imani dhabiti.

 

                      13. MAOMBI NA KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.

 

Roho mtakatifu anatuongoza kwa njia nyingi. Wakati mwingine tunaitaji kwa dharura kujua jinsi ya kuomba kwa njia sahihi, kuhusu mapenzi ya Mungu.

 

Ni kama yafuatayo:-

-         Kupitia maono na ndoto

-         Kupitia neno la maarifu na neno la hekima

-         Kupitia neno la Mungu

-         Kupitia unabii

-         Kupitia sauti kutoka ndani ama nje

-         Kupitia utu wa ndani, kuhisi,“Urim na Tummim“, jibu la ndio au la.

-         Kupitia hali ya maisha ya kawaida. ( Yonah katika mawimbi )

( Tazama pia masomo kuhusu: Njia saba za kuongozwa na Roho mtakatifu katika: Dhihirisho za Roho Mtakatifu.)

 

 

                      14. MAOMBI KATIKA CHUMBA CHA MAOMBI.

 

Hii ni aina ya maombi ambapo ni wewe tu peke yako. Mungu na wewe tu.

 

Mathayo 6:6,…. Lakini wewe unaposali, ingia chumbani mwako, funga mlango, kisha umwombe Baba yako asiyeonekana. Naye Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza.”

 

Chumba chako cha maombi chaweza kuwa popote, kwa mfano unapoendesha gari, unaweza kuomba bila kusumbuliwa. Unapotembea peke yako, unaweza kuomba bila mtu kuzungumza nawe, ama katika kitandani usiku. Mahali elfu yaweza kuwa chumba cha maombi. La muhimu ni kwamba unamwaga roho wako kwa mungu baba wako wa mbinguni wakati uko peke yako bila kusumbuliwa katika uwepo wake. Papo hapo unawasiliana kindani na mungu baba.

 

 

                      15. MAOMBI YA PAMOJA.

 

Aina nyingine ya maombi ni wakati watu wawili ama watatu wanakubaliana katika roho kuomba kwa ajili ya itaji maalum, mambo kadhaa ama shida fulani.

Hii inapatikana katika Mathayo 18:19-20, Lolote mtakalo lifunga hapa duniani, itafungwa kule mbinguni na lolote mtakalo fungua hapa duniani litafunguliwa mbinguni. Ms 19, Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.     Ms 20, …. Kwa maana popote pale wanapokusanyika wawili au watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao."

Kumbuka kukubaliana ni katika roho, sio tu katika mawaso lakini ni kwa hali ya kiroho, kukubaliana ni katika ROHO.

 

 

                      16. MAOMBI KATIKA UMATI.

 

Matendo ya Mitume 4:23, 24,….waliungana pamoja katika kumwomba Mungu…..”

 

Soma pia, Mathayo mtakatifu 18:18-20.

 

Hii ni maombi ya pamoja. Kwa hakika maombi ya umati ni ya nguvu sana, hata leo.

 

 

                      17. MAOMBI KATIKA JAMII.

 

Kichwa cha jamii pia ni kuhani katika jamii na ni lazima aongoze maombi katika nyumba yake.

 

Kornelio alikuwa mtu wa aina hiyo.Tazama, alikuwa ni kaisaria lakini MAOMBI yake na ZADAKA zake zilisikika na kupokelewa mbinguni. Matendo ya Mitume 10:4,….Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini.”

 

Filip muinjilisti katika Samaria pia alikuwa kuhani mzuri nyumbani kwake. Alikuwa na binti wanne wasioolewa wenye vipawa vya kinabii. Matendo ya mitume 21:8.

 

Kila kichwa cha jamii lazima awe kuhani katika nyumba yake, pia katika kuomba na kufundisha wote katika jamii jinsi ya kuomba.

 

 

18. MAOMBI NA NYIMBO KATIKA ROHO. MAOMBI NA KUABUDU                   KATIKA NYIMBO.

 

Colo. 3:16,”….. Fundishaneni na kushauriana kwa hekima yote. Imbeni zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho;”

 

Zaburi ni wimbo katika roho yenye maana ya kinabii na pia ni maombi. Fikiria kuhusu mazuri katika kitabu cha Zaburi, Ombi la dharura la Daudi la msamaha na kurejeshewa roho mpya wakati alipoanguka katika dhambi na Batsheba. Zaburi kwa ujumla ni nyimbo katika roho.

 

KUABUDU NA KUIMBA KATIKA ROHO:

 

Wakati mwingine umati wanapoimba katika roho, hiyo ndiyo ibada kamili ya mungu baba. Hii ni maombi wa kiwango cha juu. Hii ndio kile bibilia inaita sifa.

 

 

                      19. MAOMBI NA VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU.

 

Kufanya kwa matendo vipawa vya roho mtakatifu.

 

Aina tatu vya vipawa:

-         Kunena kwa lugha.

-         Kutafsiri kunena kwa lugha

-         Unabii

 

Aina tatu vya vipawa vya ufunuo:

-         Neno la maarifa.

-         Neno la hekima.

-         Kipawa cha kubambanua miroho.

 

 

Aina tatu vya vipawa vya uweza(nguvu):

-         kipawa cha uponyaji.

-         Kipawa cha miujiza

-         Kipawa cha imani.

 

Katika kuhudumu na vipawa vya roho mtakatifu, tunategemea sana maombi na imani, kwa hakika hatuwezi fanyia kazi roho mtakatifu pasipo kuomba na kuwa na imani.

 

Kunena kwa lugha ni maombi. Ni kuomba katika roho kwa mungu baba. Tunapowekelea mikono kwa wagonjwa, lazima tuombe, la sivyo hakuna kitu kitatendeka. Ukiwa na kipawa cha miujiza, lazima uitishe muujiza katika maombi, utaje maneno ya kuamuru, pasipo kufanya hivyo, hakuna muujiza utatendedeka.

 

Hasa kipawa cha imani hutegemea sana maombi. Baraka ya yakobo kwa Ephraim na Manasseh. Mwanzo 48. Baraka ya Isaka kwa yakobo na Esau. Mwanzo 27.

 

Kuhudumu katika vipawa vya Roho na maombi haiwezi kutenganishwa.

 

 

                      20. MAOMBI NA VITA VYA KIROHO: 

 

SEHEMU YA 1.

 

A). Kujua adui wako.Dan 10:13 na 20. roho za mipaka. ( chama cha upelesi wa kiroho).

 

B). Utawala wa shetani na mipango ya vita. Eph 6:12

 

C). Silaha ya Mungu. Hatua za vazi la kiroho. Eph 6:13-14

 

D). Viwanja vitatu vya vita.

 

E). Kutumia mamlaka uliopewa na Mungu.

                     

 

A). KUJUA ADUI WAKO.

 

Mossad, Chama cha Israeli kinacho julikana sana cha upelelesi, imeokoa Israeli kutokana na janga kubwa lingewapata na hata kuipatia Ushindi vitani, kwa sababu wanapata ujumbe mzuri kuhusu maadui zake. Sisi kama wakristu, kama Israeli wa kiroho, pia twaweza kupata ujumbe kuhusu adui wetu ambaye ni Shetani na mapepo zake zote na malaika walioanguka. Ujumbe kuhusu adui wetu tunaweza kupata tu katika neno la Mungu (bibilia) na Roho Mtakatifu atatufunulia siri katika ulimwengu wa Kiroho.

 

Roho za mipaka: Danieli 10:13, “Lakini mkuu wa ufalme wa uajemi(persia) alinipinga siku ishirini na moja…..”

 

Danieli 10: 20-21, “….na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, mkuu wa Uyunani (Greece) atakuja.”

 

Malaika mkuu Gabrieli alipigana na nguvu za giza juu ya mataifa mawili. Aliweza kupata msaada kutoka kwa malaika mkuu Michael.

 

 

B). UTAWALA WA SHETANI NA MIPANGO ZA VITA.

 

Waepheso 6:12, “Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya JESHI OVU la ulimwengu wa roho; tunapigana na WATAWALA, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.”

 

Vikundi vinne vya jeshi la shetani, vinaweka kwenye ngazi za utawala.

 

 

C). SILAHA YA MUNGU.

Waefeso 6:14-17,…..Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, vs 15, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Vs 16, Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. Vs 17, Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.”

 

D). VIWANJA VITATU VYA VITA.

 

-         Akili yako

-         Roho yako (nafsi)

-         Mdomo wako.

 

E). KUTUMIA MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU.

 

Luka 10:19,“Naam, nimewapeni uwezo wa kukanyaga nyoka na ng`e, na uwezo juu ya nguvu zote za yule adui; hakuna chochote kitakachowadhuru.“

 

Mariko 10:15-20, enendeni kwa ulimwengu wote........

 

Mamlaka yetu ni kwa sababu ya damu ya Yesu na kwa mamlaka katika jina lake.

 

 

 

SEHEMU YA 2.

 

a)      Mgongano wa kiroho

b)      Kufunga mwenye nguvu

c)      Silaha zetu katika vita vya kiroho

d)      Kufamia ngome za shetani

e)      Vita vya polland, India, Denmark na mataifa yote.

 

a). Mgongano wa kiroho

 

Mwanzo wa roho ya ibilisi.

Kulikuwa na mashindano yaviumbe vilivyoumbwa mbinguni, ambao ni malaika, kabla ya DUNIA na ADAMU kuumbwa. Kulikuwa na malaika wakuu watatu, Lucifer wa nuru, Gabrieli – mkuu wa malaika wa kutumwa na Michael – mkuu wa malaika wa vita.

 

Kukawa na vita mbinguni. Lucifer na malaika wake waliasi walitupwa kutoka mbinguni.

 

Lucifer aliasi Mungu na akawa Shetani, adui wa Mungu. Isaya 14:12-16, “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi!……”

 

Lucifer alikuwa kiongozi wa tamburines na pipes ( Nyimbo na sifa ) kule mbinguni. Ezekieli 28:13-19.

 

Lucifer anahusika na biashara duniani na shughuli za pesa.

 

Ezekieli 28: Uliishi kwenye Edeni, Shamba la mazuri ya Mungu…..

 

Ezekieli 28:16, ulikuwa ukinunua na kuuza na hii ilikufanya wa hatari na mwenye dhambi. ( Tafsiri kutokana na habari njema )

 

Shetani alitupwa kutoka mbinguni pamoja na thuludhi ya malaika (1/3) walioanguka naye.

 

Katika ufunuo 12:7-9,…Kisha kukazuka vita mbinguni:…..vs 9…. alitupwa duniani, na malaika wake wote pamoja naye.”

 

Hao, Ibilisi na malaika walioasi, wajenga ufalme wa bingamisi kwa Mungu katika “ulimwengu wa roho” eneo kati ya makao ya Mungu na mbingu . Shetani na malaika walioasi pamoja na mapepo wote wanajumlisha ufalme wa giza.

 

Ufalme wa giza imetawala, upande ama ujumla wa kila taifa, mji, kijiji, nyumba na karibu kila mtu.

 

Kusudi la shetani ni kuharibu kiumbe cha maalum cha Mungu – MWANADAMU.

 

 

b) Kufunga mwenye nguvu.

 

Mathayo 16:19… kila utakachofunga duniani, kitafungwa pia mbinguni…(Petero)

 

Mathayo 18:18….mtakachofunga…….

Colossians 2:15, “Juu ya msalaba Kristo aliwapokonya nguvu zao hao pepo watawala na wakuu; aliwafanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuwaburuta kama mateka katika msafara wa ushindi wake.

Mathayo 12:29, "Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang`anya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu? Hapo ndipo atakapoweza kumnyang`anya mali yake.” (Ni maombi pekee inaweza hii.)

c) Silaha zetu katika vita vya kiroho.

 

-         Damu ya mwana kondoo

 

-         Ushuhuda wa neno – Ufunuo 12:10-11

 

-         Jina la Yesu – Yohana 14:13-14

 

-         Maombi – Dan 10:12-13, malaika walioangushwa na mkuu wa uajemi walishambuliwa na malaika mkuu Mikaeli kwa sababu ya maombi ya Danieli ya vita vya kiroho.

 

-         Sifa na kuabudu – 2 Mambo ya nyakati 20:21-30, Ushindi wa Yehoshafati.

 

-         Kufunga na Kuomba – Kufunga ni silaha ya nguvu ya kuharibu ngome za adui.

 

-         Vipawa vya Roho – Hasa kipawa cha kubambanua miroho na kipawa cha imani

 

-         Silaha ya Mungu – Waefeso 6:14-15.-Mshipi wa ukweli, dirii ya haki kifuani, kama viatu tayari kueneza injili, ngao ya imani, chapeo cha wokovu, upanga wa Roho, siku zote mkiomba….

 

-         Ukweli – shetani huogopa ukweli. Yesu NI ukweli, njia na uzima. Neno la Mungu NI ukweli. Ukweli uliomwagwa ndani yake utamshinda shetani na ukweli utaweka huru waliofungwa.

 

-         Roho Mtakatifu – Ni nguzo ya nguvu nje na ndani ya mbingu.

 

Kanuni ya kupokea yasiyo wezekana:

MAOMBI(KUFUNG)+IMANI+ROHO YA MAOMBI=  KUPOKEA YASIWEZEKANA NA YANAYOWEZEKANA!

 

d). kuvamia ngome za shetani

2 Wakorinto 10:4, “Maana, silaha tunazotumia katika vita vyetu si silaha za kidunia, ila ni nguvu za Mungu zenye kuharibu ngome zote. Tunaharibu hoja zote za uongo,”

Maombi yetu ni kinga na inapigana.

 

Silaha ya kujikinga ni ngao ya IMANI, ikivunja mishale yote ya adui.

 

Silaha ya kupigana ni upanga ukatao kuwili ambao ni neno la Mungu. ( kuomba katika ulimwengu wa kiroho ni kutoa upanga katika ngao )

 

 

e). Vita vinavyo endelea hivi sasa.

 

Majeshi makubwa ya ulimwengu wa giza na nguvu za malaika hutembea kwa sababu ya maombi ya waombezi katika vita vya kiroho. Vita vinaendelea katika maeneo yasionekana juu ya katoliki ya Poland na India na miji mengi yenye millioni ya masanamu, hata katika eneo ya Denmark ni uwanja wa vita. Uislamu unavamia karibu kila nchi katika Uingereza kwa karne ya sasa.- Naomba Mungu awainua majeshi ya Maombi katika miji hizi. La sivyo, bilioni za watu watapotea milele ne milele.

 

Mungu bado anatafuta mtu wa kusimama kwenye pengo.

 

 

                      21). PINGAMIZI KATIKA MAOMBI.

 

1). Usherati ni kisuizi kwa maombi.

      Waebrania 13:4, ”Ndoa na iheshimiwe na watu wote……..

 

2). Waume lazima waheshimu wake zao, la sivyo maombi yao hayatajibiwa.

      1 Petero 3:7, “ Hivyo enyi waume ……….

 

3). Kutoamini hasa, ni kisuizi nambari moja.

      Yakobo 1:6-7, ”Ila na aombe kwa imani…..

 

4). Maombi ya mwenye dhambi haitasikika mbinguni, ila tu maomba ya toba.

      Yohana Mtakatifu 9:31, ”Twajua ya kwamba Mungu hawasikii wenye dhambi….

 

5). Dhambi iliyofichika ndani ya roho, itakuwa kisuizi kwa maombi.

      Zaburi 66:18, ”Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, bwana asingesikia.”

 

6). Moyo usiyosamehe haitajibiwa katika maombi.

        Mariko 11:25, ” Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni,…..

 

7). Laana iliyotokana na mababu au dini yasiyo ya ukweli, itazuia maombi.

Kutoka 20:5, ”……kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana      maovu ya baba zao, hata kizaza cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

 

8). Kuomba pa tupu.

        Yakobo 4:3, “Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa Zenu.”

 

9).  Kwanini magonjwa mengine zaponywa na mengine hapana? Mbona maradhi mengine haiponi? Kwanini hali hii ya  uponyaji hukawia?

 

a)      Kutosamehe. Mariko 11:25.

 

b)      Kutoamini. Yakobo 1:6, Omba na imani bila shaka…..Mariko 11:24, amini kuwa tayari   ameishapokea……

 

c)      Kutotii neno la Mungu. ( Neno katika Bibilia )

 

d)      Kutotii sauti ya Mungu. ( inayonenwa na Roho Mtakatifu )

 

e)      Indulgence. Yakobo 4.3,…..ili mvitumie kwa tamaa zenu.

 

f)        Kuabudu miungu na laana zinazoifuatilia.

 

g)      Kuvunja nadhiri.

 

h)      Kumwaga damu isiyo na hatia ( Kutoa mimba )

 

                      i).   Usherati ( isiyojulikana na inayojulikana )

 

                      j). Kuabudu miungu (Kuabudu miungu mengi, ili Yesu akafanyika kama mmoja ya miungu hizo (India)

 

                      k) Kuamini katika imani tofauti ( superstitions)

 

l). Kuomba wafu ( Watakatifu waliotutangulia, black Madonna, Mama mtakatifu wa Mungu, Bikira Maria, waliokufa zamani, kutumia rosari katika maombi.)

 

m). Kuabudu miroho.

 

n). Dhambi katika maisha yako, dhambi yaweza kuwa sababu ya kutopokea uponyaji wako.

 

o). Uchungu, kuwa na uchungu ya undani.

 

p). Uchungu na hasira juu ya Mungu Yahweh, hasira iliyo mbaya zaidi ( usinungunikie Mungu Yahweh)

 

q). Udhaifu katika maombi, wanyonge hawatapokea majibu ya maombi.

 

r). Laana kutoka kisasi cha tatu hadi cha nne. Kutoka 30:5.

 

s). Freemasonry.

 

t). Ushetani ( Kuweka sahihi ya kujikabidhi kwa shetani kutumia damu ya binadamu )

 

u) Kujiuzisha na Mambo ya Kisasa.

 

v) Maovu.

 

 

 

                      22. KUVUMILIA KATIKA MAOMBI.  

 

Waefeso 6:18, ”….mkisali kila wakati…….na kudumu…….

 

Eliya katika kilele cha Karmeli, 1 Wafalme 18:43-44, ”…..mara saba…..”

 

Mjane na kadhi dhalimu. Luka 18:3-8.

 

Danieli alidumu katika maombi kwa siku 21, japokuwa malaika alitumwa kwa siku ya kwanza, na maombi yake ilisikika mbinguni pia kwa siku ya kwanza. Hebu fikiria, Ikiwa Danieli angeacha kuomba katika siku ya ishirini, malaika mkuu hangeweza kumtembelea katika siku yake ya 21 ya kufunga na kuomba.

 

 

                      23. MAOMBI NA UPENDO WA MUNGU.

 

Wagalatia 5:6,…. Bali imani itendayo kazi kwa upendo.

 

Imani ni kiungo ya muhimu katika maombi na imani inatenda kazi kwa upendo, hivyo hivyo, unapoendelea kuonyesha upendo wa Mungu, ndivyo utapokea zaidi katika maombi!

 

Hata hivyo, hii ni upendo wa Kristu katika matendo kwa maisha yako ya maombi, sio tu upendo wa kawaida wa mwanadamu.

 

Upendo na Imani ni mojawapo ya tundo la Roho ambalo ni la muhimu sana.

 

Wagalatia 5:22-23, Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, vs 23, upole na kuwa na kiasi….”

 

Uliza Mungu akubatize kwa Roho mtakatifu kwa moto. Luka 3:16. Ndivyo utakuwa na upendo na imani ikitenda kazi katika maisha yako ya maombi na kuleta majibu mazuri ya maombi yako.

 

 

                      24. MAOMBI NA UPONYAJI WA ROHO. UPONYAJI WA HISIA.

 

Yesu kwa hakika ataponya kila aina ya magonjwa na kutokamilika katika mwili na nafsi. Pia pamoja na mawaso na hisia. Kila hali isiyo ya kawaida katika mawaso na hisia ataikamilisha.

 

2 Tim 1:7, “Kwa maana Mungu hakutupa Roho wa kutufanya tuwe waoga, bali alitupa Roho wa kutujalia nguvu, upendo na nidhamu.”

 

Waona, hofu yaweza kuwa ni roho, lakini Mungu anataka atupatie amani na akili timamu. Kusumbuliwa kwa hisia mara kwa mara inaletwa na roho chafu ya ibilisi.- Tazama pia masomo kuhusu ushetani.

 

Yohana 8:36, “Kama mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli.”

 

Yesu anataka kutuweka huru katika roho, nafsi na akili.

 

 

                      25. MAOMBI NA UOMBEZI.

 

Waebrania 7:25, ......“maana yeye anaishi milele kuwaombea kwa Mungu.

 

Mwokozi wetu amesimama katika hekalu la mbinguni akituombea.

 

Warumi 8:26,....“ lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka.

 

Warumi 8:27,....“ kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu.

 

Roho mtakatifu ndani yako ni muombezi. Warumi 8:26,....“ lakini Roho mwenyewe anatuombea.....

 

Zaburi 106:23,....kama Musa, mteule wake,asingalisimama, mbele zake kama mahali palipobomoka, ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.

 

Mungu anatafuta mtu anayeweza kusimama katika pengo ( Daraja )

 

Ezekieli 22:30, Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakaye litengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.

 

Umati kubwa wa watu wanapotea kwenye kuzimu milele yote. Mabilioni ya watu hawakupata nafasi ya kuguzwa kwa ajili ya dhambi zao na hawakuweza kuufikia hali ya kuweza kuokoka, na hatimaye kupoteza wokovu wa nafsi zao kwa sababu hakuna mtu aliwapenda kiasi ya kuwaombea. Hakuna mtu aliweza kurehemu na kuugua katika maombi kwa ajili yao. Ni nguvu tu ya waliohaki, wakiugua katika uchungu wa moyo kwa kuongozwa na ROHO YA MAOMBI, ndio itapenya. Yesu Kristu tayari aliumia na kuchukua ghadhabu iliyo yetu na haisatahili hata kidogo kwa mwadamu mwisho wake uwe ni moto wa milele ya jehanamu. Ezekieli 18:23, Mungu hafurahishwi na kifo cha mwenye dhambi.

 

Maombi kikamilifu yaweza tu tukamilishwa wakati unaomba katika roho, jinsi Paulo alieleza katika Warumi 8:26-27.

 

Kuomba bila Roho haina mazao, karibu na bure.  Maombezi chini ya uweza wa roho wa maombi italeta matunda mengi. Imani inafunguliwa na majibu makuu ya maombi itamiminika.

 

 

                      26. MAOMBI NA UTAKATIFU. MAOMBI NA UPAKO.

 

Tunapoishi zaidi katika utakatifu, ndivyo zaidi nguvu katika maombi!

 

Tunapokuwa na tabia zaidi ya kiungu, ndivyo tunakuwa na upako zaidi.

 

Unapokuwa na upendo zaidi wa kiungu moyoni mwako, ndivyo unapata nguvu zaidi katika maombi.

 

 

                      27. MAOMBI NA KUUGUA KWA NAFSI.

 

Mathayo 25:36-46, ” Yesu katika shamba la Gethsemane

 

Warumi 8:26……lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.”

 

 

                      28. MAOMBI YA KUFUNGUA NA KUFUNGA.

 

Mathayo 18:18-20, “ …….mtakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na mtakachofungua duniani kitafunguliwa mbinguni…..”

 

 

                      29. MAOMBI NA KUABUDU MIUNGU: ( OCCULTSM )

 

Kutoka 20:4-5, “………Usijifanyie sanamu ya kuchongwa, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho dunia. Ms 5, Usivisujudie wala kuvitumikia, kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

 

( Tazama pia masomo juu ya : Kuoshwakiroho kutoka   kuabudu shetani / miungu )

 

 

 

                      30. MAOMBI YA KINABII.

 

Wakati mwingine ninapofanya maombi ya binafsi, maombezi, maombi hubadilika kuwa maombi ya kinabii na ninajikuta nikiomba kuhusu mahitaji yaliyofichika ambayo mimi mwenyewe siya fahamu kabisa, lakini roho aliyendani  yangu, anaombea mahitaji yaliyo sirini.

 

 

                      31. MIKUTANO YA MAOMBI NA JINSI YA KUZIONGOZA.

 

I.                   Kusudi na jinsi ya kupanga mikutano ya maombi.

II.                Jinsi ya kuongoza mkutano wa maombi.

III.             Ugumu iliyoko katika mikutano ya maombi.

 

I. Kusudi na jinsi ya kupanga mikutano ya maombi.

 

a)      Maombi ya pamoja katika mkutano wa maombi inazaidia kuinua umoja katikati wa wakristo. Umoja na upendo ina nguvu wakati tunamwaga roho zetu mbele za Mungu.

 

b)      Omba maombi ambayo yaweza kuguza moyo wa Mungu.

 

c)      Kusudu lingine la muhimu katika mikutano ya maombi ni kuomba kwa ajili ya uguzo na kuokolewa kwa wenye dhambi.

 

II.                Jinsi ya kuongoza mkutano wa maombi.

 

a)      Huwa ni vyema kufungua mkutano wa maombi kwa kusoma kifungu kifupi ya neno la Mungu. ( Sio mahubiri )

 

b)      Toa maelezo kidogo kuhusu maombi, kuelimisha na kueleza kuhusu maombi.

 

c)      Katika kuita watu wa kuomba, wacha wale wenye kiu ya kuomba waombe. Maomba baridi ya mtu wa ulimwengu yaweza kufanya mkutano wote kuwa baridi. Ita wale ambao wamejaa Roho mtakatifu.

 

d)      Maombi kwa kawaida,ni vyema iwe fupi, Wanao omba maombi ndefu, wanafanya hivyo sio kwa sababu wana roho ya maombi lakini ni kwa sababu hawana. Wacha waombe kwenye lengo na kwa ajili ya lile ambalo wameja kuliombea.

 

e)      Kila mmoja aombee jambo moja ama maombi fupi fupi. Wakati mtu anapo hisi jambo ndani yake, ni kwa sababu anauzito wa jambo hilo moja, na baada ya kuomba kupitia roho wa maombi, atatulia kwa mpango, pengine kwa muda fulani.

 

f)       Ni la muhimu pia kuona kwamba kila dakika imepangiwa, kusiwe na muda mwingi wa ukimya.

 

g)      Njia nzuri ya kuongoza mkutano wa maombi ni kuacha watu waombe kwa pamoja. Kuna nguvu zaidi wakati kila mmoja anaomba kwa wakati moja. Watu 10 wanapoomba kwa sauti, kutakuwa na nguvu mara 10 zaidi ya maombi, kana kwamba watu 10 wanaomba moja baada ya mwingine.

 

 

III. Ugumu uliyoko katika mikutano ya maombi.

 

-Wakati umati hawana ujasiri na kiongozi wa mkutano kutokana na uwezo wake wa kuongoza, itafanya mkutano na maombi ififie ama isimame.

 

-Wakati kiongozi hakui kiroho. Hii itasababisha ukafu na ubaridi na hali yake pia inaweza toa upako ya umati wote.

 

-Ikiwa kiongozi ana roho mbaya na uchungu, itaharibu mkutano wa maombi.

 

-Watu ambao wanakuja mkutano wakiwa wamechelewa, baada ya watu kuanza kuomba. Mwingine anaingia na makelele wakati watu wameweka mawazo yao kwa maombi na kufunga macho yao, hii inaharibu roho ya maombi sana.

 

-Wakati watu wanaomba maombi kafu, na kutubu kwa ubaridi kwa dhambi wanazozijua inaua roho ya maombi.

 

-Kuimba sana kwa kawaida huumiza roho wa maombi. Roho wa kuugua wa maombi haifanyi watu kuomba.

 

-Kuleta maswala mengine ama majadiliano ambayo haiusiki na maombi, utashinda mkutano wa maombi. Maswala haya yatatuliwa kwingine.

 

-Kiongozi na wengine lazima washirikiane katika roho na kutambua ni nini roho wa Mungu anataka kutenda kwa mkutano huu.

 

-Mikutano mengi hufanywa kwa MUDA MREFU SANA. Ni lazima imalizike ilhali watu wanahisi uwepo wa Roho, sio kungoja hadi watu wamechoka sana na Roho tayari ameondoka.

 

-Wakati wakristo wanatumia muda wote kujiombea na mahitaji yao wenyewe. Wanastahili kuwa wamefanya hivyo katika chumba chao cha maombi. Tunapokuja pamoja kwa ajili ya maombezi lazima tuwetayari kwa maombezi kamilifu kwa wengine.

 

-Usi “hubirie” umati wakati wa maombi.

 

Maelezo:

 

Mikutano ya maombi ni ufunguo katika hali ya kiroho kanisani.

 

Kila muhudumu lazima ajue ikiwa mikutano ya maombi itapuuzwa, juhudi zake zote zitakuwa bure.

 

Jukumu kubwa iko kwa anayeongoza mkutano wa maombi. Lazima awe tayari kimawaso na pia kimoyo( roho )

 

Mikutano ya maombi ndiyo ya muhimu kwa mikutano zote kanisani.  Ita:-

               

-         Inua umoja

 

-         Ongeza upendo kati ya wandugu.( wapendwa )

 

-         Inua kukua kwao kwa neema

 

-         Huisha maisha ya kiroho kwa kila mmoja

 

-         Badilisha “moyo” wa kanisa.

 

 

N.B.- Kiongozi wakati mwingine anaweza kuacha umati waombe kwa pamoja katika nia moja kama ilivyo katika Matendo ya Mitume 4:24 na 31, ......“waliungana pamoja katika kumwomba Mungu, .....ms 31, Walipomaliza kusali, pale mahali walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, nao wote wakajazwa Roho Mtakatifu.

 

 

32. MAOMBI NA MAPENZI YA MUNGU. ( JINSI YA KUJUA MAPENZI YA MUNGU ) 

 

1.Yohana mtakatifu 5:14-15,“Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya mapenzi yake, yeye hutusikiliza......

 

 

Jinsi ya kujua mapenzi ya Mungu.

 

a)      Sikiliza “sauti yako ya ndani” Roho Mtakatifu akinena na roho yako. Roho Mtakatifu atakuambia mapensi ya Mungu; Mapensi yake katika hali fulani na utakuwa na habari kamili kuhusu mambo fulani.

 

b)      Linganisha hitaji lako na bibilia, neno la Mungu. Ikiwa kuna kitu katika MAOMBI YAKO INAYOPINGA BIBILIA, basi badilisha ombi lako liwe katika mapenzi ya Mungu na utapata majibu.

 

 

 

 

33. MAOMBI NA HUDUMA, AFISI KUU YA MITUME,

Matendo ya Mitume 6:4,“ Sisi, lakini, tutashughulika na sala na kazi ya kuhubiri neno la Mungu.

Mitume waliacha kazi ya kuhudumu mezani, walijua kwamba ofisi yao kuu ya huduma ni kuhudumu katika MAOMBI na kupeana neno la Mungu kwa watu wote.

 

Pembe nne za muhimu kanisani iliyoko na bado iko leo:Matendo ya Mitume 2:42,“ Hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kidugu, kumega mkate na kusali.

 

 

 

34. MAOMBI KATIKA BIBILIA, YESU, DANIELI, DAUDI, AYUBU, ABRAHAMU, MUSA,   YABEZI, MFALME HEZEKIAH, SULEMANI, UMATI KATIKA YERUSALEMU.

 

Maombi ya Yesu katika Yohana 17:

 

Maombi ya Danieli, Dan 9:3-19

 

Maombi ya Daudi katika kitabu cha Zaburi

 

Zaburi 22 ( Maombi ya mnabii kuhusu Yesu msalabani )

 

Zaburi 23 ( Zaburi ya mchungaji )

 

Zaburi 51 ( Toba ya Daudi baada ya kuonana na Bethsheba )

 

Maombi ya Ayubu: Ayubu 42:1-6 ( Ayubu anyenyekea mbele za Mungu )

 

                                Ayubu 42:8 na 10 ( Ayubu anaomba kwa ajili ya wenzake.)

 

Maombi ya Abrahamu:- Mwanzo 18:23-33 ( Abraham anaombea haki mjini Sodoma na Gomorrah )

 

Maombi ya Musa :- Hesabu 14:11-20 ( Musa akiombea wana wa Isaeli )

 

Maombi ya Yabesi:- 1 Mambo ya Nyakati 4:9-10, (Siku za usoni zilibadilika kwa ajili ya Ombi hili.)

 

Mfalme Hezekiah:- 2 wafalme 20:1-6, Maombi ya Hezekiah ilibadilisha mawaso ya Mungu na mpango juu ya maisha yake, na akamuongezea miaka 15 zaidi.

 

Maombi ya Suleiman: 2 Mambo ya Nyakati 7:13-42, Suleiman anaomba kwa ajili ya kuweka wakfu hekalu mpya                  alilojenga.

2 Mambo ya Nyakati 7:14 ff. ( Mungu anamjibu Suleiman usiku, akamwonyesha kwamba maombi yake yamesikika mbinguni. 

 

Maombi ya umati kule Yerusalemu: - Matendo ya mitume 12:5, (Kanisa liliomba bila kukoma kwa ajili ya Petero gerezani.)

 

-         Matendo ya mitume 4:31, Walipomaliza kusali, pale mahali walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, nao wote wakajazwa Roho Mtakatifu. Wote wakaanza kuhubiri neno la Mungu bila uoga.

 

35. MAOMBI KAMA HUDUMA MAALUM. ANNAH MNABII.

 

Luka 2:36-37,….Anna, … Wakati huo wote alikaa Hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana.”

 

Wakolosai 4:12,….Epafra,…Daima anawaombeeni ninyi kwa bidii”

 

Epafra alihudumu katika maombezi. Hannah alihudumu katika kuomba na kufunga kama huduma maalum.

 

 

 

                      36. MAOMBI NA FUNGU LA KUMI.

 

Malaki 3:9-10, ms 9,Ninyi mmelaaniwa kwa laana….ms 10, Leteni zaka kamili ghalani, ili kiweko chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha,

 

Kwa hakika, maombi yetu yaweza kuzuiliwa kwa ajili ya laana kutoka kwa Mungu kwa sababu ya kutolipa fungu la kumi.

 

Tukimwibia Mungu, ataondoa baraka kwa za maombi yetu.

 

 

                      37. MAOMBI NA MAFUTA YA UPAKO.

Yakobo 5:14-16,“Je, yuko mgonjwa kati yenu? Anapaswa kuwaita wazee wa kanisa, nao watamwombea na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Vs 15, Wakiomba kwa imani mgonjwa ataponyeshwa; Bwana atampatia nafuu, na dhambi alizotenda zitaondolewa.

Kutumia vazi lililo pakwa mafuta na kuombewa pamoja na kuwekelea mikono na wazee wakati mwingine ni muhimu.

 

 

                      38. KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU, ROHO WA MAOMBI.

 

Takaza moyo wako. ( Kuoshwa kwa roho )

 

Limia udongo na mchanga utakuwa safi tena.

 

( Tazama pia somo kuhusu: Nidhamu na Roho Mtakatifu. ( Kuboresha tabia na kujazwa na Roho Mtakatifu )

 

 

 

                      39. MAOMBI NA KUTOA MSAADA.

 

Matendo ya Mitume 10:4,...“ Huyo malaika akamwambia, "Mungu amezipokea sala na sadaka zako kwa maskini.

 

Kornelio ni mtu aliyeomba sana na kutoa msaada kwa wayahudi. Alikuwa afisa katika jeshi la Kirumi lakini alimcha Mungu. Sadaka zake pamoja na maombi zililipwa vyema na pia jamii yake yote iliokolewa na kubatizwa.

Katika Matendo ya Mitume 10:31, ..“akasema: `Kornelio! Sala yako na sadaka zako kwa maskini vimekubaliwa na Mungu.

 

Kila hela unayotoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu ina nakiliwa mbinguni kwa ajili yako. Ndio, kwa hakika, kile unachotoa kuwapa masikini, unamkopesha Mungu. Maombi yako yanasikika na kujibiwa.

 

 

 

40. BARAKA NA MAOMBI KATIKA BIBILIA, BARAKA ZA DEPORAH KWA USHONAJI, BARAKA ZA KINABII, NEEMA YA BWANA.

 

Baraka za Haruni: Hesabu 6:24-26,

 

Bwana hubariki na kukuhifadhi.

 

Bwana hufanya uso wako ung´ae na ni wa neema ningi kwako.

 

Bwana huinua kikombe chake kwako na kukupa amani.

 

Baraka za kinabii: Baraka za Paulo, 2 Wakorinto 13:14.

 

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo,

 

Na upendo wa Mungu baba,

 

Na ushirika wa Roho Mtakatifu,

 

Iwe nanyi. Amen.

 

Ibada: Zaburi 100:5, 2 Mambo ya Nyakati 7:3,

 

Kwa maana Mungu ni mwema,

 

Rehema Zake ni za milele,

 

Na haki yake hudumu kwa kisasi hadi kisasi.

 

 

Maomba ya Bwana: Matayo 6:9

 

Baba wetu uliye Mbinguni,

 

Jina lako litukuzwe,

 

Ufalme wako uje,

 

Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani, kama ilivyo Mbinguni,

 

Utupe leo mkate wa kila siku,

 

Na utusamehe makosa yetu kama vile tunavyo wasamehe waliotukosea,

 

Na usitutie katika Majaribuni bali utuokoe na yule muovu,

 

Kwa maana ufalme ni wako, nguvu na utukufu, milele na milele,

 

Amen.

 

 

Meza ya Bwana: Wakati wa ibada ya kumega mkate: ( baada ya Didache )

 

Maran atha: Bwana yuaja, ama Maranatha: Tazama, Bwana amekuja.

 

 

                      41. MAOMBI NA MAHUBIRI.

 

Waefeso 6:19,.“Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti.

 

Ikiwa katika Maombi unaweza kufunga nguvu za giza kabla ya mahubiri, roho ya muhubiri yaweza kuuhishwa na kupewa maneno atakayoyanena bila kuzuiliwa, na anatoa ujumbe katika upako wa Roho Mtakatifu.

 

Kwa mengine, ukipuuza maombi na hakuna yeyote yule anayekuombea kabla ya kuhubiri, hakuna kinga kinyume cha muovu na matendo yake ya uovu, na pia upako waweza kupotea na mahubiri yakawa hayana nguvu na kuchosha.

 

 

42. MAOMBI NA AHADI ZA MUNGU KATIKA BIBILIA NA MASHARTI YA MAOMBI KUJIBIWA. 

 

Kupokea majibu ya maombi, kufanya ahadi za mungu ifanye kazi katika hali yetu ya kawaida, kuna masharti lazima zitimizwe. Ahadi za Mungu yafuatanishwa na masharti. Kunazo sheria za kiungu za kutii kuhusu maombi.

Mariko 11:24, Kwa hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, AMININI kwamba mmekipokea, nanyi mtapewa. ( Kununi ni KUAMINI )

Mariko 11:25, Mnaposimama kusali, SAMEHENI kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu.*fg* hata Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu." ( Kanuni ni KUSAMEHE )

Mariko 9:29, Naye akawaambia, "Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa Kuomba na kufunga tu." ( Kanuni ni kuomba na KUFUNGA)

Mathayo 7:7, "Ombeni, nanyi mtapewa; ( Kanuni ni KUOMBA )

 

John 9:31, Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake.( Hapa kuna kanuni tatu:

1)      Lazima uwe UMEOKOKA na KUSAMEHEWA DHAMBI,

2)      Uwe mtu wa KUMCHA na KUMWABUDU Mungu,

3)      Uwe wa KUTIMIZA / KUFANYA MAPENZI YA MUNGU.

 

 

 

                      43. MAOMBI NA SHUKRANI KWA MUNGU SIKU ZOTE.

 

1 Wathesalonike 5:17-18,“salini kila wakati, ms 18, na muwe na shukrani katika kila hali.....

 

 

                      44. ROHO YA NEEMA NA KUOMBA.

 

Zakariah 12:10, Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.

 

Roho ya neema na maombi inapatikana kwa wakristo kama msaada katika maombi na maombezi, - ikiwa utafuata masharti!

 

                     

 

                      45. MAOMBI NA KUABUDU KATIKA WIMBO.

 

Kuabudu ni neno lingine la Kumpenda Yesu. Pia ni aina ya maombi, ila tu ni kipitia wimbo.

 

Kuabudu na kuimba katika roho kwa sauti moja pia ni maombi, lakini kwa lugha isiyo julikana.

 

 

 

                      46. MAOMBI YA KUJENGA:

 

Isaiya 40:31, bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

 

Kungojea bwana ni kuwa kimnya na kusikiliza bwana kwa hali ya kumsujudu na kushukuru na kunyenyekea. Ni kule kusikia kile bwana ananena na ROHO yako!

 

Mara kwa mara, unaongelesha ( kuomba ) Mungu hadi ikawa ni vigumu kwa Baba kunena nawe, japokuwa wewe ni mwanawe mpemdwa.

 

Maombi hasili ni kuwasiliana wote wawili, sio kwamba unaongea tu peke yako.

 

 

 

                      47. MAOMBI NA KUBATIZWA KWA MOTO.

 

Luka Mtakatifu 3:16,…Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa MOTO”.

 

Matendo ya Mitume 2:3, Kisha, vikatokea vitu vilivyoonekana kama ndimi za MOTO, vikagawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao.

 

Matendo ya Mitume 1:8, Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni ninyi, mtajazwa nguvu…..”

 

Luka 24:49,…..lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu."

 

 

                      48. MAOMBI NA MAJARIBU.

 

Sio dhambi kujaribiwa, lakini kuangukia  majaribu ni dhambi.

 

Yesu akasema katika Luka 22:40, "Salini, msije mkaingia katika kishawishi." Ms 46, "Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi."

1 Wakorinto 10:13, Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.

Namna ya kushinda majaribu ni kuomba.

 

 

 

                      49. MAOMBI NA UTUKUFU WA MUNGU.

 

Luka 9:28-29,....Yesu aliwachukua Petro, Yohane na Yakobo, akaenda nao mlimani kusali. Ms. 29, Alipokuwa akisali, sura yake ilibadilika, mavazi yake yakawa meupe na kung`aa sana. Ms 34, Petro alipokuwa akisema hayo, mara wingu likatokea na kuwafunika; na wingu hilo lilipowajia, wale wanafunzi waliogopa sana.

 

 

 

                      50. MBINU ZA MAOMBI, MAOMBI NA KUFANYA MAOMBI.

 

a)      Wakati wa kuomba haijalishi,

 

Watu wengine wanapenda kuomba asubuhi, wakati akili zao bado safi.

 

Wengine hupenda kuomba jioni, wakati shughuli zote zimeisha.

 

Wengine huona wakati mzuri wa maombi ni usiku, wakati kila kitu kimekimnya.

 

-         Chagua wakati unao kufaa wewe. Sana sana watu wengi hawana wakati wa kuomba kabisa. Lazima UTENGE muda wa maombi.

 

 

b)      Jinsi utakavyokaa unapoomba pia haijalishi.

 

Watu wengine wanaomba wakiwa wamefunga macho. Wengine husema Yesu aliinua macho yake mbinguni na kisha akaomba, hata hivyo wengine huomba macho yao yakiwa wazi.

 

Uwezi kumwona Mungu na macho yako ya kawaida. Fungua macho yako ya Kiroho.

 

Wengine huomba kama wamepiga magoti, na wengine wakisimama.

 

 

Wengine wanamuda mzuri wa maombi wakitembea na wengine wanachumba cha maombi kwenye vitanda vyao.

Wengine huomba wakifanya kazi zao na hata hivyo maombi haitazuia shughuli za kawaida.

 

La muhimu ni kwamba mradi tu UMEOMBA.

 

c)      Je, naweza omba nikipasa sauti ama ninongoneze maombi yangu kwa Mungu?.

( Hannah alifanya hivyo ) Naweza kuelekeza mawaso yangu kwa maombi ama kilio changu kwa Mungu? – Yote ni juu yako, jinsi inavyo kupendeza, ama kuamua.

 

 

d)      Maombi mafupi ama marefu.

 Mhubiri mmoja aliulizwa; Unaomba maombi marefu? Jibu lake lilikuwa, Si ombi kwa lisali moja bali lisali moja halitaisha kabla sijaomba!

 

Ups – huyo mtu huomba na tena mara kwa mara.

 

Ikiwa unaona ughumu wa kuomba maombi marefu, unaweza omba mafupi, yenye maana na inajielekeza.

 

Usi ngoje roho Mtakatifu aje kwa nguvu juu yako kuanzia mwanzo, wakati mwingine inagharimu kujitolea kuanza kuomba.

 

e)      Wakati tunaomba katika mkutano, twaweza kuomba wote kwa kauli moja ama tutaomba moja baada ya mwingine? Kiongozi mzuri wa mkutano atafanya uamuzi unaofaa.

 

f)       Naweza omba zaidi katika ndimi? ( Paulo alifanya hivyo )

Kuomba sana katika ndimi hujenga roho yako.

Naweza omba kwa ndani kwenye mkutano ama ni nyamaze?

Kuwa makini kwa ROHO MTAKATIFU na umuachie akuongoze na akuelekeze.

 

 

 

51.KUPUUZA MAOMBI.

 

Maombi ni pumsi ya moyo.

 

Mtu akiacha kupumua, atakufa haraka sana.

 

Ikiwa mkristo atasahau kuomba, anakufa kiroho. Anakuwa ni mtu aliye rudi nyuma.