Index 

 

DHIHIRISHO YA ROHO MTAKATIFU 


By Vagn Rasmussen.  Translated by Jackline J. Kristensen.

 

 

                                                                                       Last update april 2008

 

 

Dhihirisho ya Roho Mtakatifu.

 

Roho Mtakatifu katika asili ya kihebrania.:RUAH ( hutamkwa kama RUACH ) kumaanisha,hewa inayotembea, pumsi ama pumsi ya UZIMA. RUAH ni sawa na jina la Kiyunani: PHNEUMA.

 

Roho Mtakatifu ni kama baba na mwana:wa milele, haina kipimo, haikuumbwa, ni Mungu wa kweli na ni bwana, ametoka kwa baba na kutumwa na mwana.

 

 

Yaliyomo:

 

1.         Usawa wa Roho mtakatifu. Majina ya Roho Mtakatifu.

 

2.         Roho Mtakatifu kama Mungu, utatu wa Mungu.

 

3.         Roho Mtakatifu kama Mtu.

 

4.         Roho Mtakatifu, Jukumu na kazi ya Roho Mtakatifu.

 

5.         Roho Mtakatifu kama mfariji na mwalimu wetu.

 

6.         Roho Mtakatifu na vipawa tisa vya Roho.

 

7.         Roho Mtakatifu na makao yake.

 

8.         Roho Mtakatifu na pingamizi za Roho Mtakatifu.Kuhusunisha Roho mtakatifu.

 

9.         Ubatizo katika Roho Mtakatifu.

 

10.     Roho mtakatifu na kanisa.

 

11.     Roho Mtakatifu na Nguvu,uweza wa kiungu, nguvu za kiungu,afya na msaada wa kiungu, usafirishaji wa kiungu.

 

12.     Roho mtakatifu na dhambi siyosameheka.

 

13.     Roho mtakatifu kama mwalimu na mfariji.

 

14.Roho mtakatifu na kukubali dhambi zako

 

15.Roho Mtakatifu na huduma.

 

16.Upako wa Roho Mtakatifu.

 

17.Ujazo wa Roho Mtakatifu.Kujazwa kwa Roho mtakatifu

 

18.Roho Mtakatifu na Roho ya uombezi.

 

19.Roho Mtakatifu na Ufufuo.

 

20.Roho Mtakatifu na utukufu wa Mungu.( Shekina, Kabod, Gloria).

 

21.Roho Mtakatifu na matunda ya Roho.

 

22.Roho Mtakatifu na uhisho kwa mahubiri, Nyimbo na Kuabudu na uimbaji.

 

23. Roho Mtakatifu na  miujiza(mysticism). Ukweli na uongo.

 

24.Roho Mtakatifu na uongozi.( Njia saba ya uongozi )

 

25.Roho Mtakatifu na huisho wa neno la Mungu.

 

26.Roho mtakatifu na Yesu kama msaliwa wa kwanza na wa pekee wa Mungu Yahweh, baba.

 

27.Roho Mtakatifu na manabii wa agano la kale.

 

28.Roho Mtakatifu na hekalu.

 

29.Roho mtakatifu na ubatizo katika Roho na moto.

 

30.Roho Mtakatifu na kuubiri injili.

 

31.Roho Mtakatifu na mwanzo.(Genesis)

 

32.Roho Mtakatifu na silaha kamili za Mungu.

 

33.Roho Mtakatifu waweza kukasirishwa.

 

34.Roho Mtakatifu na Nguvu za Kiungu.

 

35.Roho Mtakatifu na kuzaliwa mara ya pili.(wokovu)

 

36.Roho Mtakatifu na roho ya mwanadamu(ki utu)

 

37.Roho Mtakatifu na umoja wa kweli.

 

38.Roho mtakatifu na Roho ya maombi.

 

39.Roho mtakatifu na kuabudu.

 

 

1.     USAWA WA ROHO MTAKATIFU. MAJINA YA ROHO MTAKATIFU.

 

Roho wa Mungu, wa baba, ya mwokozi, ya Kristu, ya mwana, wa ukweli, ya uzima, ya utukufu, ya nguvu, wa ushuhuda, wa maarifa, ya ufunuo, wakili, mfariji, mwalimu, njiwa, moto, nguvu, maji, mafuta, mhuri.

 

2.     ROHO MTAKATIFU KAMA MUNGU WA KWELI, UTATU WA MUNGU.

 

a)Tuna batizwa katika JINA la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu. Mathayo 28:19.Tuna batiswa katika jina la UTATU wa Mungu.

Maandiko yatuonyesha kwamba utu utatu wa Mungu ni MUNGU MMOJA.

 

b) Mwanzo 1:26, Na tumfanye mtu kwa mfano WETU…….

 

Katika andiko la kiebrania, hali ya uwingi umetumika.Wote utatu wa Mungu walikuweko katika uumbaji. Yahweh baba, Yeshua Messia na Mungu Roho Mtakatifu.

                     

 

3.     ROHO MTAKATIFU KAMA MTU:

Tazama pia: Wakili, hunena, Hushuhudia, Anasauti, huzuni, hufu, hushawishi, huongoza, tabia, hufunza,hukumbusha, hufariji. Haya yote ni majina ambayo tunamwuta Roho Mtakatifu kama Mtu.

 

Katika Yohana 16. Hapa Roho Mtakatifu ametajwa mara nyingi kama YEYE, Mtu wa kiume ( He).

 

 

4.     ROHO MTAKATIFU, JUKUMU NA KAZI YA ROHO MTAKATIFU

 

Jukumu lake ni ku…shawishi, zalisha,fundisha, elekeza,             , wito, shuhudia, boresha tabia, kumbusha, fariji, leta maarifa, takaza, paka, angaza, fanya upya, huisha, batiza, jaza..

 

Warumi 5:5…

 

 

Roho Mtakatifu humwaga upendo wake wa kiungu katika mioyo zetu. Anaumba, anaponya, na anatenda miujiza. Yeye ndiye nguvu utokanao kwa Mungu Yahweh.

 

Yeye, Roho Mtakatifu, huomba NDANI  yetu na KUPITIA kwetu, HADI kwa Mungu baba.

 

 

5.     ROHO MTAKATIFU KAMA MFARIJI NA MWALIMU.

Tazama pia, Kuadhibisha, fundisha, Kumbusha, elekeza, elimisha, Shuhudia, Sadikisha, Huzunishwa, Mfuasi.

 

Matendo ya mitume 9:31,… na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.

 

Luka Mtakatifu 12:12,.. Roho Mtakatifu atawafundisheni…..

Yohana 14:26,… lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni.

 

 

                      ROHO MTAKATIFU NA VIPAWA .

 

 1. Kunena na ndimi

 

 1. Kutafsiri ndimi

 

 1. Kipawa cha unabii ( Njia 6 za kuamua unabii )

 

 1. Neno la Maarifa

 

 1. Neno la hekima

 

 1. Kubambanua miroho

 

 1. Vipawa vya uponyaji

 

 1. Kipawa cha miujiza

 

 1. Kipawa cha imani.

 

 

Kubatizwa katika Roho Mtakatifu ni mwanzo ya kuhudumu katika vipawa 9 vya Roho Mtakatifu.

 

Ni : Vipawa 3 vya

-         Kunena kwa Lugha

-         Kipawa cha unabii

-         Kutafsiri ndimi

 

                Vipawa 3 Ufunuo,

-         Neno la hekima

-         Neno la Maarifa

-         Kubambanua ndimi

 

                  Vipawa 3 vya Nguvu,

-         Kipawa cha uponyaji

-         Kipawa cha miujiza

-         Kipawa cha Imani.

 

1. Kunena katika ndimi. Matendo ya Mitume 2:

 

Wakati mtu anaponena kwa lugha, akili na ufahamu hupumzika.

 

Roho Mtakatifu anatumia kinywa cha mtu tu, sio bongo au akili ya mtu.

 

Usemi ni ya kiroho

 

Kuna aina nyingi za kunena kwa lugha. ( Lugha mbali mbali )

 

 

Kusudi ya kunena kwa lugha:

 

1.      Ni dhihirisho ya kiroho ya kubatizwa katika Roho Mtakatifu ( Matendo ya Mitume 10:46)

 

 1. Ili mwanadamu aweze kuwasiliana na Mungu Kiroho. ( 1 Wakorintho 14: 2 )

 

 1. Ili waumini wamtukuze Mungu. ( Matendo ya Mitume 10:46)

 

 1. Ili itubariki sisi wenye. ( 1 Wakorintho 14:39)

 

 1. Ili itubariki katika nyimbo katika Roho. ( Wakolosai 3:16)

 

 1. Ili roho zetu, mbali na mawaso yetu, iweze kuomba. ( 1 Wakorintho 14:14)

 

 1. Kwamba pamoja na kutafsiriwa kwa lugha, kanisa iweze kuinuliwa. ( 1 Wakorintho 14:12,13,5,26.)

 

 1. Ndimi ni kama ishara kwa wale wasio amini. ( 1 Wakorintho 14:22)

 

 

 

 

 

 

2. Kutafsiri ndimi ( Lugha )

 

Kutafsiri  lugha ni katika hali ya kiroho, usemi wa kiajabu.

 

Inahusika hasa na kunena kwa lugha.

 

Kuna mashauri machache kuhusu maswali ambayo mara kwa mara inaulizwa:

 

 1. Kutafsiri ndimi sio sawa na kutafsiri lugha moja hadi lingine. Kutafsiri lugha fulani ni kutafsiri neno kwa neno bali kutafsiri ndimi ni kutoa maana.

 

      Kutafsiri ndimi yaweza kuwa kupitia picha, maelezo ama kinaganaga.

 

2.      Asili, vipawa vya kiasili, na elimu na pia utaifa wa mwenye kutafsiri ita adhiri utafsiri bali kipawa sio kwa ajili hiyo ila kwa miujiza.

 

 1. Wale ambao hunena  kwa ndimi ni bora waombe kwa ajili ya kipawa hiki cha kutafsiri. ( 1 Wakorinto 14:13)

 

 1. Mtu asitafsiri. ( 1 Wakorinto 14:27)

 

 1. Kutoa ujumbe kwa lugha mengine na kujitafsiria yaweza kujizoeza.

 

 1. Andiko yatueleza tusitoe zaidi ya ujumbe tatu katika mkutano moja. ( 1 Wakorinto 14:27 )

 

 

 

3. Unabii.

 

Kiyunani: profemi=kunena, kutabiri, kubashiri.

 

Kiyunani:profetes=Mnabii.

 

Kutoa unabii:Kunena kwa ajili ya mwingine, kuwa msemaji wa Mungu.

 

Unabii kwa urahisi inatokana na msingi wa kiungu na msemo uliopakwa mafuta.

 

Kuna tofauti kati ya kipawa cha unabii na huduma ya mnabii.

 

Mnabii kama afisi hunena kwa miji, mataifa ama dunia nzima. Kipawa cha unabii sana sana hutumika kuhudumia watu na umati.

 

 

Kusudi la Unabii.

 

1.      Unabii ni kunenea watu katika hali ya kiroho. ( 1 Wakorinto 14:3)

 

 1. Kujenga kanisa – mwili wa waumini. ( 1 Wakorinto 14:4)

 

 1. Kuinua kanisa ( 1 Wakorinto 14:3) Kuinua haimaanishi kukemea.

 

 1. Kufariji Kanisa ( 1 Wakorintho 14:3,31)

 

 1. Iliwaumini wafundishike. ( 1 Wakorintho 14:31)

 

 1. Kushawishi asiyeamini na kudhiirisha siri za moyo wake. ( 1 Wakorintho 14:24,25)

 

Maswali zaidi kuhusu matumizi na udhabiti.

 

A: Tunaamuriwa tutamani hasa kipawa hiki. ( 1 Wakorintho 14:1)

 

B: Unabii ni kuu kuliko ndimi wakati haijaambatanishwa na utafsiri – ikiwa ujumbe utatafsiriwa,basi zatakuwa vya karama sawa.

 

C: Ingawa unabii ni wasi kwa kuelewa, sio kunena na ufahamu. Ni Roho wa mungu ananena kupitia mwanadamu.

 

D: Muumini aweza kupata kipawa cha unabii ( ama yeyote ile) katika ujazo/ ubatizo wa Roho Mtakatifu pamoja na kunena kwa lugha ( Matendo ya Mitume 19:6)

 

E: Unabii haichukui nafasi ya neno lililoandikwa,

 

F: Neno la Mungu ni msaada ulioimara, Kila unabii ambao unapinga neno la Mungu twaweza kana, kataa bila hofu.

 

G: Aliye na kipawa hicho anawajibika kwa utumizi, kutotumia jinsi inavyoitajika, Kufinyilia chini au udhabiti.

 

H: Roho wa unabii hutii mnabii. ( 1 Wakorintho14:32)

 

I: Paulo pia alisema; ” Wasizidi watatu wenye kutoa unabii katika mkutano moja. (1 Wakorintho 14:29) na wengine waamue.

 

J: Ujumbe wa unabii wakati mwingine haiwezi kubainika na kueleweka vizuri. (Mafuta unaotiririka Mwambao ya magharibi ya Norwe)

 

 

 

 

 

 

 

 

__________________________________________________________________________

  

Unabii:

Mzee mmoja, Martin Anderson, kutoka kanisa la kipentekote kule Moss, Norwe, alishuhudia unabii huu kule Moss:

 

Wakati mafuta itatoka bahari za kaskazini na kutoka pwani ya Norwe, mambo yataanza kutendeka na kurudi kwake Yesu Kristu inakaribia.

 

Wakati haya maneno yalinenwa, watu walisimama kwenye miguu yao na mtu huyo aketi na aache kuongea maneno haya ya upusi, kwamba mafuta inapitishawa juu kwenye pwani ya Norwe. Kwa wakati huo, Ujumbe ulikuwa mgumu kuaminika, hata hivyo, sasa hivi kampuni nyingi za mafuta zinapampu mafuta kupitia pwani ya Norwe na nchi ya Norwe sasa inaongoza kwa kusafirisha mafuta duniani baada ya Saudi arabia

 

K: Inahitaji imani kutabiri.(.... Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake. Warumi 12:6)

 

Usitafute habari kuhusu maisha yako ya baadaye kwenye yafuatayo:

 

-         Horoscopes, Mpigaramli, Mwaguzi, Vyeti, Vyeti vya Tarot nk.

 

 

4. Neno la maarifa.

 

Neno la maarifa ni ufunuo wa Roho Mtakatifu kuhusu manbo fulani katika akili ya Mungu.

 

Sio kipawa vokal, ni kipawa cha ufunuo. Inakuwa vokal wakati inashirikishwa kwa wengine.

 

Ni kipande cha maarifa ya kiungu. Neno la maarifa inahusu yaliyopita ama wakati huu, haihusiki na wakati ujao/ usoni kama vile neno la hekima hufanya.

 

 

Kusudi la Kiungu:

 

1.      Kukanya mfalme kuhusu mpango wa adui ya kuharibu.

 

 1. Kuangaza na kutia moyo mtumishi wa Mungu aliyevunjika moyo.(1Wafalme 19:14-18)

 

 1. Kufichua mnafiki. ( 2 Wafalme 5:20-27)

 

 1. Kushawishi mwenye dhambi kuhusu haja ya mwokozi. ( Yohana 6:18,19,29.)

 

 1. Kutambua mtu aliyejificha. ( 1 Samwel 10:22)

 

 1. Kuonyesha mtu aliye na hitaji. ( Matendo ya mitume 9:11)

 

 1. Kubukua ufisadi kanisani.

 

 1. Kuonyesha mahali panapo stahili pa kukutania watu wa Mungu. ( Mariko 14:34-37)

 

 1. Kujua mawazo ya wanadamu.( Yohana 2:24) ( 1 Samuel 9:19).

 

 1. Neno la maarifa inaweza kusaidia sana katika maombi kamili kwa aidha mtumishi wa Mungu aliye katika dhiki ama wale ambao wanahitaji usaidizi wa Kiroho. ( Mmishinari anayekufa katika kijiji cha Afrika).

 

 1. Kupfidia watu waliopotea au rasilimali.

 

 1. Kutambua chanzo cha magonjwa a kupagawa.

 

 

5. Neno la Hekima

 

Ni hekima ya Mungu sio la Mwanadamu.

 

Neno la hekima laweza kuwasilishwa kupitia sauti ya kiungu. Inaweza pia wasilisha kwa mwaliko wa malaika, kupitia ndoto na maono, au kupitia kipawa cha unabii cha kiungu,ama ndimi na utafsiri wake.

 

Hekima inahusu siku zijazo.

 

Baadhi ya maandiko katika bililia ni kama yafuatayo:

 

 1. Kuonya na kuelekeza watu kuhusu ukumu ijayo na maafa. ( Mwanzo 6:13-22, na Mungu akamwambia Nuhu......)

 

 1. Kudhihirisha mpango wa Mungu kwa wale ambao atawatumia. ( Mwanzo 41:16, 28-41, Pharaoh – Joseph)

 

 1. Kuhakikishia mtumishi wa Mungu jukumu lake la kiungu. ( Kutoka 3:10, Musa alipotumwa kwa Pharaoh.)

 

 1. Kudhihirisha maagizo sahihi na jinsi ya kuabudu kiungu. ( Kutoka 25, Onyesho la jinsi hekalu litakavyo kuwa ladhihirishwa kwa Musa).

 

 1.  Uchanuzi wa pendelevu wa mungu kuhusu  neema kuu inayotolewa bure kwa wote.    ( Matendo ya mitume 10:9-16)

 

 1. Kuhakikisha ukombozi unayokuja katikati ya dhiki. ( Matendo ya mitume 27:24,

             Paulo usiogope! Ni lazima utasimama mbele ya Kaisari…)

 

7.      Kutoa hakikisho  ya baraka zijazo. ( Mwanzo 23: 10-15 )

 

Katika nyakati hizi:

 

   A. Neno la hekima huonya kuhusu hatari inayokaribia.

 

 Ushuhuda:

Binti mmoja aruhusu jambazi kwenye gari lake.

Ilifanyika katika magharibi mwa Denmark. Dada huyu Mkristo, alikuwa njiani kuelekea mahali pake pa kazi, akambeba mtu aliyesimama kando ya barara. Punde tu, mtu huyo alipoingia kwenye gari, dada alihisi moyoni mwake onyo kwamba kuna hatari inakaribia. Mwishowe aliuliza yule mtu atoke ili ampanguzie kioo cha nyuma ya gari lake, Kisha dada huyo akaonda na kumwacha mtu yule. Alipofika kazini, akapata mfuko chini ya gari lake na ndani yake kulikuwa na bunduki lililotiwa risasi. Hapo ndipo alipogundua mungu amemuepusha kutokana na hatari kubwa ambayo hangeweza fikiria nini kingetokea. Basi alikabidhi polisi bunduki hilo. Mungu huonya wanawe wakati mwingine kupitia neno la hekima.    

 

 

B. Kutambulisha au kudhibitisha wito wa umishionari.

 

Ushuhuda:

Wito wa umishionari kwa Axel Jensen katika Zion Oelgod, Denmark:

Mmoja wa wazee Asimulia kuhusu tukio lilitokea hapa kanisani kwetu katika siku za kale. Katika jumapili moja asubuhi, Mbaba mmoja na mwanawe ( kijana mdogo ) walikuwa wanasafafiri kwenye gari la moshi. Walipofika kituo cha oelgod, ilikuwa masaa za ibada, waliamua kutua kidogo wahudhurie ibada kasha baadaye waendelee na safari yao. Mhubiri wa jumapili hii akatoa unabii. Ujumbe ulikuwa mwito kwa kijana huyo mdogo, mwito wa kufanyika mmishionari. Jina lake ni Axel Jensen. Miaka mingi baada ya tukio hili akawa mmishionari aliyejulikana sana Afrika na baadaye China.

 Roho mtakatifu anajua moyo wa mwanadamu, hata kwa kijana mdogo kama huyu. Katika kipawa cha unabii na neno la hekima kupitia kwa roho mtakatifu ukatoa maagizo na kudhihirisha mpango wa Mungu katika siku zijaso  kwa kijana mdogo.

 

 

C. Kudhihirisha siku za usoni.

 

D. Kutoa maelekezo kwa mtu binafsi.

 

 

6.Kupambanua miroho.

 

Utumizi wa vipawa vya roho katika nyakati hizi ni sawa na vile ilivyo kwenye bibilia:

 

1. Kusaidia katika ukombozi kwa walio teseka, gandamizwa na kuadhibiwa. ( Mariko 5:5, ”Mchana na usiku alikaa makaburini na milimani akipaaza sauti na kujikatakata kwa mawe.”

 

Miroho michafu yaweza kusabisha uasimu, udhaifu na maelfu ya magonjwa mbali mbali.

 

2. Kutambua mtumishi wa shatani. ( Matendo ya mitume 13:9-10,

“Basi, Saulo ambaye aliitwa pia Paulo, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alimkodolea macho huyo mchawi, akasema, "Mdanganyifu wa kupindukia na mlaghai wewe! Wewe ni mtoto wa Ibilisi! Wewe ni adui wa chochote kile kilicho cha kweli; hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotosha njia za Bwana zilizonyoka“

 

3. Kusaidia katika kuangalia mipango ya mwaribivu.( Matendo ay Mitume 16:16) Paulo atambua roho ya uaguzi.)

 

4. Kuweka wazi makosa. ( mafundisho ya mapepo na laana zake.( 1 Tim 6:1, 2 Pet 2:1)

 

5. Kuweko wazi watenda-miujiza za kipepo.( 2 Tesalonike 2:9,Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,”

 

7.(Vi)pawa vya uponyaji.

Huu ni uponyaji wa kipekee kupitia kwa Roho mtakatifu, bila matibabu wala ujuzi wowote ule wa kisayansi. Baadhi ya wakristo hupenda kusema:, ”Mungu pia hutumia madaktari.” Kwa hakika ndivyo, lakini SIYO kuhusu vipawa vya uponyaji, Roho mtakatifu PEKEE hufanya kazi hapa. Madaktari bado ni njia ya kiasili ya uponyaji.

Vipawa vya uponyaji hufaya kazi kwa imani na kwa kuwekea mikono kichani kwa muumini ama tu kwa kuamini maombi.

Imani:dhambi ya kutoamini haihusu kusindikana kwa uponyaji – bali inahusu dhambi ya kutoamini katika Yesu kristu mwana wa Mungu.

Vipawa vya uponyaji imeandikwa katika uwingi katika maandiko asili.

Ni kama ifuatavyo:

1.      Uponyaji wa magonjwa katika mwili.

2.      Uponyaji wa ulemavu.

3.      Uponyaji wa hisia, na kumbukumbu.

4.      Uponyaji wa akili, ukichaa na kadhalika

5.      Uponyaji kwa uweza wa miujiza.

6.      Uponyaji kwa kupakwa kwa mafuta.

7.      Uponyaji kupitia nguo uliopakwa mafuta.

8.      Uponyaji kupitia punguo.

 

Kwa kuongezea:

9.      Uponyaji wa kiasili kupitia nguvu za mwilini.

10.  Uponyaji kupitia kufunga.

11.  Uponyaji kupitia Mungu anapotuma neno lake la uponyaji, kama jibu kwa maombi. ( Zaburi 107:20 )

 

Uponyaji kupitia matibabu na upasuaji ni njia ya kiasili sio njia ya uponyaji wa kiungu.

Uponyaji kupitia kufunga sio uponyaji kutokana na vipawa vya uponyaji, bali ni kutumia njia ya uweza wa kiasili ya mwili kujitawasha na kujirejesha na hivyo uponyaji unafanyika.

Mifano katoka bibilia kwa ajili ya kufafanua zaidi:

a)      Kwanza kabisa, vipawa vya uponyaji unaleta ukombozi kutokana na magonjwa na kuharibu kazi za ibilisi mwilini mwa mwanadamu.

Matayo 8:2-4 ( Luka 5:12-16 ) Yesu aponya ukoma.

Matayo 9:1-8 ( Luka 5:17-26 ) Yesu aponya mtu kiwete ugonjwa wa mifupa.

Matayo 9:27-31. Vipovu wawili waponywa?

Matayo 14:34-36, Yesu akiponya wengi.

Matayo 9:18-26,( Mariko 5:21-43 ) Mwanamke aponywa ugonjwa wa damu.

 

b)      Uponyaji wa kiungu sio sawa na ukombozi kutokana na nguvu za giza.

 

Mifano ya uponyaji baada ya ukombozi kwa sababu nguvu za giza mara kwa mara husababisha aina nyingi ya magonjwa:

Matayo 9:32-34, bubu na aliyepagawa aponywa.

Matayo 15:21-28, Yes aponya mtoto mdogo msiria kutokana na nguvu za giza.

Matayo 17:14-21, kijana mwenye kichaa aponywa.

Luke 13:10-17, Mwanamke aliyefungwa na nguvu za giza awekwa huru.

 

c)      Kudhibitisha madai ya kushangaza za Yesu:

Yohana 10:37-38, Kama sifanyi kazi za Baba yangu msiniamini, Lakini ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, walau ziaminini hizo kazi mpate kujua na kutambua kwamba Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake."

d)      Kumamlakisha ujumbe wa habari njema ihubiriwayo na watumishi wa Mungu.

 

Wakati viwete wanatembea, vibovu wanaona, wagonjwa wanaponywa, mapepo yafukuzwa, yote katika jina la Yesu, kila mtu atajua kwamba Yesu hakika yu HAI, na alifufuka kutoka kwa wavu.

e)      Kuvuta watu waje kwa kristo, waje wasikie habari njema.

Kila mmoja ameona umati kubwa wakingoja mlangoni mwa mkutanoni wakingojea zamu   yao ya kupokea uponyaji, je, sio nguvu hizi za vipawa vya uponyaji inayo wa vutia kuja kuudhuria mkutano na wengi pamoja na wao?

f)       Kuresha watu kwa Mungu:

Peter akiwa Lydda. Matendo ya mitume 9:33-35, Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Enea ambaye kwa muda wa miaka minane alikuwa amelala kitandani kwa sababu alikuwa amepooza, v34Basi, Petro akamwambia, "Enea, Yesu Kristo anakuponya. Amka utandike kitanda chako." Enea akaamka mara.v35Wakazi wote wa Luda na Saroni walimwona Enea, na wote wakamgeukia Bwana.

g)      Kushawishi wasiomini kuhusu ukweli wa neon la Mungu.

Hakuna lililo la nguvu la kuvutia asiyeamini zaidi ya uponyaji wa kimiujiza, ambalo hauwezi kuikataa wala kuipuuza.

h)      Kuleta utukufu kwa Mungu, Halleluyah:

Na watu wakashangilia kwa ajili ya matendo matakatifu yalifanywa naye. Mariko 2:12, Luke 13-17.

i)        Kuinua imani na ushujaa katika watu wa Mungu:

 

Wakati mwinjilisti anapoombea wagonjwa kisha wakapona, wote tunainuliwa hadi kiwango kingine cha imani na tunahisi kutiwa ujasiri kufanya hivyo.

 

Upako wa mafuta ( Yakobo 5:14 ) sio kupitia kazi ya vipawa vya uponyaji kwa roho bali ni jawabu kutokana na kutii na pia kwa majibu ya kuamini katika maombi.

Wazee na wahudumu ndio wanajukumu la kutekeleza upako wa mafuta.

Mchungaji ndiye mkuu wa viongozi.

Kuwekelewa mikono sio tu kwa walio na vipawa vya Roho, bali nikitendo cha imani ya kila mmoja na kwa kila mmoja.

Ilhali upako wa mafuta ni kwa wale wagonjwa waaminio.

Kwanini sio wote huponywa?

Kulikuwa na watu wengi wagonjwa katika kizima cha Betsaida – ni mmoja tu aliponywa- na hiyo kwa mshindi wetu Yesu Kristo. Tunaweza waza kwamba Yesu ataponya wote lakini hakufanya hivyo, kwa ajili ya sababu isiyojulikani.

Imeandikwa: kwa sababu ya kutoamini kwao katika mji huo, yesu hakufanya muujiza yeyote ile ama kuponya. Matayo 13:58, “Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao.”

Wakati mwingine kutosamehe ni sababu ya mtu kutopona ijapo maombi mengi yamefanywa.

Wakati mwingine kazi za miungu mingine (occult ) ina zuia uponyaji.

Wakati mwingine nadhiri iliyovunjwa ni kisuizi.

Wakati mwingine kutoamini maishani mwetu ndio sababu.

Wakati mwingine ibada ya sanamu (miungu mengine) imeharibu uhusiano wetu na Mungu.

Pengine wakati mwingi kutoamini tu ndio sababu, kupuuza neno la Mungu kama neno lililoandikwa.

Mahali ambapo haustahili kutafuta uponyaji:

(Zonetherapi – Acupunture – Hypnosis – Pendulum – Homeopathic – copper arm rings – means of protection against radiation from the underground – mesmerism – Wanaoponya bila kutumia jina la Yesu – uchawi – uganguzi mweupe na mweuzi – n. k ( samahani, maneno mengi hayaelezeki kwa kiswahili. )

 

MIUJIZA:

Maana: Muujiza ni njia ya kiungu inayodhihirishwa katika hali ya kawaida ya kiasili. Muujiza ni tendo la Roho wa Mungu. Ni kitanguo cha sheria za kawaida.

Haiwezi kuelezeka pasipo nguvu za Mungu. Kipawa cha muujiza ni kipawa cha nguvu.

Uponyaji wote mwilini mwa mwanadamu, ulemavu na kivunjo – hata uponyaji wa kitaalamu, unatokana na kipawa cha uponyaji, kwa sababu inatendeka ndani ya mwili. Hii haitakuwa utendaji wa miujiza.

Tofauti kati ya kipawa cha imani na kipawa cha miujiza ni : Miujiza hutendeka papo hapo na kwa njia ya kustaajabu ilhali, kipawa cha imanihufanya kazi kwa muda mrefu na sana sana sio la kustajabisha bali bado ni kipawa chenye nguvu kwa vipawa vyote.

Baadhi ya maandiko ya kipawa kinavyotumika:

Kipawa kilitumika kwa ukombozi wa kimuujiza kwa wana wa Mungu kutoka mkono ya adui.

Kutoka 14:16, Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu. Nao majeshi ya wamisri pia litaingia bahari mtakapopita nitasababisha maji yarudi pamoja na Jeshi la Farao lote litaangamia. Miujiza mengi yalitendeka hapa.

 Kuzaidia walio na hitaji.

Kutoka 14: Musa mara tena kainua fimbo na kugonga mwamba, na maji yakatiririka, mengi inayotosha kunywesha wanawaisreli milioni 1.5 jangwani. Hii ni ukumbusho kwetu kwamba Yesu ndiye mwamba wetu.

Mariko 6:36-37, Yesu afanya muujiza wa kulisha umati kubwa, kwa hakika ni muujiza.

 

Ushuhuda:

Ilitendeka kule China, Watoto waliokuwa na njaa walikuwa kwa maombi, biwi la ngano liliangushwa papo hapo kwenye watoto walikuwa wakiomba kwa Yehovah Jireh, kwa hakika ni jibu la kiajabu la maombi.

 

Kufanya uamuzi wa kiungu na nidhamu:

Tauni kumi za mizri zilikuwa miujiza kumi kutoa nidhamu, kumpa Farao nafasi ya mwisho ya kutubu na kuwapa watu wa Mungu uhuru wao wa kuondoka, lakini hakukubali, ilhali alipata nafasi ya mwisho.

Kudhibitisha neno lililo hubiriwa.

Matendo ya mitume 13:11-12, ni mafundisho ya nani yalikuwa kweli, Elymas ama Paulo, Muujiza ulifanya Elymas muofu, katika giza, kipofu kwa muda na maneno ya Paulo yakakubalika na kuaminika.

Kutuliza hali siziso epukika katika hali ya hatari.

Matayo 13:23, Yesu atuliza mawimbi katika bahari la Galilaya.

Kufufua walio kufa.

Kijana wa njane, Lazaro, Tabitha.

Kudhihirisha nguvu za Mungu na ukuu wake.

Fununu kuhusu Yesu akitenda miujiza ilifanya watu wamtukuze na wamheshimu Mungu.

John 4:48,  Yesu akamwambia, "Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!"

Luka 1:5, ububu wa Zachariah, Vs 64, Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariya      vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu.

Katika maandiko kumejaa mifano mengi ya miujiza ya kiungu, hata leo waumini, wamishonari, mitume, wainjilisti waweza kushuhudia miujiza mengi yanayofanyika kwa -  utukufu wa Mungu.

Mahali ambapo haustahili kutafuta miujiza!

Uaguzi wa maji – Voodoo – Uchawi n.k.

 

KIPAWA CHA IMANI.

Kipawa cha imani ndio bado kipawa chenye nguvu kati ya vipawa zote tatu vya nguvu – kipawa cha uponyaji – kipawa cha muujiza – kipawa cha imani.

Kuna aina tofauti vya imani.

1)      Imani ya kuokoa. Aina hii hufanya kazi kabla ya mtu kuoka.

2)      Kuna pia imani asili; tunaamini kile ambacho tunasimuliwa kilitendeka katika kihistoria. Mkulima huamini kuna mavuno baada ya kupanda mbegu.

3)      Pia kuna imani kama tunda la Roho. Wagalatia 5:22, Imani ni tunda huleta tabia. Kipawa cha imani ni ya nguvu.

 

Imani kama tunda la Roho hukua, ( imani kama mbegu ya haradari ),  Imani kama kipawa ni kiwango fulani cha imani ambacho mtu hupewa mara moja. Iko tayari siku zote kutumika. Imani kama tunda hukua katika muumini, sio vile kwa kipawa cha imani, lakini inavyotumika zaidi ndivyo zaidi hupokelewa.

Imani cha kuokoa huja kabla ya mtu kuokoka.

Imani kama tunda huja baada ya mtu kuokoka.

Imani kama kipawa huja baa ya ubatizo katika Roho mtakatifu.

4)      Imani kama kipawa cha Roho mtakatifu, ni kiwango spesheli cha imani inayo pokekelewa kutoka kwa Mungu moja kwa moja. Ni imani ya Mungu.

 

Kipawa cha imani ni tofauti na kipawa cha muujiza kwa sababu; kipawa cha miujiuzi inaonekana ila haijatulia bali kipawa cha imani kimetulia na kinafanya kazi kwa mda mrefu, hata hivyo huwa cha nguvu zaidi mwishoni.

Kipawa cha imani ni chombo cha kiroho cha mhumini na mhuduma na ina,; baraka na laana, uumbaji na pia katika kubamoa, kuondoa ama kubadilisha hali, na mengine mengi.

Kipawa cha imani sana sana ni kitendo cha papo hapo, wakati mwingine cha kushangaza. Kipawa cha imani ni hatua inayoweza kufanyika kwa muda fulani lakini matokeo yake ni ya nguvu hata ingawa sio cha kuonekana.

Mwanzo 17:27, Isaka akibariki Yakobo ( Waebrania 11:20 )

Vipawa vyote tisa vya Roho vyafanya kazi kwa imani ( imani kama tunda la Roho ) hata kipawa cha imani inafanya kazi kwa imani( tunda la imani ), kama vile meli yote kubwa inaendeshwa kwa kutumia mafuta, sawa na malori.

Tunda la imani ndilo la muhimu machoni pa Mungu, ndio aina ya imani inayo heshimu Mungu na kufurahisha moyoni mwake. Kipawa cha imani haizai matunda kwa sababu ni imani ya Mungu mwenyewe inafanya kazi kupitia mtumishi wake.

Kipawa cha imani ni sehemu ya imani tunayokabidhiwa na Mungu, sehemu ya imani yake mwenyewe.Haikui kama tunda la imani bali inatiwa nguvu nalo.

Mifano kutoka maandiko:

Baraka za Miujiza 

Baraka za Isaka kwa Yakobo. Mwanzo 17:28, Waebrania 11:20.

Baraka za Yakobo kwa Ephraim na Manasseh

Unabii wa Nuhu kwa Cam ( laana pia inafanya kazi kwa imani )

Ulinzi katika nyakati za hatari

Danieli katika tundu la simba. Dan 6:17-23, Wahebrania 11:33

Paulo na nyoka. Matendo ya Mitume 18:5, Mariko 16:18.

Kuhifadhiwa kimujiza katika njaa na kwa kufunga.

Eliya katika kijito cha cherith. Kunguru walimletea nyama. 1 Wafalme  17:3-6

Mjane katika Zareptha. Unga na mafuta ilitosha hadi wakati mvua ilipoanza. 1 Wafalme 17:14-16.

Kupokea ahadi za Mungu za kustaajabisha.

Abrahamu hakuwa na shaka bali alikuwa na imani ya nguvu. Mwanzo 21:5, Warumi 4:20.

Kuadhibisha nidhamu ya kiroho kwa wanao kosa.

1 Wakorinto 5:1-5. Mtu aliyezini na mke wa babaye. Mwili wake ulikabidhiwa ibilisi na adhabu ya kiroho ukobadilisha maisha yake.

Elisha akiwazuia watoto wadhihaki. 2 Wafalme 11:2-3, 24.

Kwa ushindi wa kimujiza vitani.

Haruni na Hur wakishikilia mkono wa Musa. Kutoka 17:11

Kusaidia katika shida za kinyumbani na pia shinda kubwa kubwa.

Mwanamke mmaskini alipiwa deni zake kupitia kwa kipawa cha imani.2 Wafalme 4:1-7.

Kufufua wafu.

Hapa, vipawa zaidi ya moja inafanya kazi. Vipawa vya Roho wakati mwingine vinahusika pamoja. Kipawa cha uponyaji na kipawa cha kutenda miujiza vyaweza kuhusika pia katika kufufua wafu. Lazaro alikuwa mgonjwa na alipofufuliwa akawa mzima.

Pia imani ni kipawa kinacho tumika katika kutoa mapepo.

Imani kama kipawa na kubambanua miroho huweza kufanya kazi pamoja hapa.

Kuna mifano nyingi katika bibilia na hata sasa hii inatendeka kwa wahuduma wengi na wahumini pia.

Shetani na miroho ya kufisidi huiga vipawa zote tisa vya Roho mtakatifu. Kuna roho mchafu nyuma ya kila ibada isiyo ya kiungu.

Baadhi ya mapepo huiga vipawa vya Roho mtakatifu ni kama yafuatayo;

( Clairvoyance, familiar spirits, crystal ball, fortune telling, horoscopes, black magic, voodoo, witchcraft, water divination, spell, hypnosis, n.k ) Samahani kiswahili hakitafsiri sawasawa hapa ).

 

7.Roho Mtakatifu na makao yake:

Tazama pia, Wana wa Mungu, kanisa,( mwili wa Kristo ) na moyo.

Miili yetu ni hekalu ya Roho Mtakatifu. 1 Wakorinto 3:16, Je, hamjui kuwa, miili yenu ni hekalu…

Roho mtakatifu anaishi ndani yetu. Warumi 8:11, Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa uzima miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake AKKYE NDANI YENU.

MUNGU yuaishi ndani yetu kupitia kwa Roho. Waefeso 8:11, Katika kuungana naye, ninyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, muwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.

8.      Roho Mtakatifu na pingamizi za Roho Mtakatifu. Kukufuru Roho Mtakatifu:

Tazama pia: Ulimwengu, shetani, uofu, kutoamini, uongo, utu, Kuvunjika moyo

a).Pingamizi kwa Roho Mtakatifu:

Matendo ya Mitume 7:51,Enyi wakaidi wakuu! Mioyo na masikio yenu ni kama ya watu wa mataifa. Ninyi ni kama baba zenu. Siku zote mnampinga Roho Mtakatifu.

b).Kuhuzunisha Roho mtakatifu.

Waefeso 4:30, Msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu maana Roho huyo ni alama ya Mungu kwenu kwamba ninyi ni watu wake, na thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu atawakomboeni.

 

9. Ubatizo katika Roho Mtakatifu.

Luke 3:16,….Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Matendo ya mitume 1:5,…. Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache, ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu."

Matendo ya mitume 2:4,.. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema LUGHA MBALIMBALI kadiri Roho alivyowawezesha.

Matendo ya mitume 2:38,.. Tubuni na kila mmoja wenu abatizwe kwa jina la Yesu Kristo ili mpate kuondolewa dhambi zenu na kupokea ile zawadi ya Roho Mtakatifu.

10.Roho mtakatifu na kanisa.

Matendo ya mitume 4:31,Walipomaliza kusali, pale mahali walipokuwa wamekutanika pakatikiswa, nao wote wakajazwa Roho Mtakatifu. Wote wakaanza kuhubiri neno la Mungu bila uoga.

Matendo ya Mitume 9:31, Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.

M. ya mitume 15:28, Watume walitii  Roho mtakatifu.

Warumi 8:9,…. Yeyote asiye na Roho wa Kristo, huyo si wake Kristo.

M. ya mitume 10:47, "Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi wenyewe tulivyompokea. Je, kuna yeyote atakayeweza kuwazuia wasibatizwe kwa maji?"

11.Roho mtakatifu na vipawa, utawala wa kiungu juu ya sheria za kiasili, uweza, afya, egemio na uchukuzi.

a). Utawala wa kiajabu juu ya sheria za asili. 2 Wafalme 6:6.

b). Nguvu za kiajabu. Waamuzi 14:6, 16:3.

c). Afya na egemeo la kiajabu. Kumbu kumbu la torati 8:4.

d). Uchukuzi isiyo ya kawaida. M. ya mitume 8:39-40.

12.Roho mtakatifu na dhambi isiyosameheka:

a).Ukufuru wa Roho mtakatifu. Matayo 12:31, Kwa sababu hiyo, nawaambieni, watu watasamehewa dhambi na kufuru zao zote, lakini hawatasamehewa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.

b).Kudanganya Roho mtakatifu. M. ya mitume 5:3,9,10. Ms 3,mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu…..Ms 5, Anania aliposikia hayo, akaanguka chini, akafa……

13.Roho mtakatifu kama mwalimu na muombolezaji:

a). Roho mtakatifu hufundisha. 1. Wakorinto 2:13, Basi sisi twafundisha, si kwa maneno tuliyofundishwa kwa hekima ya binadamu, bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho.

b). Hufundisha wanafunzi kila kitu. Yohana 14:26, lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni

14.Roho mtakatifu dhamira ya dhambi:

a).Dhibitisho la dhambi. Yohana 16:8, Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu.

Roho mtakatifu ndiyo tu pekee awezawe kushawishi mtu kutoka dhambini. Dhamira ya mtu ni sehemu ya roho ya mtu. Roho mtakatifu hushawishi mtu kupitia DHAMIRA yake. Hatua ya kushawishi kutoka dhambini ni hakika kupitia Roho mtakatifu – kwa neema ya Mungu.

 

15.Roho mtakatifu na huduma.

Huduma inahusika pia na – uadimishaji wa vipawa vya Roho mtakatifu.

Huduma zatiwa upako wa Roho mtakatifu.

Roho mtakatifu huongoza kila huduma iliyo ya haki.

Mhuduma ndani yake ni makao ya Roho mtakatifu.

1 Cor 12:28 Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.

A). Mtume. Kigiriki: apostolos=”kutumwa” ( na Kristo ) pia ya maanisha kumamlakishwa na Kristo.

B). Nabii. Kigiriki: prophetes, inamaanisha “wito ama kutangaza mapenzi ya Kiungu.”.Hivyo ndivyo Yahweh asema”.Kwa ujumla, twaweza kusema wanabii ni waume na wanawake wanaopokea maono ama ndoto za kiungu ( kupitia uwezo wa Roho mtakatifu) ambayo wanapitisha kwa umati kwa usemi ama kwa vitendo.

C). Muinjilisti. Kigiriki: Euaggelistes=anaye tangaza habari njema.

D). Mchungaji. Kwa kigiriki maneno 3 ya viongozi wa kanisa imetajwa: Episkopos=Askovu, Poimen=Mchungaji( anayeshughulikia kondoo), Prebyteros=Wazee( katika uwingi kwa agano jibya).

E). Mwalimu. Kigiriki:Didaskalos=mwalimu.

F). Huduma ya usaidizi. ( Kipawa katika kuadimisha).

G). Huduma ya utawala. ( Kipawa katika upangaji ).

H). Shemasi. Kigiriki: Diakonos=Yule ambaye aliyepewa jukumu ya kuhuduma kwenye meza, karamu ya upendo.

I). Wazee. Kigiriki=elders, sio huduma bali ni ofisi maalum kanisani, pia aweza kusimamia huduma yeyote.

Tazama pia: Mafunzo katika huduma. ( The fivefold ministries).

 

16.Upako wa Roho Mtakatifu:

Luka 4:18-19, "Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa, Ms 19,na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana."

Yesu kristu alitiwa mafuta katika njia spesheli kuhubiri. Upoka ni Roho mtakatifu JUU yake. Kila mhuduma wa bwana ametiwa mafuta kwa kiwango Fulani – Zaidi au kidogo. Yesu ndiye mpakwa mafuta kuliko wote. Upako utaonekana katika maisha ya mhuduma. Mhuduma anavyojihuzisha katika huduma ndivyo anavyokuwa na upako zaidi.

17.Ujazo wa Roho Mtakatifu:kujazwa na Roho mtakatifu:

Mbali na kubatizwa katika Roho mtakatifu, ujazo wa Roho mtakatifu ni HATUA. Vile ubatizo katika Roho mtakatifu hufanyika mara moja katika maisha ya mtu, ujazo yaweza kuwa mara kwa mara.Ni hatua. Kama vile Paulo amesema katika waefeso 5:18-19,… bali mjazwe katika Roho mtakatifu. Ms 19,Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.

Njia moja ya kujazwa na Roho mtakatifu ni KUABUDU katika nyimbo na maombi ya kuabudu na shukrani.

Waweza kuomba kujazwa zaidi na zaidi na Roho mtakatifu.

Dhihirisho ya kwamba umejazwa na Roho mtakatifu ni matunda ya roho inaanza kuonekana maishani mwako.

Tazama pia Ujazo wa Roho mtakatifu na (the 4 temperaments).

18.Roho mtakatifu na maombi ya uombezi:

Hutupa nguvu katika maombi. Warumi 8:26-27,Hali kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka.Ms 27, Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu.

19.Roho mtakatifu na ufufuo.

Toba itokanayo na kushawishiwa na Roho mtakatifu ndiyo njia ya kweli na ya kibibilia ya kuleta ufufuo, haijalishi iwe ni ufufuo kwa taifa ama kwa mtu binafsi. Kila ufufuo ulio halali hutokana na uweza wa Roho mtakatifu ndani ya Mtu. Ufufuo utokanayo na bidii ama uwezo wa mwanadamu haudumu mda mrefu na baadaye huleta mwanguko mkubwa wakati moto huo umepoa.

Kitabu cha Yoel pia ni cha ufufuo. Yoeli 2:23,….kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika,…na mvua ya vuli, kama kwanza.

Yoeli 2:28-29, Hata itakuwa, baada ya hayo,ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; Ms 29,tena juu ya watumishi wenu waume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

Mstari kuu ya ufufuo, ahadi ya Mungu ya UFUFUO kwa watu WAKE: 2 Mambo ya nyakati 7:14,…ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

 

Matendo ya mitume 1:5, Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache, ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu."

Matendo ya mitume 1:8, Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni ninyi, mtajazwa nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia."

Kanisa la kwanza na ufufuo wa kwanza, msingi wake ulikuwa:

1)Ujazo wa roho mtakatifu,

2)Ubatizo wa roho mtakatifu na moto,

3)Kupokea nguvu za roho mtakatifu.

Huo ndio ulikuwa kielelezo ya mvua ya KWANZA.

Pendekezo ya Mungu kuhusu ufufuo haija badilika. Kielelezo ya mvua wa sasa(masika) ya ufufuo na kujengwa kwa kanisa, bado inatekelezwa katika roho mtakatifu kwa njia ile ile sawa na kielelezo ya “mvua ya kwanza” ufufuo, ile tu mvua wa ufufuo wa sasa, umwagikaji wa roho mtakatifu na moto na nguvu utakuwa ya kiwango cha juu kisicho onekana katika historia. Wakati mvua ya kwanza ulitolewa kwa kiasi, mvua ya sasa unamwagika kama mto. Yoeli 2:23-24.

Ufufuo hauji tu kwa kipindi fulani wala kutoka hewani. Pendekezo ya Mungu kuhusu matayarisho ya ufufuo haija badilika. Kitabu cha Yoeli, mnabii wa ufufuo, anakili: Yoeli 2:12-13, lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; Ms 13, rarueni mioyo yenu, wala si mavasi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.

Kufunga na kuomba na kutubu umekuwa usioepukika na chanzo cha matayarisho ya Ufufuo wa halali wa roho mtakatifu.

Tazama pia mafunzo kuhusu Kufunga: Kijitabu cha kufunga na kuomba.

Tazama pia: mafunzo kuhusu masharti za ufufuo, matayarisho ya ufufuo.

Tazama pia: mafunzo kanuni za ufufuo.

 

20.Roho mtakatifu na utukufu wa Mungu, ( Shekinah, Kabod, Gloria.)

Utukufu Wa Mungu Yahweh.

Yohana 17:22, Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi tulivyo mmoja;

Yesu atawapa utukufu wake waliokombolewa.

Matendo ya mitume 7:55, Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akatazama juu mbinguni, akauona utukufu wa Mungu na Yesu amekaa upande wa kulia wa Mungu.

Stefano, katika dakika zake za mwisho, kabla hajauwawa na wayahudi, aliona utukufu wa Mungu JUU mbinguni.

Musa pamoja na wana wa israeli, pia waliona utukufu wa Mungu na macho yao.

Kutoka 16:7, 10.

Ms. 7, na asubuhi ndipo mtakapoona utukufu wa BWANA; na sisi tu nani, hata mkatunung´unikia?......

Ms. 10, Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa BWANA ukaonekana katika hilo wingu.

Kutoka 40:34-35:

Ms. 34, Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.

Ms. 35, Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.

Tazama pia, Kutoka 29:43. Mambo ya walawi 9:4,6,23. Hesabu 14:10, 16. Hesabu 16:19,42.

Hesabu 20:6.

1 Wafalme 8:10-11.

Ms.10, Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu, nyumba ya BWANA ikajaa wingu.

Ms.11, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya BWANA ilikuwa imejaa utukufu wa BWANA.

2 Mambo ya nyakati 5:11-14:

Ms.11, Ikawa, makuhani walipotoka katika patakatifu,.......

Ms.12, tena walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana wao,na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoaazi na vinanda na vinubi......

Ms.13, hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA nao wakipasa sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA.

Ms.14, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya wingu lile; kwa kuwa nyumba ya BWANA ilikuwa imejaa utukufu wa BWANA.

2 Mambo ya nyakati 7:1-2:

Ms. 1, Basi Suleimani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa BWANA ukajaza nyumba.

Ms. 2, wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa BWANA, kwa sababu kwa kuwa utukufu wa BWANA umeijaza nyumba ya BWANA.

Isaya 58:8:

Ms. 8, Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.

Isaya 59:19:

Ms. 19, Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.

Utukufu wa BWANA ni – Roho wa BWANA!

Isaya 60:1-3:

Ms. 1,Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.

Ms. 2, Maana, tazama, giza litafunika dunia, na giza kuu litazifunika kabila za watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.

Ms. 3, Na mataifa wataijilia nuru yako, na wafalme kkjia mwanga wa kuzuka kwako.

Ezekiel 3:23, Basi, nikaondoka, nikaenda uwandani, na tazama, utukufu wa BWANA ulisimama huko, kama utukufu ule niliouona karibu na mto Kebari; nami nikaanguka kifudifudi.

Ezekieli aliuona utukufu wa Bwana:

Ezekieli 1:28, Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA.

Ezekieli 8:4, Na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwapo hapo, sawasawa na maono yale niliyoyaona katika uwanda.

Ezekieli 10:4, Utukufu wa BWANA ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa BWANA.

Ezekieli 43:2, 4,5

Ms 2, na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling,aakwa utukufu wake.

Ms.4, Na huo utukufu wa BWANA ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile lielekealo upande wa mashariki.

Ms. 5, Kisha Roho ikaniinua, ikanichukua mpaka ua wa ndani; na tazama, utukufu wa BWANA uliijaza nyumba.

Ezekieli 44:4, Kisha akanileta, kwa njia ya lango la upande wa kaskazini, mbele ya nyumba; nikaangalia, na tazama, huo utukufu wa BWANA uliijaza nyumba ya BWANA, nikaanguka kifudifudi.

Maandiko katika agano jipya kuhusu utukufu wa Mungu:

Matayo 17:1-6, Ms.1,Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.Ms.2,Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang`aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru. Ms.3, Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye. Ms.4, Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya." Ms.5, Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni." Ms.6,Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.

Katika kitabu cha Luka tunasoma kwa wafuasi waliingia katika mawingu. Lk 9:34.

Luka 2:8-9,Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao.Ms.9, Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.

Utukufu ulingáa, na wakaweza kuiona na macho yao.

Stefano ahubiria wayahudi:

Matendo ya Mitume 7:2, Naye Stefano akasema, "Ndugu zangu na akina baba, nisikilizeni! Mungu alimtokea baba yetu Abrahamu alipokuwa kule Mesopotamia kabla hajaenda kukaa kule Harani.

Stefano aliuona utukufu wa Mungu!

Matendo ya Mitume 7:55, Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akatazama juu mbinguni, akauona utukufu wa Mungu na Yesu amekaa upande wa kulia wa Mungu.

Matendo ya Mitume 9:3-4, Lakini alipokuwa njiani karibu kufika Damasko, ghafla mwanga kutoka angani ulimwangazia pande zote.Ms.4, Akaanguka chini na kusikia sauti ikimwambia: "Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa?"

Tazama jinsi Saulo alivyoielezea wakati alipoilinganisha tukio hili na  hali zingi mbili baadaye:

Matendo ya mitume 22:6, 11,…Ms. 6,.. Basi, nilipokuwa njiani karibu kufika Damasko, yapata saa sita mchana, mwangu mkubwa kutoka mbinguni ulitokea ghafla ukaniangazia pande zote. Ms. 11,.. Kutokana na ule mwanga mkali sikuweza kuona na hivyo iliwabidi wale wenzangu kuniongoza kwa kunishika mkono mpaka nikafika Damasko

Matendo ya Mitume 26:13-14, Mheshimiwa, wakati nilipokuwa njiani, saa sita mchana, niliona mwanga mkubwa kuliko wa jua ukiangaza kutoka mbinguni, ukanizunguka mimi na wale wasafiri wenzangu.Ms.14,..Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: `Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama punda anayepiga teke fimbo ya bwana wake.`

Utukufu wa bwana ni Roho wa Bwana:

Warumi 6:4, Tulipobatizwa tuliungana na kifo chake, tukazikwa pamoja naye, ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka wafu kwa kitendo kitukufu cha Baba, sisi pia tuweze kuishi maisha mapya.

“Utukufu wa baba” ni nini?.

 

Warumi 8:11, Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu anaishi ndani yenu, basi huyo aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa uzima miili yenu yenye hali ya kufa; atafanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.

Ufunuo 15:8, Hekalu likajaa moshi uliosababishwa na utukufu na nguvu ya Mungu, na hakuna mtu aliyeweza kuingia Hekaluni mpaka mwisho wa mabaa makubwa saba ya wale malaika saba.

Ufunuo 21:23, Mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuangazia, maana utukufu wa Mungu huuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo.

Tazama vile neno la Mungu linaelezea Neno la Mungu kama: wingu, mwangaza, mwanga, ng,aa, moshi na Roho wa Mungu, ijapokuwa utukufu wa Mungu kwa hakika haielezeki.

Daudi alisema kwamba mwishowe Mungu atampokea katika utukufu:

Zaburi 73:24, Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.

Tunafahamu nakala ya Petero kuhusu unabii wa Yoeli wakati wa pentekote:

Matendo ya mitume 2:17-18, `Katika siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.Ms.18, Naam, hata watumishi wangu, wanaume kwa wanawake, nitawamiminia Roho wangu, siku zile, nao watautangaza ujumbe wangu.

Lakini tazama kile aliendelea kusema:

Matendo ya mitume 2:19, Nitatenda miujiza juu angani, na ishara chini duniani; kutakuwa na damu, moto na moshi mzito;

Wengine wanatafsiri hii kama bomu zinazoanguka duniani, lakini siyo hivi bwana aongea juu yake, Anatangaza UMWAGIKAJI wa ROHO WAKE na UTUKUFU.

Damu! – Damu ya Yesu.

Moto! – Moto wa Roho mtakatifu! Ndimi za moto zikashuka na kukaa juu ya kila mmoja wao.

Yesu alipaa mawinguni, ambayo ni wingu wa utukufu.

Matendo ya mitume 1:9, Baada ya kusema hayo, wote wakiwa wanamtazama, alichukuliwa mbinguni; WINGU LIKAMFICHA wasimwone tena.

Yesu atarudi duniani akishuka kutoka wingu wa utukufu.

Matendo ya mitume 1:11,…. wakasema, "Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mliivyomwona akienda mbinguni."

Mungu mwenyewe, utukufu wake unangáa ndani ya mioyo yetu.

2 Wakorintho 4:6-7,  Mungu ambaye alisema, "Mwanga na uangaze kutoka gizani," ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu uangazao katika uso wa Kristo. Ms.7, Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo, ili ionekane wazi kwamba nguvu hiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisi wenyewe.

Mambo mengine makuu yalikuwa ya kuvutia kama nuru ya ajabu ndani ya mioyo zao.

 

21.Roho Mtakatifu na matunda ya Roho mtakatifu:

·        Wagalatia 5:22-23, matunda ya Roho mtakatifu.

·        Wagalatia 5:19-21, matendo ya mwili.

·        Tabia – aina 4, ( the 4 temperaments )

A).Wagalatia 5:22-23, Lakini matokeo ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, Ms 23,upole na kuwa na kiasi. Hakuna Sheria inayoweza kupinga mambo hayo.

Matunda ya Roho ndio hakika inayojalisha machoni pa Mungu. Matunda haya ndani ya maisha yako hujenga tabia ya kweli, inakupa kibali cha mbinguni, na kukufanya kuwa kama Kristu.

Upendo – (Upendo wa kiungu unaotiririka ndani ya mioyo yetu kupitia kwa Roho )

Furaha – ( Raha ya bwana ndiyo nguvu yetu.)

Amani – ( Amani ya Mungu siyo ya ulimwengu )

Uvumilivu

Wema

Fadhili – ( Mungu ni fadhili)

Uaminifu – ( Uaminivu kama tunda la Roho )

Upole

Kiasi – ( adabu na kiasi kwa mtu binafsi)

B).Matunda na matendo ya mwili:

Wagalatia 5:19-21, Basi, matendo ya kidunia yanajulikana: uzinzi, uasherati, ufisadi; Ms. 20, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, choyo, mabishano, mafarakano; Ms.21,husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine kama hayo.

 

Kinyume cha matunda ya Roho ni:

Upendo:    Kinyume cha upendo ni chuki, ubinafsi, majisifu. Kwa kawaida, kuna aina mbili  za nguvu au mvutu. UPENDO na KUJI-PENDA. Mungu NI upendo. Shetani ni mpinzani, Upenda wa kujipenda. Hiza ndizo nguvu zinazopingana mbinguni na hapa duniani. Mungu Yahweh ni mwenye enzi, NSHINDI, kwa sababu: Yohana 3:16, Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Furaha:         Kinyume cha furaha kama tunda la Roho ni: raha ya ulimwengu, tamaa ya ulimwengu, usherati, ulevi, madawa za kulevya nk.

Amani:          Kinyume cha amani ya Mungu ni: hofu, wasiwasi, walimwengu hawana amani, asema bwana. Isaya 48:22.

Uvumilifu:     Kinyume ni: Hasira, uasi, chuki.

Wema:          Kinyume ni: Moyo mgumu, hukumu, ubinafsi.

Fadhili:         Kinyume ni: uchoyo, mgumu( Mkono gamu),

Uaminifu:      Kinyume ni: kutoamini, uoga(hofu). Uoga ni kuamini shetani kuliko ahadi za Mungu katika bibilia.

Upole:           Kinyume ni: kiburi, ujeuri.

Kiasi:            Kinyume ni: ulafi, kukosa kiasi, kutowajibika kifedha, upungufu wa pesa wakati wote.

 

Tabia – ( The four temperaments )

a)      The phlegmatic

b)      The choleric

c)      The melancholy- ( usununo – kusononeka )

d)      The sanguine

( Samahani maneno mengine hayana utafsiri kwa kiswahili. )

Tazama pia funzo kuhusu: Temperaments na Roho Mtakatifu.

 

22. Roho Mtakatifu na ushawishi. Musiki, kuabudu katika Roho. Maandiko itokanayo kwa Roho mtakatifu:

a)Usanifu ( Inspired art )

Kutoka 31:3-5, nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya KAZI YA KILA AINA. Ms. 4, ili abuni kazi ya ustadi,kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, Ms. 5, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

Kutoka 28:3, Nawe utawambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie…….

b) Nyimbo zilizohuishwa na Roho mtakatifu:

1 Mambo ya nyakati 25:1-3, Tena Daudi na maakida wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; …Ms 3, …walioamuriwa na baba yao Yeduthuni mwenye kinubi,aliyetabiri katika kumshukuru na kumsifu BWANA.

Waefeso 5:18-19, Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu. Ms 19,Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu.

c) Ibada katika Roho:

Yohana 4:23-24, Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka. Ms 24, Mungu ni Roho, na watu wataweza tu kumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake."

D)Maandiko kupitia Roho mtakatifu:

2 Timoteo 3:16. Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili,

 

23.Roho mtakatifu na miujiza( Mysticism), ukweli na za uongo(false)

2 Wakorinto 4:6-7, Mungu ambaye alisema, "Mwanga na uangaze kutoka gizani," ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu uangazao katika uso wa Kristo.Ms 7,Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo.....

Mysticism za uongo

Matendo yote ya ajabu ajabu, mwangaza inayoangaza isiyo ya kawaida inayohusika na dini zisizo za kikristo ni za uongo (FALSE)

2 Wakorinto 11:14,.....Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa malaika wa mwanga!

24. Njia saba za uongozo wa Roho Mtakatifu:

A. Kupitia utu wa ndani (the innerman)

Utu wa ndani = mwili – nafsi – roho yako iliyookoka – Roho mtakatifu aishiye ndani

Tunatumia siku zetu za maisha katika kiwango cha mawazo yetu, hali ya kiasili, na muda mchache tu katika hali ya kiroho. Lazima tujizoeshe kukaa katika roho. Inachukua muda na pia mazoezi kusikiliza sauti ya ndani ya roho, shahidi wa ndani.

1.      Uongozo kupitia utu wa ndani, roho yako.

-Kupitia hisia ( sauti ya ROHO):

-(Intuition) –( uongozo wa dio au la, kama Urim na Tummim katika kikundi cha wakuhani wakuu.

-Uongozo wa ndani(Taa ndogo inayoangaza ndani yako)

-Ushahidi wa ndani( kuhisi vizuri na amani moyoni – ama kusumbuka, unyonge ama kuhatarika moyoni.

2.      Uongozo kupitia maono na pia ndoto kutokana na Roho Mtakatifu.

3.      Uongozo kupitia unabii.

4.      Uongozo kupitia sauti ya kiungu.

 

Pointi hizo tatu za mwisho zote ni kwa vipawa vya Roho Mtakatifu.

5.      Uongozo kupitia neno la Mungu, ikiangazwa na Roho Mtakatifu.

6.      Uongozo kupitia hali ya maisha. ( Yona katika dhoruba )

7.      Uongozo kupitia matendo ya unabii, (Agabus mnabii, Ezekieli mnabii)

Matayo 18:16, ....Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.

Dhibitisho la hakika ni kwa uongozo, wakati inakuja mara mbili ama tatu kuhusu jambo fulani.

Tena, kwa kawaida kuna muongozo kupitia hekima ya kiasili, hisia za kawaida. Inadhihirisha waziwazi nini la kufanya katika tukio fulani.

Usidhubutu kutafuta ushauri kupitia yafuatayo:

·        Kwenye miroho ndani ya glass.

·        Uenyemali (fortune telling)

·        Bilauri(crystal ball)

·        Horoscopes

·        Usoaji wa kadi

·        Mizani(pendulums)

·        Mwaaguzi(water diviner)

·        (Seances)

·        (Occult practice)

·        Ushirikina(superstition)

Yote haya ni mashauri kupitia roho mchafu ambalo kwa hakika litakupotosha.

Wapsykologia na mapsychiatrists hawawezi kutoa ushauri wa kiroho kwa sababu hawana imani kwamba  roho mtokatikatifu yuaishi ndani ya mtu wala hawaamini kwamba roho ya mauofu iko.

Ndoto zina huishwa kwa njia tatu;

1)      Kupitia kwa roho mtakatifu

2)      Kupitia kwa roho mchafu wa ibilisi

3)      Kupitia tukio la siku kwa siku, mara nyingi huja kwa njia tofauti zizizo eleweka.

Utabiri wa ndoto wa kweli hufanyika kupitia uweza wa roho mtakatifu. Ni halali kutumia akili za werevu ama ujuzi wa mwanadamu ni limuko na mwishowe mtu anaweze kuwa na roho ya uongo.

 Danieli alitabiri ndoto kwa sababu roho mtakatifu alikuwa NDANI  yake. Danieli 4:8-9.

Usiwaendee wasiomcha Mungu kwa mashauri kuhusu mambo ya kiroho wala ushauri kuhusu maisha yako na siku zako za usoni.

 

25. Roho Mtakatifu na huisho wa neno la Mungu.

2 Tim 3:16, Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, ( naye ni roho mtakatifu)….

Bibilia, ambayo ni neno la Mungu kupiti uweza wa roho mtakatifu, haibadiliki, kamilifu na ina dumu milele. Yesu ndiye nembo(muhuri) ya neno la Mungu.Yehovah Yahweh „ MIMI NDIYE“  mwenye enzi na ni wa milele.

 

26.Roho mtakatifu na Yesu Kristu kama mzaliwa wa pekee wa Mungu baba.

Mathayo 12:40,Jinsi Yona alivyokaa siku tatu kutwa kucha tumboni mwa nyangumi, ndivyo naye Mwana wa Mtu atakavyokaa ndani ya ardhi siku tatu kutwa kucha. (Hades-ufalme wa giza)

Jukumu ya roho mtakatifu kati ya msalaba na kiti cha enzi:

Yesu alipokelewa katika wafu  na Roho mtakatifu, kafufuka,akapaa juu enzini mwa mungu na akatukuka.

1 Petero 3:18:19,  Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke ninyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;Ms.19,na kwa maisha yake ya kiroho alikwenda kuwahubiria wale roho waliokuwa kifungoni.(kaburini)

Katika nguvu za roho mtakatifu, Yesu alihuishwa baada ya kubeba dhambi ya wengi. Isayah 53:10-12

Katika nguvu za roho mtakatifuYesu alihubiri ujumbe wa wokovu kwa wote walioishi duniani na tokea mwanzo hadi wakati wa kifo chake kwa miaka 4000, hakika ndio mkutano wa ufifio mkubwa katika historia.

Warumi 8:29, …Maana hao aliowachagua tangu mwanzo, ndio aliowateua wapate kufanana na Mwanae, ili Mwana awe wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.

Soma pia Zekariah 12:10.

Tazama pia somo kuhusu. Atonement.

 

27. Roho mtakatifu na manabii wa agano jibya:

Wanabii wote wa Agano jibya walifanya kazi katika uwezo na imizo ya roho mtakatifu.

Hannah pekee alitabiri kupitia roho ya uongo.Jeremiah 28:10,12,15.

 

28. Roho mtakatifu na hekalu.

Kinara cha mshumaa chenye sehemu saba katika hekula ni ishara ya roho mtakatifu na dhihisho zake.

 

29. Roho mtakatifu na ubatizo wa wa Roho mtakatifu na moto.

Luka 3:16,…..Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Matendo ya mitume 2:3-4, Kisha, vikatokea vitu vilivyoonekana kama ndimi za moto, vikagawanyika na kutua juu ya kila mmoja wao.,Ms 4, Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema lugha mbalimbali kadiri Roho alivyowawezesha.

Waebrania 1:7 (Zaburi 104:4)…. na watumishi wake kuwa ndimi za moto."

Yaonekana kwamba sehemu ya pili, za moto, wa uatizo katika roho na moto, mara nyingi huachwa nje.

 

30. Roho mtakatifu na kuhubiri injili.

a) Injili yahubiriwa kupitia Roho mtakatifu.1 Petero 1:12, …ambayo ninyi mmekwisha sikia sasa kutoka kwa wale wajumbe waliowatangazieni Habari Njema KWA nguvu ya ROHO MTAKATIFU aliyetumwa kutoka mbinguni, hiyo kazi yao haikuwa kwa faida yao wenyewe, bali kwa ajili yenu. Hayo ndiyo mambo ambayo hata malaika wangependa kuyafahamu.

b) Roho mtakatifu huubiri.Yohana 16:13-14,Lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atawaambieni yote atakayosikia, na atasema mambo yatakayokuwa yanakuja.Ms.14, Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu.

31. Roho Mtakatifu na Mwanzo.

Mwanzo 1:2,….na Roho wa Mungu Yahweh ikatembea kwenye maji.

Mwanzo 1:26,kisha Mungu akasema,” NASI tumuumbe mwanadamu kwa sura YETU wenye…..

NASI na YETU  ni utatu wa Mungu baba.

Mungu baba, Mwana na Roho Mtakatifu walikuwa na walihusuka katika umbaji wa ulimwengu.

 

32.Roho Mtakatifu na silaha kamili, zilaha za kuangamiza na zilaha za

 Silaha kamilifu ya Mungu. Waefeso 6:11-18, Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi.Ms,12. Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza.ms.13, Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti.Ms.14, Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani,Ms.15, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.Ms.16, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu.Ms.17, Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu.Ms.18, Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.

 

33. Roho Mtakatifu haweza kuzimwa(kukasirishwa).

1 Thesalonike 5:19, Msimpinge Roho Mtakatifu;

 

34. Roho Mtakatifu na nguvu za kiungu.

Samsoni. Waamuzi 14:5-6,….Simba akamghurumia, Ms.6, na Roho wa Mungu hukashuka kwa nguvu juu yake, akamrarua zimba simba kama vile angerarua mtoto na hakuwa na chochote mkononi…..

 

35.Roho Mtakatifu na kuzaliwa mara ya pili. (wokovu).

Yohana 3:5-6,…. Yesu akamjibu, "Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.Ms.6, Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho.

Wokovu sio kwa kubatizwa kwa maji bali ni kwa kuzaliwa mara ya pili kwa roho.

 

36. Roho Mtakatifu na r oho ya mwanadamu.

Warumi 8:16, Naye Roho mwenyewe anajiunga na ROHO ZETU na kuthibitisha kwamba sisi ni watoto wa Mungu.

Kuna tofauti kati ya Roho Mtakatifu na Roho ya mwanadamu.

 

37.Roho Mtakatifu na umoja wa kweli.

Yohana 17:22, Mimi nimewapa utukufu uleule ulionipa mimi, ili wawe kitu kimoja kama nasi  tulivyo mmoja;

Umoja kanisani, umoja katika ya waumini, haipatikani kwa nguvu za mwanadamu, wala katika vyama na mtandao, haiwezi kuonekana katika hakili za mwanadamu lakini umoja wa kweli unatokana na Roho Mtakatifu katika mioyo ya waumini.

 

38.Roho Mtakatifu na Roho ya maombi.

Zakariah 12:10.Na nitamwaga juu ya nyumba ya Daudi, na wakaaji wa Yerusalemu, ROHO YA NEEMA NA MAOMBEZI; na watanitazamia mimi, ambaye walinichoma na watahuzunika.

Kumetolewa Kiwango specieli cha Roho ya neema na uombezi utakaomwa juu ya kanisa. Unabii inahusu wakati Yesu Kristo alisulubishwa na kuchomwa pavuni.

Yesu kristu, mwana wa pekee akafanyika mzaliwa wa kwanza kwa wandugu wote. Tazama pia 8:29.

Tazama pia mazama: Maombi ya muumini.

 

39.Roho Mtakatifu na kuabudu.

Yohana 4:23 Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya ROHO; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka.

Ibada ya kweli katika Roho Mtakatifu ni njia ya kweli ya kuonyesha upendo na utukufu kwa Mungu baba na mwana.Wakati umati wanaimba katika Roho, huimbaji wa zaburi hizo kwa Mungu, katika hivyo anamwabudu Mungu katika umoja. Tazama pia 1 Korinto 14:15. Nifanye nini, basi? Nitasali kwa roho yangu, nitasali pia kwa akili yangu; nitaimba kwa roho yangu, nitaimba pia kwa akili yangu.

Hakuna kusudi lingine katika ulimwengu na bingu ila kuabudu katika Roho.

Tazama pia somo kuhusu: Kuabudu.

 

                 Vagn Rasmussen Ministries.

            Anwani:rasmussenvagn@hotmail.com