Sheria za Mungu za rohoni na mafanikio

 

 

 

 

 update aug.2006

 

 

Original text: God's spiritual laws and prosperity

 By Vagn Rasmussen,    Translation by Lawrence Chepkwony                                           

                                                                                               

 

                                            

 

Sheria za Mungu za rohoni na mafanikio

 

Yaliyomo                             

 

Utangulizi

 

1. Je, mkristo anapaswa kufanikiwa?

 

2. Yesu Krsito- Je, maskini au tajiri?

 

3. Maagizo ya Mungu ya mafanikio.

 

4. Njia ya mungu ama njia ya ulimwengu?

 

5. Mungu anataka tupadilishe nia yetu kwa pesa!

 

6. Tunawezaje kupadilisha na kuweka upya mawazo yetu?

 

7. Tazamo la mungu kwa kazi na nidhamu.

 

8. Tunafuna tunachopanda.

 

9. Baraka kwa kulipa fungu la kumi.

 

10. Hatuwezi tukapeana mpaka ikawa mingi mbele za Mungu.

 

11. Kutoa kwa njia ya kiungu.

 

12. Sheria za Mungu juu ya kupokea.

 

13. Sheria za Mungu ya kuweka hazina na rasilimali.

 

14. Kutumia sheria za Mungu ya mafanikio.

 

15. Chanzo cha umaskini, umaskini na mataifa yasiyoendelea, kila maskini.

 

16. Yale bibilia inasema kuhusu pesa.

 

17. Pesa huathiri tabia na ubinafsi.

 

18. Maandiko juu ya pesa.

 

19. Hatua muhimu katika barabara ya umaskini kuingia kwa utele.

 

Utangulizi

Yote yanaanza ndani ya moyo na akili. Mawazo yako juu ya pesa lazima yabadilike kwanza. Tamaa ya kibinafsi juu ya pesa ambayo unatumia kwa manufaa yako pekee yako itabadilishwa kuwa kupeana na furaha kwa watu wengine-kupeana kwa familia, kwa maskini, kwa kueneza neno kwa njia yeyote ile, fungu la kumi na kupeana kwa nyumba ya Mungu kwa furaha.

 

Tumia pesa kwa mapendeleo ya Mungu. Wacha Roho Mtakatifu akuongoze lini na wapi utumie pesa zako. Usiweka hazina katika mambo yanayoisha bali weka katika mambo ya milele.

 

Epuka kununua vitu visivyofaa.

 

Usitumie pesa kwa kujinufaisha wewe peke yako bali kwa mahitaji.

 

Tumia pesa kidogo kuliko unachopokea kwa mshahara wako.

 

Epuka deni.

 

Ufanisi inahusu sehemu nyingi ya maisha, kifedha, kiroho, kimwili, kiakili, kihisia.

 

1. Je, wakristo wanapaswa kufanikiwa?

 

Mungu aliumba mali yote ya ulimwengu. je, aliwaumbia wasioamini, kwa walio na mioyo migumu, watenda dhambi wa kike na wa kiume wanaomlaani yeye, kumkataa na kupinga sheria zake? je, anataka kweli  wafanikiwe na watoto wake wakae bila?  la sivyo. Mungu baba yetu anataka kilichobora kwa wana wake, waumini walozaliwa mara ya bili, wakristo.

 

Kama baba yetu wa mbinguni alitupatia mwana wake wa pekee. Tayari ametupatia  iliyo bora kabisa na sasa ako tayari kutupatia hiyo yote nyingine. Warumi.8:32 Yeye asiymwachilia mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamojanaye?

 

2. Yesu kristo -maskini au tajiri?

 

Yesu alikuwa maskini?

 

Hapana!-kwa yeye na kwake vitu vyote vikaumbwa. wakolosai.1:16... vitu vyote vimeumbwa naye kwa ajili yake.

 

Anamiliki dunia yote na angali anamiliki

 

2.Wakorintho.8.9. hata ingawa alikuwa tajiri, hata akafanywa maskini ili kupitia kwa     umaskini wake tukafanywa kuwa tajiri.

 

3.   Maelezo ya Mungu kuhusu pesa.

 

  Wengi wetu tumepokea Yesu kama mwokozi lakini hatujakubali awe Bwana wa kila sehemu ya maisha yetu.

 

Baba yetu anataka tusalimishe maisha yetu yote kwake. hataki tuweke familia, pesa raha zetu au                                                                                                                           kitu chochote zaidi yake. Kutoka 20:3. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

 

Sheria ya mungu ya kufanikiwa itatenda kazi kulingana na jinsi tumemweka wa kwanza katika                              masha yetu

 

Mungu hataki tuangamizwe na tamaa mbaya. ndio sababu anaamrisha apewe nafasi ya                       kwanza. Kila wakati umweke Mungu wa kwanza. Mathayo 6:33 Tafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtasidishiwa.

 

4.Njia ya Mungu-au njia ya ulimwengu?

 

Njia ya ulimwengu- au njia ya Mungu?

 

Mungu anataka tutubu na kuweka upya mawazo yetu iweze kufikiri njia za Mungu juu ya mafanikio.                                       

 

Wakristo wanaotaka ufanisi kwa njia ya ulimwengu, mwishowe watamalizia katika ''theologia ya mafanikio.''

 

Wakristo wanaotaka mafanikio kwa njia ya kimungu wataheshimu Mungu kwa mali zao.

 

Ni muhimu sana tuelewe wazo hili, ya kwamba fedha, na dhahabu katika ulimwengu huu ni ya                            Mungu, na sisi hatuna chochote chetu, Mungu ameturuhusu tuzitumie.

 

Hagai. 2:8 fedha ni yangu na dhahabu ni yngu asema bwana wa majeshi

 

Usiseme: mali yangu ni yangu, nizipata mwenyewe.”kwa sababu mungu anasema katika kumbu la torati.8:17-18 na unasema katika moyo wako: nguvu yangu na na uwezo wa mikono yangu imenipatia hii mali. v18: lakini utamkumbuka baba mungu wako, kwa sababu ni yeye akupaye nguvu ya kutafuta mali. ili atimize ahadi yake kwa mababu wanu.

 

Njia ya ulimwengu ya kupata utajiri ni kwa kutegemea nguvu zangu mwenyewe. njia ya mungu ni kumtumainia.

 

Marko.10:24 vile ilvyongumu kwa wanao amini kwa mali zao kuingia katika.

 

Neno la muhimu hapa ni uamini katika mali”badala ya kuamini katika bwana. yule kijana tajiri alipenda (amini) sana pesa zake kuliko kumpenda(amini) mungu.

 

Sheria ya mungu kuhusu mafanikio inatuhitaji tumtumainie yeye badala ya kumtumainia utajiri.

 

Nji za mungu ziko kinyume na njia za kiduni. badala ya kuamini katika mali ya kidunia baba yetu anatsks tumwamini  yeye na ktumia kile tunacho na watu wengine.

 

Timotheo. 6:17-18 wahukumu wale walio na mali katika dunia, wasijiwazie kuwa juu na wala wasiamini katika mali isiyoeleweka, lakini kumwamini mungu aiishiye na kupeana kila kitu kwa wingi ili mpate kuzifurahia ili zitende mema na pia watende kazi nzuri tayari kupeana....

 

Muhubiri 5:13 kuna roho chafu mbaya nimeona chini ya jua, kwa majina mali inayowekwa na wenyewe ili kuwadhuru wenyewe.

 

Kusanya pesa ni mbaya na mwishowe itatudhuru

 

Pia kuiba ni mbaya, kuiba chakula, mafuta, pesa na kadhalika. hii inaonyesha uoga wetu na ya kwmba hatmwani mungu.

 

Sheria ya mungu ya kufanikiwa itatunyesha wazi jinsi ya kufaidika wakati wa shida ya kiuchumi.

 

Isaya 48:17 mimi ni mungu baba yenu nikufundishaye kufaidika....

 

Sasa ni wakati wa kuacha njia zakitambo za kuamini katika mabenki, akiba za kufaidika, mashamba, pesa za uzeeni, mipango za kufaidika, akiba za wakati wa shida, na kadhalika. na aanza kufanya hivyo kwa njia ya kimungu na kufwata maagizo zake za kufwata ili uendele.

 

Utajiri unaopatikana kwa njia ya kiulimwengu haitoshelezi zaidi zaidi tunavyopata ndio zaidi tunahitaji.

 

Muhubiri 5:10 yule apendaye dheluji hawezi akatosheka na dheluji, pia yule apendaye kwa wingi na kuongezeka, hii yote haina maana.

 

Mungu anataka tupadilishe nia yetu juu ya pesa na kuweka upya mawazo yetu.

 

Mungu anataka tuwaze katika njia zake kwa mambo yanayo husu pesa.

 

Tunawezaje kubadilisha na kuweka upya mawazo yetu

 

Sheria ya Mungu ya upya: soma bibilia, fikiri na kuomba, kuwa na imani, kutubu dhambi na kufuata maagizo ya Roho Mtakatifu na neno la Mungu.

 

Mtazamo wa Mungu kwa kazi na nidhamu.

 

Mungu anataka tufanye kazi na kutenda vizuri.

 

Mojawapo ya matunda ya roho mtakatifu ni nidhanu. mtu lazima ajifunze kuwa na nidhamu katika kutumia pesa. si lazimatuishi kaika maisha ya kuharibu ati kwa sababu sisi ni wakristo na tuko na baba tajiri kabisa.

 

Tunavuna tunachopanda.

 

Ufanisi kuhusiana na kupanda na kuvuna- mbegu ya kawaida-upenda-imani-pesa-wema.

 

Urafiki-elimu-hekima. sheria ya kupanda nakuvuna inafanya kazi katika kila sehemu ya maisha yetu.

 

Panda mbegu yako nzuri ya pesa kwa udongo nzuri, ndiyo katika kazi ya umishnari kwa walio maskini.

 

Wagalatia 6:7.... chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna.

 

Mshangao, watu wanatarajia kuvuna pes mingi bila hata kupanda mbegu kidogo. wanafikiria maombi inatosha, lakini hii ni kuvunja sheria ya Mungu. ukitaka kuvuna pesa ni lazima upande pesa, sio maombi katika hali hii. ukitaka kuvuna pesa nyingi ni lazima upande pesanyingi, sio kuomba sana pesa. tunastahili kuombea sana waliopotea kiroho na wanaohitaji. hii ni njia rahisi sana ya kutengeneza pesa, peana pesa na furaha, vile Roho Mtakatifu inakuongoza. tafuta mwelekeo wake na utvuna mbegu yako ya pesa mahali pafaayo na wakati ufaayo, na kiwango kifaacho.

 

Kumbuka pia kupanda: upndo-uzuri-pia neno la Mungu-mbegu zote nzuri.

 

Panda mbegu yako ya pesa kwa umishonari, katika kanisa, kwamaskini, kwa famili yako na kadhalika.

 

Baraka ya kutoa fungu la kumi.

 

Hakuna amri wazi katika agano. jipya juu ya fungu la kumi.

 

Mungu anakubali tumjaribu anaahidi baraka tele tukifanya hivyo.

 

Malaki 3:10 leteni zaka ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha.

 

Mungu anatujaribu tumhakikishe. hapo ndio mahali papekee katika bibilia ampabo anatujaribu tumhakikishe.

 

Tunamheshimu Mungu kwa kutoa asilia kumi ya mapato yetu.

 

Ni vigumu Mungu kubariki watoto wake ikiwa tutamwibia fungu la kumi bibilia intuambia sehemu kumi ni yake.

 

Unachopeana kama zawadi kwa ajili ya kusudi spesheli sio fungu la kumi lakini hupeana kando na fungu la kumi.

 

Nyumbani mwangu inaamrisha kuleta fungu lako la kumi katika kanisa lako la nyumbani.

 

Ushuhuda.: wakati ule nilikuwanina hubiri katika kanisa, rafiki wangu mwema  alikuja na agizo la pesa,35,000dkr. hii pesa nyingi ambayo alitaka kupatia kanisa kama mbegu la kupanda. saa hiyo alikuwa hakika katika shida ya kifedha. mwagizaji wake alikuwa amemuhatarisha asifanye hivyo. kama mtu asiyeokoka alidhania pesa hiyo itapotea, na hakuamini katika kutoa  kupanda mbegu ya kiroho na kuvuna biashara. bibila inasema: ünavuna unavyopanda

 

Hatuwezi tukapeana Mungu zaidi

 

Matendo ya mitume10:14....na yeye (malaika) akamwambia(cornelio)¨maombi yako na sadaka amemkujia Bwana kama ukumbusho.

 

Marko 9:41 kwa hiyo yeyote atakayekupa hata maji ya kunywa kwajina langu, kwa sababu wewe ni mali ya kristo, ama kweli nawambieni, hatapoteza kamwe zawadi yake.

 

Kutoa- njia ya kiungu.

 

Peana nawe utapewa, kipimokizuri, imefinywa na kutingishwa pamoja, na kupitishwa juu, watu watakupatia kwa maendeleo yako. kwa sababu kipimo ukitumiacho ndio itatumiwa kukupimia. luka 6:38

 

Sheria ya Mungu juu ya kupokea.

 

Mungu hupeana kwa njia ambayo haitadhuru nafsi zetu.

 

James 4:3    hata mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya ili mvitumie kwa tamaa zenu.

 

sheria za Mungu juu ya kuweka hazina na rasilimali.

 

Matayo. 6:20 Bali jiweekeni hazina binguni,, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wavi hawavunji wala hawaibi.

 

Mithali19:17. amhurumia maskini humkopesha bwana: naye atamlipa kwa tendo lake jema.

 

Kutumia sheria za Mungu juu ya mafanikio

 

Tafuta maandiko katika biblia juu ya mafanikio- tendo la imani.

 

Sababu ya umaskini, kutokuendelea na taifa maskini, na watu maskini.

 

Elimu ya upotovu

 

Nyumba zilizochafuliwa

 

Kuabudu miungu aina zote kati utamaduni ya mashariki- utamaduni ya kaskazini

 

Kuunguzwa na pepo ya tamaa, ulevi, madawa  ya kulevya.

 

Uzembe.

 

Kuongezeka kwa  asilimia  ya wakristo wanaotoa ushuhuda ndivyo mali inavyoongezeka na pia utaratibu katika nchi hiyo.  kuongezeka kwa dini na kuabudu miungu ndivyo umaskini na kutokuwa na utaratibu na ufisadi katika nchi hiyo.

 

Tumaini kwa ajili ya pesa zako.

 

Uwe na tumaini kwa sheria za Mungu juu ya kupanda na kufuna

 

Bibilia husema nini kuhusu pesa.

 

Pesa- na mafunzo ya kikristo, je, wakristo wanastahili kuendelea? soma 2.wakoritntho8:9

 

Pesa- na kufunga na kuomba na kutoa misaada.(matendo ya mitume 10:4,30) kornelio

 

Pesa- na imani 2.wakorintho9:10 mbegu ya kupana iongezeke maradufu.

 

Pesa- na ukweli, luka 16:10-13 hasa v 12

 

Pesa- na nidhamu mithali 6:9-10

 

Pesa- na wakati muhubiri11:4 na 6

 

Pesa- na kupanda na kuvuna wagalatia 6:7, wakorintho wa pili 9:6

 

Pesa- na mtindo wa ulimwengu kulinganishwa na mtindo wa mbinguni. luka 6:38, mathayo 6:19-20

 

Pesa- na rasilimali ya benki ya dunia luka 12:21

 

Pesa na rasilimali katika benki ya dunia mathayo 6:19-20 na mathayo 19:21

 

Pesa- na faida. mithali 28:8,kutoka 22:25 na kumbukumbu la torati 23:19 (dhambi ya kuchukua faida nyingi)

 

Pesa- na kupeana ulinzi, hakikisho, ya kufunguliwa. mithali 22:26 na 11:15 na 20:16

 

Pesa- na fungu la kumi malaki 3:10, luka 11:42, mithali 3:9

 

Pesa- na sadaka matendo ya mitume 10:4.

 

Pesa- na kupeanamithali 28:27, wafilipi 4:17-19, luka 6:38.

 

Pesa- na kumwibia Mungu malaki 3:10

 

Pesa- na watoto wakorintho zaburi 37:25

Pesa na ulafi zaburi 127:2

 

Pesa- na kuiba Yohana 12:6 na 1wakorintho 6:10

 

Pesa- na karata mithali16:33

 

Pesa- na mwenye haki mithali 15:6

 

Pesa- na ukweli mithali 21:6

 

Pesa- na nia nzuri luka 6:35 na luka 6:38 pana na wewe utapewa

 

Pesa- na hasara ya milele( Judas) mathayo 27:3-5 na Yohana 17:12

 

Pesa- dhambi kinyume na Roho Mtakatifu matendo ya mitume 5:1-5

 

Pesa- na waanzilishi (Abrahamu, Yakobo, Ayubu, Daudi na Suleimani)

 

Pesa- na kubadilika kwa uchumi Mathayo 6:19-21

 

Pesa- na kazi Mithali 28:19

 

Pesa- na uzembe Mithali 6:6,9 Mithali24:33-34

 

Pesa- na kulala sana asubuhi Mithali 6:10, MIthali 24:33-34

 

Pesa- na deni Mithali 22:7

 

Pesa- na kupenda sana pesa 1 thimoteo 6:10 na waebrania 13:5

 

pesa- na utajiri uliofichwa  Isaya 45:3

 

Pesa- na kuirithi. Mithali 13:22, 19:14, 14:18.

 

Pesa- na mataifa wanaojiita maskini na matajiri. Ibada ya miungu licha ya asilimia kubwa ya wakristo katika taifa. Kumbukumbu la torati 31:16

 

Pesa- na yesu alifanywa maskini ili sisi tuwe matajiri. anamiliki ulimwengu mzima- aliziumba pesa zote. wakolosai 1:16

 

Pesa- na Mungu Yahweh. Hagai 2:8 fedha ni yangu na dhahabu ni yangu...

 

Pesa- na kusanya kidogo kidogo Mithali 13:11

 

Pesa- na maafisaa (kodi) Mathayo 22:21, Mariko 12:17, Luka 20:25, Warumi 13:7

 

Pesa- na kuchochea; kutia moyo. Proverbs 4:4

 

Pesa- na wivu (kutajirika haraka haraka) Mithali13:11, Mithali 28:22

 

Pesa na baraka za Mungu. Mithali 10:22

 

Pesa- na laana za kifamilia.Kutoka 20:5

 

Pesa- na ahadi zilizovunjwa. Zaburi 15:4. (Anayeapa kwa moyo wake na abadiliki)

 

Pesa- na mambo ya kwanza. Luka 12:31 tafuteni kwanza ufalme wa Mungu

 

Pesa na tabia yako. (tabia nzuri inayozalisha inaweza kupokea baraka za mali bila kuadhiri nafsi)

 

Pesa- na kuridhika (utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa) 1,thimoteo 6:6.

 

Pesa- na kanisa mwanzo 18: 26 fungo la kumi.

 

Pesa- na wahudumu 1. timateo 3:3 na tito 1:7

 

Pesa na mpangilio

 

Pesa- na ndoa mithali 31:10.

 

Pesa na kunywa na kulala zaidi mithali 23:20 walevi ............

 

Pesa- na hakikisho mithali 6:1, 11:15, 17:18, 20:16, 27: 13.

 

Pesa- na adui wako mithali 25: 21

 

Pesa na kazi mithali 18: 9, 1.timateo 5;18, mithali 14:23, zaburi 127:2.

 

Pesa na jinsi ya kuomba Mungu yahweh mithali 19:17.

Pesa na kupokea neno la mungu mathayo 13:23

 

Pesa na mambo ya kwanza Muhubiri 11:4, na mithali 24:27

 

Pesa- na mali chini ya laana na chini ya lahana na chini ya baraka.kutoka 28.

 

Pesa- na viongozi wa kanisa; kuweka pesa za kanisa, na pesa za kibinafsi kuganywa vizuri.yahana 12:6 ............ yuda mweka hazina alikuwa mwizi.

 

Pesa- na kuanguka kwake shetani Ezekiel 28:4-5.

 

Pesa- kupenda pesa 1Thimoty 6:10. ......ni chanzo cha maovu yote...

 

 

Pesa- visababisho kwa  tabia  na ubinafsi utu.

 

Mkarimu.

 

Atoaye kwa furaha.

 

Mgumu kwa kupeana.

 

Mchoyo

 

 Anayejua kutumia pesa vizuri

 

Mpole na asiyeitisha kwa nguvu.

 

Mcheza kamari

 

Mpotevu na mharibivu.

 

Mwaribivu.

 

Mwingiliaji

 

Mwizi

 

Tamaa ya mwili

 

 Muuzaji

 

Mweka hazina

 

Mkweli

 

Mpangilio katika mambo yanayohusu pesa.

 

Mwerevu kwa mambo yanayohusu pesa.

 

Mpumbavu, kwa mambo ya fedha, asiyejifunzi kwa kukosea.

 

Anayetamani nguvu

 

Mpenda nguvu

 

Kuweka hazina

 

Kuweka kwa lazima

 

Akusanyaye vitu

 

Aliye na nidhamu kwa mambo yanayohusu pesa.

 

Wewe ni wa aina gani? Uwe mwaminifu kwako mwenyewe. unataka mabadiliko? Jambo nzuri kuihusu: ni kwamba kuna uwezekano wa mabadiliko.  hatua zinazofaa kuchukua ni : kutubu, kuamua mabadiliko na kuifanyia kazi. Maendeleo ama kukuwa nayo, yote inategemea nia. uamuzi wa mwanadamu ni muhimu.

 

Maandiko juu ya fedha

 

Kanuni za biashara katika biblia

 

Jinsi Mkristo anapaswa kuvitumia pesa.

 

Mithali 22:7 -Tajiri humtawala maskini, naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.

 

Mithali 23:4 -Usijitaabishe ili kupata utajiri;  acha kuzitegemea hekima akili mwenyewe.

 

Mithali 23:21 -kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, na utepetevu humvika  mtu nguo tambara.

 

Mithali 24:27 -Tengeneza kazi yako bila ( nje), na ufanye ikufaye shambani, ukiisha, na badaye ujenge nyumba yako.

 

Mithali 24:30-31 -Nalipita karibu na shamba la mvivu, na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. v31 kumbe ! lote pia limemea miiba: uso wake ulifunikwa kwa viwawi; na ukuta wake wa mawe umebomoka.

 

Mithali 24:33-34 -Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono  upate usingizi!  hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

 

Mithali 27:23-24 -Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; na kuwaangalia sana ng'ombe zako. v24 kwa maana mali haziwi za milele; na taji je! yadumu tangu kizazi hata kizazi?

 

Mithali 28:8 -Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida; humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

 

Mithali 28:19 -Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele; bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.

 

Mithali 28 : 22 - Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri ;Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia.

 

Mithali 28:27 -Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu ;Bali afichaye macho yake atakuwa na laana             nyingi.

 

Mithali 30: 8-Uniondolee ubatili na uongo;Usinipe umaskini wala utajiri;Usinilishe chakula kilicho kadiri          yangu.

 

Mithali 31:10-Mke mwema ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha majirani.

 

Mhubiri 4:4 -Tena nikafikiri amali zote,na kila kazi ya ustadi ,ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake .Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.

 

Mhubiri 11:4-Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.

 

Mhubiri 11:6-Asubuhi panda mbegu zako,Wala jioni usiuzuie mkono wako.

            Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa ,kama ni hii au ni hii .au kama zote zinafaa        sawasawa

 

Mithali 11:24 Kuna atawanyaye ,lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea     uhitaji.

 

Malaki 3:10  Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu,mkanijaribu kwa njia           hiyo ,asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni ,na kuwamwagieni baraka , hata isiwepo nafasi ya kutosha ,au la

 

Warumi 13:7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahihiye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.

 

Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa ;kipimo cha kujaa na kushindiliwa ,na kusukwa-sukwa hata kumwagika ,ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

 

Luka 6: 35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.

 

Mathayo 6:33-Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

 

Wakorintho wa pili 9:6 Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba ;Apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.

 

Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakacho vuna.

 

Mithali 3: 9 -10 Mheshimu Bwana kwa mali yako.Na kwa malimbuko ya mazao yako yote .Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi,Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

 

Mithali 6:6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima.

 

Mithali 6:9 Ewe mvivu utalala mpaka lini? Utaondoka lini katika usingizi wako?

 

Mithali 8:18 Utajiri na heshima ziko kwangu,Naam, utajiri udumuo ,na haki pia.

 

Mithali 10:22 Baraka ya Bwana hutajirisha Wala hachanganyi uzuni nayo.

 

Mithali 13: 11 Mali inayopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.

 

Mithali 14:23 Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo tu huleta hasara tu.

 

Mithali 15:6 Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mabato ya mtu mbaya huwa taabu tu.

 

Mithali 16:33 Kura kutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hakumu zake zote ni za Bwana.

 

Mithali 17:18  Aliyepungukiwa na ukali hupana mkono wa mtu ;Na kuawa mdhamini mbele ya mwenzake.

 

Mthali 18: 9 Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu.

 

Mithali 19: 17 Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA Naye atamlipa kwa tendo lake njema.

 

Mithali 20: 16 Twaa  nguo yake amudhaminiye mgeni; Mtoze rehema aliye mdhamini wa mgeni.

 

Mithali 21: 6 Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongo Ni moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.

 

Mithali 3:27 Usiwanyime  watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.

 

Waebrania 13:5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo ; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungia kabisa ,wala sitakuacha kabisa.

 

1Timotheo 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha ; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

 

2Wakirintho 9:7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, wala si kwa lazima ;maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

 

Mithali 25: 21 Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula;Tena akiwa ana kiu ,mpe maji ya kunywa.

 

Mathayo 6:24 Hakuna mtu  awezaye  kutumikia mambwana wawili;kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharahu huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

 

 Zaburi 127:2 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko ,Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa,Bwana amewatendea mambo makuu.

 

Mwanzo 3: 19 Kwa jasho la uso wako utakula chakula,hata utakapoirudia ardhi,ambayo katika hiyo ulitaliwa ;kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

 

Timotheo wa kwanza .....kwa maana mfanyi kazi anastahili ujira wake.

 

Matendo ya mitume 10:4 Kornelio .... sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.

 

Timotheo wa kwanza 6:6 Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa .

 

Kugharamia deni

 

Mithali 27:13 Twaa nguo yake amdhaminiye mgeni;Mtoza rehani aliye mdhamini wa malaya.

 

Mithali 6:1 -2 Mwanangu,kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako,Ikiwa wewe na mgeni mmepana mikono,Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako,Umekamatwa kaw maneno ya kinywa chako.

 

Mithali 11:15 Amudhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama.

 

Mithali 17:18 Aliyepungukiwa na akili hupana mkono wa mtu; Na kuwa mdhamini mbele ya mwenzake.

 

Jiwekeni katika umilele.

 

Mathayo 6:19-20 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo,na wevi huvunja na kuiba;    bali jivukeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi.

 

 Marko 10:29:30 Yesu akasema, Amin, nawaambiyeni, Hakuna mtu aliye acha nyumba, au ndugu waume ,au ndugu wake, ua mama ,au baba, au watoto, au mashamba kwa ajili yangu, na kwa ajili ya injili ila atapewamara mia sasa wakati huu, nyumba,na ndugu waume,na nduguwake,na mama, na watoto,na mashamba,pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.

 

Luka 14:33 Basi, kadhlika kila mmoja wenu asiye acha vyote alivyo navyo,hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

 

Kutoa fungu la kumi katika bibilia.

 

Mathayo 23:23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari najira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yani adili na rehema, na imani; hayo inawapasa kuyafanya wala yale mengine msiyaache.

 

Malaki 3: 10 Leteni zaka kamili ghalani,ili kiwemo chakula katika nyumba yangu,mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi ;mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni , na kuawmwagieni baraka, hata isiweponafasi ya kutosha ,au la.

 

Wabrania 7:2 Ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi na vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki ,tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;

 

Hesabu 18:26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli, niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.

 

 

Nehemiah 10 ..... Walawi, watwaapo zaka Walawi .nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, katika nyumba ya hazina.

 

 Fungu la kumi ya Walawi. Fungu la kumi la Haruni.

 

Kabila ya walawi walichaguliwa na Mungu wahudumu katika hekalu . Walikuwa makuhani .

Swali: Je huduma yako ya kanisa hutoa fungu la kumi?

 

Jibu liko katika Hesabu 18:26-29 Makuhani Walawi waliamurishwa walipe fungu la kumi kutokana na fungu la kumi ambao watu waliwatolea.

 

Himizo: Mchungaji na wahuduma na wote ambao kanisa linawalipa mshahara nao wanapaswa walipe fungu la kumi kutoka kwa mshahara wao.

Luka 18:12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma;hutoa zaka katika mapato yangu yote.

(Mfarasayo  alilipa fungu la kumi ,mtoza ushuru hakulipa,lakini akahesabiwa haki.)

 

Luka 12:32-34 Msiogope ,enyi kundi ndogo;kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka . Jifanyieni mifuko isiyochakaa,akiba asiopungua katika mbingu ,mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu. Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapo waponya mioyo yenu.

 

Matendo ya mitume 20:35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge,na kuyakumbuka maneno ya bwana Yesu jinsi alivyosema mwenyewe ,heri kutoa kuliko kupokea.

 

 Wefeso 4:28 Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi ilyo nzuri kwa nikono yake mwenyewe,apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

 

Wafilipi 4:19 Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachohitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo.

 

Mathayo 6:3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wa kuume;

 

Mathayo 6:1 Angalieni msifanye wemw wenu machoni pa watu, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani ,ili watukuzwe na watu.

 

Mathayo 5:42 Akuombaye, mpe;naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

 

Kuiba pesa za kanisa na mwisho kuingia jehenamu kwa sababu ya pesa.

 

Yuda Iskariote alipotezwa milele kwa sababu ya kupewa pesa na akawa mwizi na msaliti kwa fedha thelathini.

 

KUHUSU KUCHUKUA FAIDA

 

Zaburi 15:5 Hakutoa fedha zake apate kula riba,Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.

Mtu atandaye mambo hayo Hataondoshwa milele.

 

Kutoka22;25 Usikopeshe mtu aliye maskini, katika watu wangu waliopamoja nawe, usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai;wala hutamwandikia faida.

 

Mithali28;8` Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

Hazina zilizofichika.

 

Isaya 45: 3 Nami nitakupa hazina za giza, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Isreali.

 

2 Wakorintho 9:10 Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;

 

Isaya 33:6 Nyakati zako zitakua nyakati za kukaa imara ;za wokovu tele na hekima na maarifa ;kumcha BWANA  ni hazina yake ya akiba.

 

Zaburi 119: 127 Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi.

 

Mhubir 5:10 Apandaye fedha atavuna fedha, Wala apandaye wingi hatashiba maongeo. Hayo pia ni ubatili.

 

Mhubiri 5: 12 Usingizi wakekibarua ni mtamu, kwamba amekula kingi ;lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.

 

Mhubiri 5:13 Kuna na balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima.

 

Mhubiri 5:19 Tena, kwa habari za kila mwanadamu,ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake na kuhifurahia mali yake ;hiyo ndiyo karama ya Mungu.

 

Mathayo 6:25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini,wala miili yenu, mvae nini. Maisha je? si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

 

Mithali 23:4 Usijitaabishe ili kupata utajiri Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe.

 

Mathayo 6:24 Haku mtu awezaye kutumikia mabwana wawili ;kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu na kumdharahu huyu .Huwezi kumtumikia Mungu na mali.

 

1Timotheo 6:10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenad fedha, amabayo wengine hali wakiitamani  hiyo wamefarakana na Imani,na kujichoma kwa maumivu mengi.

 

Kuhusu kulipa ushuru.

 

Mathayo 22;21na Marko 12;17 na Luka 20:25 Akawaambia ,Basi vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu.

 

Warumi 13:7 Wapeni wote haki zao mtu wa kodi, kodi, mtu wa ushuru, astahili hofu hofu, astahili heshima,heshima.

 

Luka 16:10-13 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana huwa mwaminifu lililo kubwa pia . 11, Basi kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu ni nani atakaye wapa amana mali ya kweli.12, Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? 13, Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

 

Maandiko zaidi kuhusiana na pesa.

 

Mithali 22:1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi;na nehema kuliko mali na fedha.

 

Mhubiri 5:10 Apendaye fedha atashiba fedha wala apendaye wingi hatashiba maongeo.

 

Mhubiri 5:12 Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au ;au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumachi kulala usingizi.

 

Zaburi 119:127 Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, kuloko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi.

 

Mithali 23 :4  Usijitaabishe ili kupata utajiri Achakuzitegemea akkilil zako mwenyewe.

 

Mathayo 6:24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili;kwa maana atmchukia huyu na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu na kumchukia huyu,huwezi kumtumikia Mungu na mali.

 

19. Hatua muhimu katika Barabara ya kutoka kwa umasikini kuingia utele.

 

Kuwaza kama mtu aliye na mali.

 

Badilisha hali yako ya kufikiria juu ya mambo yahusuyo pesa.

 

Weka upya mawazo yako kwa kusoma neno la Mungu Kujifunza bibilia.

 

Fanya mabadiliko katika mtindo wa ulimwengu ingie njia za Mungu.

 

Elewa kanuni za kiungu ya kupanda na kuvuna.

 

Lipa fungu la kumi kwanza si mwishowe.

 

Lipa fungu la kumi kwa kanisa lako la nyumbani.

 

Mpende Yesu zaidi ya pesa zako Yule tajiri mdogo hakupenda Luka 18:23.

 

Anza kupanda -kwa wingi ama kidogo- haijalishi, lakini panda kila wakati , fanya iwe sehemu ya maisha yako.

 

Anza kuweka katika hazina ya soko la mbinguni na ufanye kwa furaha.

 

Jifunze nafasi iliyo sawa juu ya kutoa na kutumia pesa.

 

Tumia mpango wa mda mrefu. Hakikisha umejiokoa kutokana na laana.

 

Jifunze jinsi ya kupokea pesa kiutaraji bila kuadhiri nafsi yako.

 

Uwe na Imani na utumie Imani katika uchumi.