Condition on revival and preparation for revival

 

Masharti ya ufufio na kujiandaa kwa ufufio

Index                 

                                                                               By Vagn Rasmussen  Translation by Lawrence Chepkwony

 

Kuna aina nyingi za ufufio.

 

Unapokea aina ya ufufio unayoiombea  na kupokea unachohitaji kwa  imani .

 

Ufufio inaweza kuwa ya mashinani au ya taifa nzima, ufifuo waweza kuwa wa muda mfupi au muda mrefu.

 

Ufifuo huanzwa na mtu au Roho mtakatifu.

 

Utafsiri wa Biblia katika lugha ya kijerumani na Martin Luther ilileta Ufufio la neno na kusababisha

mabadiliko makuu ya ufufio.

 

 

Wesley alisababisha utakaso wa ufufio na kuinuka kwa kanisa la kimethodisti.

 

William Booth alianzisha kazi ya msaada na  utumizi wa uimbaji iliyogeuzwa kuwa nyimbo za kiroho .

 

Kanisa la ubatiso liligundua ubatiso wa maji iliyokuwa imefifia.

 

Wapentekoste wakagundua Roho Mtakatifu na kunena kwa ndimi pia karama za Roho katika kanisa ambazo zilikuwa zimefifia.

 

Kanisa la mitume likaanzisha huduma zaidi chache za uinjilisti, uchungaji, ualimu,  unabii na la kimitume.

 

Kuanzia hapo tukatazama makanisa yakisisitiza vitu vya kiroho, kucheka kwa roho ,uangusho wa roho.

baraka za Toronto, Uongozi wa imani, huduma ya akina  mama, kuoshwa  miguu, kusisitiza kuabudu na          mengine mengi.

 

Aina nyingi za ufufio imesabisha sana dunia katika miaka elfu mbili zilizopita .

 

Aina gani ya ufufio inayokuja  nyakati za mwisho, mavuno ya mwisho ?

 

Unavuna unapopanda!  aina ya ufufio tunayopanda (kuhubiri) ndicho tutavuna!

 

Amua aina ya ufufio unayoitaka.

 

Mungu yu tayari kutumia mtu yeyote aaminiye ili kunia ufufio.

 

Mungu yu tayari kutuma ufufio kwa kanisa yeyote

 

 

Ahadi za mungu wakati wote huwa na masharti.

 

Masharti mazuri yakiwepo, mungu atatuma ufufio lakini wachache sana huambatana na masharti haya ,pia wachache watalipa gharama yenyewe.

 

Ingawa kuna aina nyingi za makanisa na imani yao kiroho na kimwili, hapa kuna vipengele  28 ambazo ni lazima iwepo  katika kanisa la ufufio. Angalau kwa kiwango fulani

 

Kufikia kiwango cha  utayari kwa ufufio.

 

  1. Uhusiano wa dhati

            Kanisa kama familia

            Watu kuwa na imani  kwa mchungaji

 

 

    11    Upendo wa mchungaji kwa watu

            Hata kuteremka chini kwa watoto

            Kushirikiana hata katika machungu yao na shidazao.

 

    111   Mchungaji mpya (au kanisa mpya -ni nadra sana kuwa na ufufio katika makanisa ya kale')

            Mchungaji wa kanisa la ufufio si mzee, na sio mgeni aingiapo (sio  aliyezaliwa upya)

            Mchungaji ana mwito wa kiungu na maono kutoka kwa Mungu.

            Mchungaji ataleta kitu kipya katika kanisa

 

 

 

     1V  Kuachilia vitu vya kale

            Mchungaji katika kanisa la ufufio hatafuata  washirika wazee na utamaduni katika kanisa.

            Kuachilia uongozi kwa kila kiwango (Tazama funzo la uongozi).

 

     V   Fafanua kufikia

            Mchungaji atafafanua aina za ufikishaji / kufikia.

            Mchungaji ana mpango rahisi ya ufikishaji.

            Aina tofauti ya ufikishaji kutoka kanisa hadi kanisa lingine.

            Kanisa linasimama na mchungaji na kupokea maono yake

 

  Wachungaji wenye maono hujulikana wa maana.

 

VI Andaa washirika

            Karama za roho. (kanisa lenye ufufIo lazima iwe lenye kuchechemka)

 

            Kujazwa na Roho Mtakatifu kwa ndani, hubadilisha mdundo wa moyo wa kanisa.

 

 VII   Mazoezi ya kiroho.

            Moyo uliopondeka na toba.

 

            Uwepo wa roho wa maombi ni wa maana sana, na lazima angalau iwepo kwa baadhi ya wahirika       

            kanisani wa roho wa maombi, hakuna ufufio.

                         

            Maombi

 

            Kufunga

 

            Weka ratiba ya maombi. kutubu dhambi za taifa. Kumbukumbu la torati 7;14, Danieli 9:3-5 Luka           

            4:3-5

 

            Kila mshiriki lazima awe mfuaji wa nafsi.

 

            Huruma kwa nafsi zilizopotea.

 

    VII   Mahubiri yenye uzito.

 

            kurudi kwa mambo ya msingi.

 

            Injili kamilifu, sio sehemu ya neno.

 

     IX  Msaada ya watenda kazi ni muhimu.

 

     X    Kikundi wenye kujitolea.

 

            Kamati ya wazee na watenda kazi.

 

      X   Uzito wa kuabudu.

            Jinsi ya kupima hali ya kiroho katika kanisa ni kusikiliza kuabudu.

 

            Nyimbo mpya na za kale sikwa sawa.

 

            Mtindo usio mgumu sana.

 

            Kila ufufio mpya huleta nyimbo mpya za ufufio.

 

      XII Kasi ya pesa.

            Pesa sio ya maana ili kuwe na ufufio.

 

            Pesa haziwezi kuchangia iwapo kuna ukosefu wa Roho mtakatifu.


            Pesa haiwezi kuchukua nafasi ya upako wa Roho Mtakatifu.

          

            Hasira ya viongozi, kutoaminiwa  hasa katika mahali pa pesa inazuia roho ya ufufio.

 

 XIII. umoja inahitajika.

            Hakuna mwanya katika kizazi.

            Umoja katika baraza la wazee 

 

 XIV Kuwa tayari kupokea mabadiliko kanisani.

 

XV. Mapatanisho katika sehemu zote.

            Wazazi/Watoto

            Kisasi kipya na ya zamani kanisani.

            Waliotalakiana wanaporejeana

            Mapatanisho na makanisa mengine n.k

 

XV. Ugomvi wa madhehebu na utengamano lazima iondolewe. kanisa moja tu machoni pa Mungu.

 

XVI. Imani katika ufufio lazima ienezwe  kanisani . washirika kutarajia ufufio katikati yao.

 

XVII. Huruma kwa  wenye dhambi lazima iwepo

 

XVIII. Kukubali  kulipa gharama, kama vile kukaribisha shida kanisani kwa njia ya ufufio. Kuvumilia kwingi lazima iwepo.

kufutlia mbali wasiwasi wa kiroho na pia kiburi maishani mwetu.

 

XIX. Utumizi wa vipawa vya wanawake na huduma zao imeshauriwa.

 

XX. Shida ya rangi lazima iondolewe /kuangamizwa .Makabila wakaribishwe katka kanisa wa ufufio.

 

XXI. Kuongoza ufufio.

         1. Mipangilio mwafaka katika mikutano ya ufufio.2-5.

 

         2.Mwito wa kuombea watu katika kila mkutano wa ufufio.

 

         3. waombezi kuenda kuomba wakati wa mkutano.

 

         4. Wahubiri waliopakwa mafuta.

 

         5. Ibada iliyopakwa

 

         6.Kazi ya kuwafwatilia ni lazima.

 

XXII. Kujitolea kwa mtu binafsi wakati wa ufufio (  mazoezi  ya kibinafsi ya kiroho)

 

           Kufungua na kuomba ni lazima hasa baadhi ya washiriki wa kanisa

 

           Kuwa tayari kwa mateso, waliopoteza upako watatesa walio na upako.

 

           ufufio wa hapo awali utateza na kuzuia ufufio unaoendelea sasa.

 

Ufufio inaanza na mimi -Nifanyaje ili niwe chombo katika mkono wa Mungu kwa ufufio ijayo?

 

1. Maombi Roho ya maombi – Usafishaji kiroho, dhambi  iliyotendwa kwa kujua na kutojua.

 

            Maisha ya maombi ya lazima ibadilishwe.

 

            Kupatia maombi nafasi ya juu.

 

            Kukiri, toba, kuacha, utakaso.

 

            Uombezi, kusimama kwenye pengo.

 

            Kufunga milango, elimu za upotofu n.k.

 

            Uzidisho wa tunda za Roho -omba.

 

            Silaha kamili ya Mungu.

 

            Kuwa na huruma  kwa wenye dhambi.

 

            Kuabudu katika roho na kweli.

 

            Ombi la Bwana.

 

            Amri kumi

 

2. Mtindo wa kufunga.

 

3. Vita vya kiroho.

 

            Ufuniko chini damu ya yesu.

 

            Usafishaji kiroho hasa uambudu wa miungu.

 

            Kufunga (kufunga iliyotakaswa)

 

            Maombi -wakati mwingine kukumbana ana kwa ana  na vita .

 

            Kuabudu kwa roho na kweli.

 

Kumbuka hauwezi kuzaa au kuiga 'Uchungu wa kuzaa'' Roho Mtakatifu ndiye  awezaye kufanya hivyo.

 

Ukiiga basi litakuwa la kimwili wala sio ya Roho mtakatifu.

 

Maongezi ya ndimi inachochewa tu na Roho mtakatifu, na hauwezi kuamuru au kuzuia Roho mtakatifu, La sivyo utamhuzunisha Roho mtakatifu.

 

Kwa upande mwingine mori ya maombi ikiwepo juu yako na unahisi nguvu ya huruma/uguzo kwa wale waliopotea usipoteze kamwe bali itunze , Ni wakati huo wa utakatifu unaweza kuwa na ushindi mkubwa na kufanya kazi ya Mungu vyema.

 

Kuomba na maombezi ukiogozwa na Roho wa maombi' itakufanya uwe na ujasiri kama simba na inapotokea basi itakufanyaumsihi Mungu awarehemu wenye dhambi kwa kuwaokoa.

 4.Nia:-    Lazima uwe na nia njema ili kuinua ufufio.

            Matarajio : weka kila matarajio ya kibinafsi chini

            Wacha kumcha na kumpenda Baba na mwana iwe usukumo maishani mwako

            Kuwa na upendo na huruma kwa wenye  dhambi.

 

 5.Maisha ya familia na ndoa.

            Umuhimu :- Mungu kwanza ,familia ya pili tatu huduma yako kwa Bwana

 

6.Uchumi kuwa na mazoezi ya nidhamu.

 

7.Haki:- kuwa na ukweli ,haki kwa vitu vyote  katika fedha katika maongezi vitendo kwa mwenzio ,watoto wapendwa , watenda kazin.k

 

8. Upenyezo katika neno la Mungu.

            Kusoma bibilia Majarida na vitabu yv akikristo

            Mawasilia/vyombo vya mawasiliano

 

9. Kutii na kumcha Mungu.

 

10. usiwahi kuchukua utukufu na heshima kutoka kwa Mungu bali nyenyekeeni kwa Mungu

 

XXIII. Vizuizo vya ufufio.

 

Kuwepo kwa roho ya kidunia, utamhusunisha Roho wa ufufio na itatoweka.

 

Nia mbovu za wachungaji, matarijio kwa viongozi wasio na ukweli katika ufufio.

.

Wachuangaji wanapoinua viburi vyao kanisani itamkwaza Roho Mtakatifu na ataondoka.

 

Ukosefu wa Roho wa maombi itafanya maombi kufifia.

 

Kutowafuata waliopokea wokovu, waliopokea wokovu kuachwa peke yao.

 

Hakuna kanisa inayojitolea kwa moyo wote.  Hatuwezi kutarajia kufaulu katika kuinua ufufio wa kweli kama sisi (kanisa) wenyewe hutuna ufufio ndani yetu.

 

XXIV Ujazwe na Roho mtakatifu waefeso 5. 18.

 

XXV Roho wa maombi   Zech 12 :10 na warumi 8: 26

 

XXVI Umwagaji wa roho mtakatifu kama siku ya pentekote inahitajika, kusababisha ufufio wa kudumu pia umwagaji wa Roho na moto.

 

Yesu akasema  "mtapokea nguvu, baada ya Roho mtakatifu kuja juu yenu ,na mtakuwa mashahidi wangu judea, samaria na sehemu zote za duniani''.(matendoya mituma1:8).

 

Ukosefu wa moto wa ufufio, ambayo ni moto wa Roho Mtakatifu,basi ni ukosefu wa ufufio.

 

XXVII Moyo uliyopondeka na roho wa maombi, vyote viwili vinahitajika kuwepo katika ufufio, katika kuinua ufufio, viongozi lazima wawe wamebondeka, katika mioyo  yao na roho zao.

 

Zaburi 51:17 Dhabihu ya Mungu ni  moyo na roho uliobondeka, ee Mungu hautaidharau.

 

XXVIII. "Ratiba" inaweza kukusababisha kuacha mwelekeo wa ufufio, na  kutomtazama Yesu.

 

            Wapangaji wazuri na viongozi walio imara  hujaribiwa.

 

            Wapangaji wazuri na viongozi walio imara, mara nyingi humpinga Roho Mtakatifu, hasa wakati                                         

             wa ufufio.

 

            Wapangaji wazuri hawamtegemei Roho mtakatifu. Mwenye ujuzi katika mipangilio

            mara nyingi huegemea uwezo wake zaidi kuliko kuegemea Roho mtakatifu.